Pre GE2025 Dkt. Slaa: Minyukano ya kambi za uchaguzi wa Mwenyekiti (Mbowe & Lissu) CHADEMA, sababu ni Mbowe anataka kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kusema Lissu ni myopic ni kumkosea heshima. Si lazima yeye na wewe myaone mambo yote katika mtazamo unaofanana.

Unapoona kuna maeneo anaweza kufanya vizuri zaidi si vibaya ukitoa ushauri kama mzalendo, japo wewe ni wa upande mwingine kichama (sijasema kiitikadi, siku hizi vyama vyetu havina itikadi). 😀 😀
Mkuu Gagi,@gagnija,mypic ni kushindwa kuona mbali!,no election ni kitu kisichotekelezeka,utopia!,nguvu itakayotumika kuzuia uchaguzi,ingetumika kujipanga,Chadema ingetusua kwa ulaini kama kuokota dodo chini ya mwembe!。

Nilipokuwa kule,nikaiona fursa,nikaitangaza humu Inawezekana Wamarekani ni wajinga ajabu? Wamemchagua mwanaume na kumtosa Mwanamke. 2025 Watanzania tuchague mwanamke kuonesha tuna akili zaidi yao? kisha nikashauri Kilichotokea Uchaguzi wa Marekani, kinaweza kutokea Uchaguzi 2025?. Tuyatumie matokeo yao kama shamba darasa la 2025 au wao ni wao, na sisi ni sisii?

P
 
Japo nimemtangulia darasa na vidato,ila amenizidi akili,TAL ni akili mingi ila maarifa ni issue kidogo!,mimi nimemzidi kidogo maarifa!。 Mfano,juzi kati nilikuwa US kuangalia uchaguzi wao mkuu,kuna kitu nime observe,ambacho unashabihiana na Uchaguzi。wetu wa 2025 TAL,akikijua, ni bonge la fursa kwake kuichangamkia na kuachana na hayo ma utopia yao,ila yeye mwenzangu hajaiona hiyo fursa, Chadema hawajaishtukia, they are simply mypic due to having myopia,just too blind to see!。
P
Mkuu p hakuna cha fulsa ,acha kutupanga hivi sheria za USA za uchaguzi na Tz mbona ni mbingu na ardhi, hadanganyiki mtu ,no reforms no election
 
Fuatilia kwa umakini minyukano ya siasa za uchaguzi wa Mwenyekiti CHADEMA Taifa utakaofanyika tarehe 21/01/2025 inayoendelea ndani ya chama hiki kisha husianisha na matukio haya👇..

TUKIO #1: Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea u - Rais wa JMT 2025 iwapo chama chake kitampa ridhaa. Asema, tayari ameshaiweka nia yake hiyo kwa barua (maandishi) na kuiwasilisha kwa katibu mkuu.

TUKIO#2: Sambamba na kuweka wazi nia yake kugombea u - Rais wa JMT, TL pia atangaza kusudio lake la kuwania Umakamu mwenyekiti wa CHADEMA kwa awamu ya pili 2024 - 2025..

TUKIO #3: Ghafla, Tundu Lissu aondoa kusudio lake la kuwania Umakamu mwenyekiti wa CHADEMA na badala yake kutangaza kuwania nafasi ya juu zaidi (Uenyekiti) wa CHADEMA...

TUKIO #4: Tundu Lissu apokea vitisho vya kuuwawa tena kama ilivyokuwa mwaka 2017 alipopigwa risasi 37. Anasema mtu muhimu na mzito sana ndani ya serikali kampa siri ya mipango inayosukwa na kikosi kazi cha siri ndani ya serikali. Aambiwa achukue tahadhari zote kwa usalama wake. Aanza kuvaa "bullet proof" kila anapokuwa ktk shughuli zake za nje.

