Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Nadhani anajaribu kuota uteuzi kwa mama ilhali ashatumiwa kama kondomu hana matumizi tena
1646059471087.png
 
Kwani ndo maana tulituma Takukuru kumchunguza Mbowe pamoja na Chama chao vipi walikuja na majibu gani kwani ni muda sasa.
Kudhibitisha tuhuma ndo mtu hupata hoja kwani hoja hujibiwa kwa hoja ndo afya siasa sio maneno matupu
akijibu nistue
 
Kwavile amestaafu siasa achane na mambo yanayohusisha siasa ili alinde heshima kubwa ambayo wengine tumeijenga kwake kwa miaka mingi.

Kwa level yake ajue kila tamshi lake litapimwa kwa uzito ule ule.
Kwi Kwi Kwi Kunguru hafugiki
 
Dr,Dr,Dr Tlaa.Unataka kutufundisha uoga?Yaani,unawezaje kuitenganisha kesi ya Mh.Mbowe na siasa wakati sote tukifahamu kuwa hata walioifungua wanatambua kwamba nia ya kesi ni kukidhoofisha harakati za kudai Katiba mpya,CDM na Mwenyekiti wao?
Je,Dr haufahamu kuwa hamu kubwa ya CCM yako ni kuifuta CDM ili wao wajinafasi?Je,haufahamukwamba wewe binafsi 2010 uliporwa urais?Hata 2015 Lowassa alishinda urais na tena 2020 Lissu naye alipoporwa wewe haufahamu!
Haikosi kuna tatizo,labda Dr umedukuliwa akili!
Wananchi/Wana CHADEMA wana haki ya kudai kwamba Mbowe siyo gaidi hadi mahakama itakapothibitisha vinginevyo.Hakuna namna ya kutenganisha kesi hii na siasa.
Natarajia Dr ujiunge na chain,ulishavuka kikwazo cha uoga na hofu.CCM hawatakufanya lolote,sikia kilio cha Watanzania wenzako.Tunataka Katiba mpya.
umetoka povu jingi
 
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno kuwa 'Mbowe si gaidi' ambayo hutolewa na baadhi ya wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Amesema wananchi wanatakiwa kuiachia mahakama ambayo ndio chombo cha haki.

“Katika masuala yaliyoko mahakamani ninaona kwanza kuna sura inatumika, kwenda kule Mahakamani kama sehemu ya siasa kitu ambacho mimi sikubaliani nacho.

“Hivyo sijaenda kwa kuwa ni kitu ambacho sikubaliani nacho, sikubaliani na principal ambayo inatumika, mnaenda kule kisha mnaanza kujipiga picha na mpo kwenye mitandao, hiyo ni siasa, mimi sichezi hizo siasa.

“Mimi nikiamua kumtembelea Mbowe nitaenda nyumbani kwake, sitaki kufanya kitendo cha Mbowe kuwa gerezani kuwa siasa, kama ni kumuombea nitauombea kwa nafsi yangu.

“Niliudhika tangu siku ya kwanza na yale maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema Mbowe siyo gaidi?

“Wanatakiwa kuachia chombo cha haki kitoe maamuzi siyo wananchi.

“Lakini sina chuki na Mbowe wala sina uadui, nimeshakutana na Mbowe mara kadhaa airport, tukakumbatiana, tukabadilishana namba japo hakuna aliyempigia mwenzake,” anasema DK SLAA.

Source: MwanaHalisi


Mbowe sio gaidi
 
Fuatilia vuzuri ndo mtetee Dr. kwani Mbowe kwenye siasa za hapa Tanzania hakuna wa kumfananisha naye lile la kweli litakuweka huru.
Unataka kulazimisha yaakuwa Mbowe hakumshawishi kujiunga na Chadema hivi ni kiongozi gani wa upinzani anaweza kutoka Tanzania na kwenda Uingereza kumshawishi mtu arudi tanzani kujiunga na chama cha siasa yaani Chadema kwa garama zake mwenyewe na huyu sio mwingine ni Dr. Kaburu kwa hiyo Mbowe ni zaidi ya mwanasiasa.
Jibu rahisi sana angalia ile clipu aliyoongea siku ya uhuru pale Magufuli alipompa nafasi ya kutoa neno kujambo utalipata kwake alafu wangalie viongozi waliokaa pembeni yake yaani Cheyo na Lipumba
ni kosa kubwa kumlinganisha mbowe na Dr. Slaa.
1. Elimu tu hawalingani, yaani unataka kumfananisha Dr. na Mbowe aliye feli form 6?!!
huo ni ukosefu wa adabu, tafkari upya.
ujanja ujanja wa kuongea mboe anao...ni mtu wa kutaka na yy aonekane kasoma lkn bahati mbaya hana elimu.
ujanja wa kuongea tu kila mtu anao.
 
I don’t like to take sides ,lakini huyu mzee amekosea sana
 
Nimefutiwa comment yangu.

Huo ni uchuro mambo yakufutiana comments.

Kwanini mnafuta?

Mna watu humu kazi yao nikumtukana mbowe kwa maneno kibao ya kumvunjia heshima tukisema sisi mnafuta tunayoandika.

Dokta sila ni mjinga kabisa asifanye ujuaji kama anakereka ajitunge tu.

Na nyinyi mnaofutafuta mjiangalie nitawapiga kipapai.
 
Chama cha upinzani pekee kinacho ongozwa na mwenyekiti aliye feli form 6 ni Chadema.
karne hii ya 21 mnaongozwa na form 6 failure!! ni aibu kubwa.
ndio maana aliamua kutumia mipango haramu ya kuihujumu serikali....hiyo inadhihirisha ukosefu wa maarifa/Elimu ya kutosha.
ukisikiliza tu ushahidi ulio tolewa dhidi yake utagundua kweli huyu jamaa hana elimu.
ukosefu wa elimu ndio umemfikish hapo kwa kufanya mipango ya kijinga kabisa.
 
Kipindi anakula alikuwa kimya kastaafu ndo anaongea.
Muulizeni Josephine mushumbushi hajambo?
Akijibu nitag
 
Dr. Slaa
Dr. Mashinji hawa wote walikuwa watendaji wakuu wa CDM, awanajua mikakati yote ya siri iliyo kuwa ikiratibiwa na Mbowe dhidi ya Serikali.
Na mmefaidika nini na wao kujua siri za Mbowe? Au nao walikuwa watoe ushahidi kwenye kesi ya ugaidi?

Amandla...
 
Chama cha upinzani pekee kinacho ongozwa na mwenyekiti aliye feli form 6 ni Chadema.
karne hii ya 21 mnaongozwa na form 6 failure!! ni aibu kubwa.
ndio maana aliamua kutumia mipango haramu ya kuihujumu serikali....hiyo inadhihirisha ukosefu wa maarifa/Elimu ya kutosha.
ukisikiliza tu ushahidi ulio tolewa dhidi yake utagundua kweli huyu jamaa hana elimu.
ukosefu wa elimu ndio umemfikish hapo kwa kufanya mipango ya kijinga kabisa.
Uko sahihi kabisa. Ndio maana aliweka bajeti ya shilingi 600000 za kupindulia nchi. Na alijua ataweza kulipua kituo cha mafuta bila explosives. Na mbaya zaidi alijua akipanga magogo Morogoro road, nchi itakuwa ya kwake!

Amandla...
 
Kwani ni Balozi wa nchi gani tuanzie hapo kwanza.
 
Back
Top Bottom