Panua akili kidogo. Hapa siyo swala la kupenda hili jina Tanganyika.Hivi ni kwa nini unalipenda sana hilo jina la Tanganyika tulilopewa na mkoloni Mwingereza? Yule mkoloni Mujerumani alituita Deutsche Ouster Africa. Hata muungano wetu na Zanzibar ukivunjika, kamwe hatutakubali majina hayo waliotuita wakoloni hao yarejee. Tutatafuta jina letu wenyewe zuri. Tunaweza kuendelea na jina la Tanzania. Au tukajiita Nyanyembe au Msimbazi na kadhalika.
Hata hivyo umekosea, Tanganyika siyo jina alilotoa mkoloni. Inaonekana historia ya nchi hii huijui. Lakini la muhimu ninakuelekeza kwenye huo mstari huo wa kwanza.
Naona wewe ni kati ya hawa watu wa aina ya 'mwendo kasi', pamoja na kuwa na hiyo MD.
Pamoja na hayo yote, mada yako ni ya msingi sana.