TUKIO #5: Katibu mkuu John John Mnyika, atangaza rasmi tarehe ya uchaguzi, kuchukua na urejeshaji fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi mbali ndani ya chama ikiwemo Uenyekiti Taifa. Tundu Lissu siku ya kwanza tu aenda kuchukua fomu na kesho yake akalipia 1,500,000 (pesa ambayo anasema ilitolewa na mwanaharakati Sativa kama njia ya kumsapoti)

TUKIO #6: Wanaosemekana wafuasi na wapenzi wa M/Kiti kadhaa wafika kwake kwa kile walichodai kumshawishi achukue fomu Ili naye agombee (atetee nafasi). Asita kukubali siku hiyo. Awaambia wasubiri, atafakari kwanza aone mambo yanavyokwenda na akiona "chama chake kinaparanganyika, ataingia mzigoni" na masaa 48 atakuwa analo jibu. Masaa 48 yakaisha, akatoa jibu la NDIYO na kutangaza rasmi kuwa atachukua fomu na kutetea kiti chake...!

TUKIO #7: Freeman Mbowe baada ya siku kadhaa kuwa kimya, aonekana kwenye kituo kimoja cha TV ya matandaoni (Online TV) akifanya mahojiano na mwandishi wa habari maarufu Salimu Kikeke. Mahojiano yake hayo yanazua maswali mengi. Anasema, haelewi ni kwanini Makamu wake (Tundu Lissu) ameamua kugombea uenyekiti kwa kuwa walikaa, wakazungumza na kukubaliana. Hakuweka wazi walizungumza na kukubaliana nini. Anamshauri mwandishi aende akamuulize swali hili Tundu Lissu, maana yeye hana jibu. Japo hakusema wazi, lakini inawezekana makubaliano yao ni "NANI AWE MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA" tena 2024 - 2029...

TUKIO #8: Hili ndilo msingi mkuu wa mjadala huu na hayo mengine yote yatakuwa ni rejea.

Katika audio video hiyo👆👆, ni Dr Wilbroad Slaa (Balozi) akiwa kwenye mjadala wa Moja ya Club 🏠 House mtandaoni akichambua hoja za Freeman Mbowe ktk interview ile ya kwenye Online TV....

Dr Slaa anasema, kiini cha vita hii ya siasa za madaraka ya uongozi kati ya FREEMAN MBOWE na TUNDU LISSU, ni kwa sababu mapatano ya Samia na Mbowe ni kuwa, yeye Freeman Mbowe ndiyo agombee u - Rais ktk uchaguzi mkuu mwaka huu 2025 kwa tiketi ya CHADEMA na sio Tundu Lissu. Mama Abdul atatoa mapesa mengi kwa CHADEMA na watapata/achiwa/shindishwa kwenye majimbo kadhaa ya ubunge...!

✓ Inasemekana Moja ya makubaliano ya kilichoitwa "maridhiano" ni Freeman Mbowe kuhakikisha Tundu Lissu "anatoka katika picha" kabisa ya CHADEMA kwa kutokuwa na nafasi yoyote ya uongozi. Sasa anza kuunganisha dots:

✓ Ndiyo maana TL aliwekewa Hezekiah Wenje apambane naye kwenye nafasi ya Umakamu mwenyekiti. System ingehakikisha Wenje anashinda iwe mvua au jua huku Freeman Mbowe naye akiwa mgombea pekee au akiwekewa mshindani dhaifu kwenye Uenyekiti..

✓ Tundu Lissu akatonywa mkakati huu, akaambiwa, mfuate huko huko juu naye akajibu "sasa nampandia huko huko juu", kwenye Uenyekiti....

✓ Kwa mujibu wa Dr Wilbroad Slaa, ni kuwa mapatano ya Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa JMT na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA) kwenye "maridhiano" yao ni:
Moja; Ni kuhakikisha Tundu Lissu hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na ikibidi afukuzwe uanachama kabisa. Kwa njia hii hatakuwa na jukwaa la kusemea.

Pili, kuhakikisha yeye Freeman Mbowe ndiye anakuwa mgombea u - Rais wa CHADEMA na siyo Tundu Lissu. Lengo sio Mbowe ashinde bali kutoa unafuu wa Samia Suluhu na CCM kushinda kilaini. Mtu kama Tundu Lissu kwa ushawishi alionao kwao CCM na Samia wao ni hatari, atakuwa anawalaza na viatu...

##Sasa unaweza kuelewa ni kwanini TL mara kwa mara anayaponda maridhiano hayo na kusema wazi "Kuna mengi nyuma ya pazia ambayo Mwenyekiti huwa hawaambii wenzake kwenye hii kitu inayoitwa maridhiano..."

✓Pamoja na mikakati na figusufigisu hizi zinazoendelea ndani ya CHADEMA kuhakikisha TL "is out of the picture" kwa vihoja vya mara oh anatoa siri za chama, mara ooh hana busara, au amevunja na kukiuka katiba au mara hivi au vile; ieleweke tu kuwa, yote haya ni harakati za kujaribu kumjengea hoja ya "kumkosesha sifa ya haki ya kugombea uongozi na uanachama" Ili lengo na kusudi la kumtoa ktk chama (to take him out of the picture) litimie, ili CCM na Samia wao wapumue..!

✓ Lakini pia moja ya "option" iliyosukwa kama njia hizi za ndani ya chama zinashindikana, ni kumuua kabisa au kumdhuru au kumjeruhi vibaya kabla ya uchaguzi Ili atumie muda mwingi kujiuguza hospitalini, akitoka huko akute mwana si wake.

✓ Huu mkakati wa kumdhuru TL unasukwa na "wasiojulikana" ndani ya serikali/CCM na wengine wako ndani ya CHADEMA na Freeman Mbowe anajua fika.

Sasa unaweza kuelewa ni kwanini Team Campaign ya Freeman Mbowe ni wakali na wanahakikisha yanakuwa kama ilivyopangwa iwe jua au mvua kwa sababu ya ahadi walizopewa ikiwemo viti kadhaa vya ubunge, fedha za kampeni ya u - Rais nk

Aidha unaweza sasa pia kuelewa ni kwanini Chawa wa Freeman Mbowe wanatumia kauli au kigezo cha fedha kama turufu yao. Kwamba, hata akiwa Mwenyekiti huyu TL atatoa wapi pesa za kuendesha chama, kampeni ya u Rais nk iwapo TZS 30,000,000 tu za kuchangia gharama za mkutano mkuu wa uchaguzi ameshindwa kutoa. Msingi wa hoja hii, ni kuwa, wao wanategemea pesa za Abdul na mama yake alizohongwa na waarabu DP World na Oman kwa kuwapa rasrimali asili zetu bandari, misitu na mbuga za wanyama..!!

Sharti ni Moja tu: Mdhibitini huyu bwana.....Tundu Lissu

Mungu mkubwa. Kama Mbowe angerejea kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti wa CDM, kazi ya kwanza ilikua ni "KUMSHUGHULIKIA" TAL, na kwa bahati sote tulishuhudia katika majadiliano yake yote Sultan Mbowe alikuwa akiahidi kazi yake ya kwanza itakuwa ni "kushughulikia wavunja katiba" kwenye chama chake.

Sasa kwisha habari yake, ni kama AMEJIFUKUZISHA mwenyewe.
 
Mkuu Gagi,@gagnija,mypic ni kushindwa kuona mbali!,no election ni kitu kisichotekelezeka,utopia!,nguvu itakayotumika kuzuia uchaguzi,ingetumika kujipanga,Chadema ingetusua kwa ulaini kama kuokota dodo chini ya mwembe!。

Nilipokuwa kule,nikaiona fursa,nikaitangaza humu Inawezekana Wamarekani ni wajinga ajabu? Wamemchagua mwanaume na kumtosa Mwanamke. 2025 Watanzania tuchague mwanamke kuonesha tuna akili zaidi yao? kisha nikashauri Kilichotokea Uchaguzi wa Marekani, kinaweza kutokea Uchaguzi 2025?. Tuyatumie matokeo yao kama shamba darasa la 2025 au wao ni wao, na sisi ni sisii?

P
Bwana Paskali sisi sio watoto, upinzani unawezaje "kufanya vizuri" kwenye uchaguzi kupitia mifumo hii tuliyonayo ya CCM?
Uchaguzi mkuu ukifanyika katika mifumo hii hii tuliyonayo, matokeo yake yatakuwa ya HOVYO KABISA kuliko hata yale ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

Acha utoto.
 
Katiba ya CDM isifuatwe kwa sababu ni mwiba mchungu kwa Lissu? Hilo haliwezekani na halitafanyika.

Hao wanachama wanaomtaka Lissu ilipigwa kura ya maoni lini na wanachama wote walijulishwa ili washiriki?

Wacha Lissu ashindwe aondoke CHADEMA kama ni asset basi hao wanaomtaka watampigia kura huko huko atakakotimkia sio lazima iwe ndani ya CHADEMA.
We TAPELI upo?
 
Bwana Paskali sisi sio watoto, upinzani unawezaje "kufanya vizuri" kwenye uchaguzi kupitia mifumo hii tuliyonayo ya CCM?
Uchaguzi mkuu ukifanyika katika mifumo hii hii tuliyonayo, matokeo yake yatakuwa ya HOVYO KABISA kuliko hata yale ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

Acha utoto.
Wakati Dodoma wanajipitisha kugombea urais na kumpa mzee Wasira umakamu mwenyekiti, walijua wameshamaliza kazi kwenye uchaguzi wa chadema, wakijua mtu wao atapita kwa kishindo.

Ilifanyika juhudi kubwa kwa upande wa Lissu kuzuia hujuma zozote ambazo zingefanywa kuvuruga uchaguzi. Ushindi wa Lissu uliwaacha na mshangao mkubwa hadi leo.
 
Kwa kweli ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa CCM na magenge yake yote.
 
Fuatilia kwa umakini minyukano ya siasa za uchaguzi wa Mwenyekiti CHADEMA Taifa utakaofanyika tarehe 21/01/2025 inayoendelea ndani ya chama hiki kisha husianisha na matukio haya👇..

TUKIO #1: Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea u - Rais wa JMT 2025 iwapo chama chake kitampa ridhaa. Asema, tayari ameshaiweka nia yake hiyo kwa barua (maandishi) na kuiwasilisha kwa katibu mkuu.

TUKIO#2: Sambamba na kuweka wazi nia yake kugombea u - Rais wa JMT, TL pia atangaza kusudio lake la kuwania Umakamu mwenyekiti wa CHADEMA kwa awamu ya pili 2024 - 2025..

TUKIO #3: Ghafla, Tundu Lissu aondoa kusudio lake la kuwania Umakamu mwenyekiti wa CHADEMA na badala yake kutangaza kuwania nafasi ya juu zaidi (Uenyekiti) wa CHADEMA...

TUKIO #4: Tundu Lissu apokea vitisho vya kuuwawa tena kama ilivyokuwa mwaka 2017 alipopigwa risasi 37. Anasema mtu muhimu na mzito sana ndani ya serikali kampa siri ya mipango inayosukwa na kikosi kazi cha siri ndani ya serikali. Aambiwa achukue tahadhari zote kwa usalama wake. Aanza kuvaa "bullet proof" kila anapokuwa ktk shughuli zake za nje.

TUKIO #5: Katibu mkuu John John Mnyika, atangaza rasmi tarehe ya uchaguzi, kuchukua na urejeshaji fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi mbali ndani ya chama ikiwemo Uenyekiti Taifa. Tundu Lissu siku ya kwanza tu aenda kuchukua fomu na kesho yake akalipia 1,500,000 (pesa ambayo anasema ilitolewa na mwanaharakati Sativa kama njia ya kumsapoti)

TUKIO #6: Wanaosemekana wafuasi na wapenzi wa M/Kiti kadhaa wafika kwake kwa kile walichodai kumshawishi achukue fomu Ili naye agombee (atetee nafasi). Asita kukubali siku hiyo. Awaambia wasubiri, atafakari kwanza aone mambo yanavyokwenda na akiona "chama chake kinaparanganyika, ataingia mzigoni" na masaa 48 atakuwa analo jibu. Masaa 48 yakaisha, akatoa jibu la NDIYO na kutangaza rasmi kuwa atachukua fomu na kutetea kiti chake...!

TUKIO #7: Freeman Mbowe baada ya siku kadhaa kuwa kimya, aonekana kwenye kituo kimoja cha TV ya matandaoni (Online TV) akifanya mahojiano na mwandishi wa habari maarufu Salimu Kikeke. Mahojiano yake hayo yanazua maswali mengi. Anasema, haelewi ni kwanini Makamu wake (Tundu Lissu) ameamua kugombea uenyekiti kwa kuwa walikaa, wakazungumza na kukubaliana. Hakuweka wazi walizungumza na kukubaliana nini. Anamshauri mwandishi aende akamuulize swali hili Tundu Lissu, maana yeye hana jibu. Japo hakusema wazi, lakini inawezekana makubaliano yao ni "NANI AWE MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA" tena 2024 - 2029...

TUKIO #8: Hili ndilo msingi mkuu wa mjadala huu na hayo mengine yote yatakuwa ni rejea.

Katika audio video hiyo👆👆, ni Dr Wilbroad Slaa (Balozi) akiwa kwenye mjadala wa Moja ya Club 🏠 House mtandaoni akichambua hoja za Freeman Mbowe ktk interview ile ya kwenye Online TV....

Dr Slaa anasema, kiini cha vita hii ya siasa za madaraka ya uongozi kati ya FREEMAN MBOWE na TUNDU LISSU, ni kwa sababu mapatano ya Samia na Mbowe ni kuwa, yeye Freeman Mbowe ndiyo agombee u - Rais ktk uchaguzi mkuu mwaka huu 2025 kwa tiketi ya CHADEMA na sio Tundu Lissu. Mama Abdul atatoa mapesa mengi kwa CHADEMA na watapata/achiwa/shindishwa kwenye majimbo kadhaa ya ubunge...!

✓ Inasemekana Moja ya makubaliano ya kilichoitwa "maridhiano" ni Freeman Mbowe kuhakikisha Tundu Lissu "anatoka katika picha" kabisa ya CHADEMA kwa kutokuwa na nafasi yoyote ya uongozi. Sasa anza kuunganisha dots:

✓ Ndiyo maana TL aliwekewa Hezekiah Wenje apambane naye kwenye nafasi ya Umakamu mwenyekiti. System ingehakikisha Wenje anashinda iwe mvua au jua huku Freeman Mbowe naye akiwa mgombea pekee au akiwekewa mshindani dhaifu kwenye Uenyekiti..

✓ Tundu Lissu akatonywa mkakati huu, akaambiwa, mfuate huko huko juu naye akajibu "sasa nampandia huko huko juu", kwenye Uenyekiti....

✓ Kwa mujibu wa Dr Wilbroad Slaa, ni kuwa mapatano ya Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa JMT na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA) kwenye "maridhiano" yao ni:
Moja; Ni kuhakikisha Tundu Lissu hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na ikibidi afukuzwe uanachama kabisa. Kwa njia hii hatakuwa na jukwaa la kusemea.

Pili, kuhakikisha yeye Freeman Mbowe ndiye anakuwa mgombea u - Rais wa CHADEMA na siyo Tundu Lissu. Lengo sio Mbowe ashinde bali kutoa unafuu wa Samia Suluhu na CCM kushinda kilaini. Mtu kama Tundu Lissu kwa ushawishi alionao kwao CCM na Samia wao ni hatari, atakuwa anawalaza na viatu...

##Sasa unaweza kuelewa ni kwanini TL mara kwa mara anayaponda maridhiano hayo na kusema wazi "Kuna mengi nyuma ya pazia ambayo Mwenyekiti huwa hawaambii wenzake kwenye hii kitu inayoitwa maridhiano..."

✓Pamoja na mikakati na figusufigisu hizi zinazoendelea ndani ya CHADEMA kuhakikisha TL "is out of the picture" kwa vihoja vya mara oh anatoa siri za chama, mara ooh hana busara, au amevunja na kukiuka katiba au mara hivi au vile; ieleweke tu kuwa, yote haya ni harakati za kujaribu kumjengea hoja ya "kumkosesha sifa ya haki ya kugombea uongozi na uanachama" Ili lengo na kusudi la kumtoa ktk chama (to take him out of the picture) litimie, ili CCM na Samia wao wapumue..!

✓ Lakini pia moja ya "option" iliyosukwa kama njia hizi za ndani ya chama zinashindikana, ni kumuua kabisa au kumdhuru au kumjeruhi vibaya kabla ya uchaguzi Ili atumie muda mwingi kujiuguza hospitalini, akitoka huko akute mwana si wake.

✓ Huu mkakati wa kumdhuru TL unasukwa na "wasiojulikana" ndani ya serikali/CCM na wengine wako ndani ya CHADEMA na Freeman Mbowe anajua fika.

Sasa unaweza kuelewa ni kwanini Team Campaign ya Freeman Mbowe ni wakali na wanahakikisha yanakuwa kama ilivyopangwa iwe jua au mvua kwa sababu ya ahadi walizopewa ikiwemo viti kadhaa vya ubunge, fedha za kampeni ya u - Rais nk

Aidha unaweza sasa pia kuelewa ni kwanini Chawa wa Freeman Mbowe wanatumia kauli au kigezo cha fedha kama turufu yao. Kwamba, hata akiwa Mwenyekiti huyu TL atatoa wapi pesa za kuendesha chama, kampeni ya u Rais nk iwapo TZS 30,000,000 tu za kuchangia gharama za mkutano mkuu wa uchaguzi ameshindwa kutoa. Msingi wa hoja hii, ni kuwa, wao wanategemea pesa za Abdul na mama yake alizohongwa na waarabu DP World na Oman kwa kuwapa rasrimali asili zetu bandari, misitu na mbuga za wanyama..!!

Sharti ni Moja tu: Mdhibitini huyu bwana.....Tundu Lissu

hisia tupu
 
Mleta mada Umeandika kirefu tuhuma bila chembe ya ushahidi hakikika hata mmoja

Umejaza umbeya wa uswahilini mwanzo hadi mwisho
Nimekuwekea mpaka video za wahusika wakisema maneno yao...

Lakini cha ajabu wewe huoni wala kusikia...!!
 
Uongo mtupu mnajihami baada ya kuona Tundu anaenda kupotezwa katika ra.mani za kisiasa.

Lissu ilikuwa rahisi kwake kumshinda Wenje katika nafasi ya Umakamu kuliko kumshinda Mbowe katika nafasi ya m/ kiti hivyo hata kama amewekewa Wenje kama angetaka kubaki katika uongozi basi angepima ipi ni nafasi rahisi kwake kushinda na kugombea. Ni wazi akishindwa uenyekiti automatically atakuwa ametolewa katika uongozi na hiyo haimaanishi ni kwa sababu ya njama bali matokeo ya uchaguzi na hapo huwezi kumlaumu Mbowe.

Kuhusu kugombea urais Lissu aelewe hiyo siyo haki yake bali ni favour mtu yeyote anaweza kupewa hiyo fursa akawakilisha chama.

Kama anataka sana kugombea urais basi vipo vyama aombe agombee kutoka huko tuone kama atashinda.

Hoja yako ya urais ni mufilisi kabisa mtu yeyote timamu anajua CCM hawawezi kuuachia urais uchukuliwe na mtu nje ya CCM na yeyote anayegombea anajua hilo hata Lissu wako analijua hilo.

Faida pekee ya kugombea urais ni chama kupata ruzuku kubwa na wabunge wa viti maalum wengi kutokana na zile kura za urais atakazopata mgombea.

Lissu anajifuta mwenyewe katika siasa kwa kutengeneza uadui na viongozi wenzake ndani ya CHADEMA na option pekee iliyo salama akaanzishe chama chake atoke jasho kukijenga na itamchukua miaka na pengine asifanikiwe sana maana hana fedha .

Akijiunga na hivi vyama vilivyopo atapata fursa ya kugombea urais tu lakini cheo hawatampacna baada ya uchaguzi watamtosa.

Lissu amelikoroga mwenyewe.
Uko wapi ndugu RMC.....?

Una maoni yoyote au umelowa na umeamua kulamba vumbi moja kwa moja...?

Umeshajiunga na NO REFORMS, NO ELECTION; Tone Tone pamoja NA MIMI NIMO...?

Pole sana brother...
 
Katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa.

Lissu amemshinda Mbowe kwa margin ndogo ta kura 31.

Mbowe bado atabaki kuwa kiongozi bora aliyeijenga CDM.

No reform no election siwezi kujiunga nayo na mwisho wa hiyo slogan ni October 2025. Uchaguzi utafanyika kama kawIaida. Hata wewe hapo hautatoka nje ya key board kwenda kuzuia uchaguzi.
 
Kazi yangu ni kukumbusha tu. Hivyo, nitakukumbusha wakati wake ukifika...

Nevertheless, nimependa hoja yako Moja. Kwamba, kwenye uchaguzi kuna kushindwa au kushinda no matter the margin difference ya kura. Ushindi ni ushindi tu, au siyo ndugu RMC...?

Kikubwa na muhimu ni wapiga kura, mshindi na mshindwa waridhike na mchakato mzima wa uchaguzi kuwa, huu kweli ulikuwa uchaguzi huru, wa wazi na wa haki. Bila shaka kwa hili, tunakubaliana wote. Na kwa hhakika uchaguzi wa CHADEMA wa 21. 01. 2025 ulibeba sifa hizi zote ndiyo maana hakuna malalamiko....

Tuje kwa hoja na dhana nzima ya movement ya NO REFORMS, NO ELECTION inayoongozwa na CHADEMA...

Wewe unaonaje chaguzi za nchi hii? Kwanini zisifanyike kama huu wa CHADEMA tunaousifia? Huoni kuwa chaguzi za Tanzania zinaweza tu kuwa HURU, za HAKI na za WAZI iwapo tutakuwa na sheria na utaratibu mzuri wa kuzisimamia? Au wewe unaona mambo ni mazuri tu na chaguzi zetu Tanzania hazina shida yoyote...?

Hapa ninachotaka ujue ni kuwa hakuna anayesema kuwa uchaguzi hautafanyika..

No Reforms, No Election haina maana ya "uchaguzi usifanyike..."

Maana yake ni kuwa, tufanye uchaguzi lakini baada ya reforms kadhaa muhimu za kisheria na kikatiba kufanyika ili kuruhusu chaguzi Huru, za Wazi na za Haki kufanyika hapa Tanzania...

Na sababu ya kila mtu kutaka mabadiliko haya ni ili wewe RMC kura yako iwe kwenye hesabu na ihesabiwe kwani as for now, viongozi tulionao wanaongoza serikali kuu na za huku chini hawakutokana si ridhaa ya wananchi, Bali wamepachikwa tu....

Hawatukuwachagua, wako pale kwa chaguzi ambazo ni rigged and manipulated. Hii maana yake kura yangu na ya kwako chini ya mfumo huu wa chaguzi hata ukienda kupiga kura kuchagua kiongozi umtakae, haina maana wala thamani yoyote. Hebu nijibu toka moyoni mwako, kwamba, hivi ndivyo unavyotaka iwe...?

Kwa hiyo kubwa kuliko yote tunataka ,fumo wa kutupatia viongozi wa serikali waliochaguliwa kwa kura za wananchi si kama ilivyo sasa...!

Wewe hutaki hayo? Wewe hupendi na hutaki uchaguzi HURU, wa HAKI, na ulio WAZI? Ina maana hupendi haki na badala yake unapenda dhuluma ndugu RMC..?

Kwa hiyo hakuna asemaye tusiwe na uchaguzi kabisa. Uchaguzi utafanyika lakini si lazima iwe Oktoba, 2025 iwapo reforms tunazotaka hazitakuwa zimefanyika...

Uchaguzi mkuu utafanyika tu hata kama ni mwakani 2026 au 2027 only after all necessary legal and constitutional reforms are made...

Do you now understand? Do you agree that, as it stands now, free, fair and transparent elections in our country are absolutely impossible?

If you agree, why then hesitate to support this very crucial movement of NO REFORMS, NO ELECTION by CHADEMA in order to put pressure on the rulers to accept changes..?

And remember, the changes/reforms we all demand are for the benefits of all us as a nation, our children and the entire coming generations...

HAKI HUINUA TAIFA..
 
Japo sikubaliani na wewe katika baadhi ya hoja ulizozieleza lakini nakiri kuwa umejitahidi kujenga hoja objectively.

Mimi huwa siku zote nachangia hoja objectively siyo subjectively.

Nimekuwa nikishiriki uchaguzi tangu mwaka 1985 na sijawahi kukosa kupiga kura na mwezi oktoba 2025 nitapiga kura.

Ninafahamu kuwa uchaguzi wa mwisho katika nchi hii ulifanyika mwaka 2015 japo haukukidhi viwango kwa asilimia 100 lakini walau matokeo ya kura kwa kiasi kikubwa yaliamua nani awe mbunge/ diwani japo kwa urais ilipangwa. Mwaka 2019, 2020, 2024 hakukuwa na uchaguzi bali maigizo na ilipangwa nani awe mbunge , diwani na kura za urais zilipangwa.

Ninahisi pia 2025 yatajirudia yaleyale. Kwa nini ninashiriki? Mungu anataka tutmize wajibu wetu ndipo tumuombe msaada. Najua kura yangu inaweza isiheshimiwe lakini nikimlilia Mungu akiamua anaweza kunisaidia kwa sababu nilitimiza wajibu wangu

No reform no election haiafanikiwa.
Katiba na sheria za kweli na za haki haziwezi kupatikana kwa aina hii ya watu waliopo. Watanganyika hawa ambao tangu asubuhi hadi usiku wanachajadili Simba na yanga, mapenzi na umbea ndio washinikize no reform no election? Rejea nchi kama Kenya, Benin na nchi zingine katiba zao zilipatilanaje Kenya kwa mfano kila mwanasiasa ana watu na anajua idadi yake ndio maana hata kukaa mezani kupanga inawezekana. Juzi hapa Ruto baada ya kuona amekosana na Gachagua aliyekuwa makamo wake na pia amekosana na Kenyatta, akajua fika kariba nusu ya kura alizopata hatazipata mwaka 2027 hivyo ameingia makubaliano na Raila ambaye ana kura milioni kadhaa za wajaluo. Hivyo wajaluo kama kabila la tatu kwa ukubwa na Wakalenjini kama kabila la kwanza wakijumlisha kura zao zitafikia nusu na wakiongezea na za wanasiasa wa makabila mengne ana uhakika wa ushindi. Japo mwaka 2027 bado haujafika lakini kwa hesabu za mezani Ruto au mtu yeyote mfuatiliaji anaweza kukwambia Ruto atapata kura ngapi. Basis ya hii yote ni kwa sababu Kenya wanasiasa wana watu nyuma yao.

Hapa Tanzania huwa nasema mwanasiasa pekee aliyekuwa na watu ni maalim Sefu na Nyerere basi. Kwa sasa si CCM wala upinzani hakuna mwanasiasa binafsi mwenye watu. Maalim Sefu kwa zanzibar alikuwa na watu karibia nusu ya pupalation na nusu ya wapiga kura ( laki mbili hivi) na alikuwa na uwezo wa kuwaingiza barabarani. Kama isingekuwa support ya Tanganyika CCM ya Unguna ingelazimika kukubaliana na matakwa ya wazanzibari na ndiyo sababu pekee inayofanya CCM UNGUJA iuhitaji muungano. Kama zanzibar ingekuwa,nchi huru siku nyingi wazanzibari wangekuwa na katiba mpya na sheria mpya na za haki za uchaguzi.

Wakati Mbowe alilpoitisha maandamano yaiyoshindwa, wakati wa uchaguzi wafuasi wa Lissu walimtukana kuwa watu hawajitokezi sababu wamemstukia ni pandikizi. Sasa tusubiri Lissu aitishe maandamano ya no reform no election tuone kama mtajitokeza hata wewe hautaingia barabarani.

CDM wanajidanganya kuwa watarally support ya vyama vingine. Kwanza nje ya CDM vyama vingine vyote vilivyo upinzani ni CCM B. ACT kwa mfano wao wanaendelea kuandaa wagombea huku wakiwahadaa kuwa wanapogania sheria za uchaguzi zibadilishwe. Oktoba watashiriki uchaguzi na watagawiwa baadhi ya viti vya ubunge na udiwani pamoja na vyama vingine ili kuleta taswira ya kuendelea kuhadaa dunia kuwa uchaguzi ulkuwa huru.

Katika. mazingira haya ya watu waliolala usingizi ni afadhali kushiriki uchaguzi kuliko kususia.

Hoja yenu ya no reform no election Ingeweza kufanikiwa kama mmgekuwa na watu. Viongozi wa CDM ghafla hawawajui watanganyika?

Kitakachotokea oktoba 2025 itakuwa ni aibu na failure kubwa kwa Lissu, CDM itakuwa haina ruzuku, itakuwa imethibitika haina watu, haitakuwa na mbunge wala diwani.

Oktoba 2925 sio mbali tusubiri tuone.

Nb, CCM wanajua fika wakiruhusu uchaguzi hata walau ule wa kiwango cha mwaka 2015 wataambulia kura zisizozidi asilimia 65 na hata chini ya hapo. Wanaweza kupoteza ubunge kwa hadi asilimia 45. Hivyo kutegemea itaruhusu shinikizo tena la kwenye social media ni kujidanganya.
 
Back
Top Bottom