Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno kuwa 'Mbowe si gaidi' ambayo hutolewa na baadhi ya wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Amesema wananchi wanatakiwa kuiachia mahakama ambayo ndio chombo cha haki.

“Katika masuala yaliyoko mahakamani ninaona kwanza kuna sura inatumika, kwenda kule Mahakamani kama sehemu ya siasa kitu ambacho mimi sikubaliani nacho.

“Hivyo sijaenda kwa kuwa ni kitu ambacho sikubaliani nacho, sikubaliani na principal ambayo inatumika, mnaenda kule kisha mnaanza kujipiga picha na mpo kwenye mitandao, hiyo ni siasa, mimi sichezi hizo siasa.

“Mimi nikiamua kumtembelea Mbowe nitaenda nyumbani kwake, sitaki kufanya kitendo cha Mbowe kuwa gerezani kuwa siasa, kama ni kumuombea nitauombea kwa nafsi yangu.

“Niliudhika tangu siku ya kwanza na yale maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema Mbowe siyo gaidi?

“Wanatakiwa kuachia chombo cha haki kitoe maamuzi siyo wananchi.

“Lakini sina chuki na Mbowe wala sina uadui, nimeshakutana na Mbowe mara kadhaa airport, tukakumbatiana, tukabadilishana namba japo hakuna aliyempigia mwenzake,” anasema DK SLAA.

Source: MwanaHalisi

Mtu mzima akili mtoto
 
CHADEMA ilipoteza muelekeo uyu mzee alipokiacha chama Sasa wamebakia wahuni wahuni na program zao cha upato wa changia sijui mawakili, sijui makamanda yani janja janja tu na matusi
Utakubali kuwepo tume huru ya uchaguzi 2025?
 
Hii sio Karne ya Kuongozwa na mwenye Karama.
Huwezi kulinganish mwenye Elimu na asiye na Elimu.

Mbowe hajaelimika...yaani kafeli kidato cha 6 sasa kweli unaweza kulinganisha kwenye mizani na Dr. Slaa?!
haiwezekani.....yaaani Mbowe anafaa kwenye kupiga debe tu lkn kwenye mambo ya kisomi/kitaalamu hawezi.
FB_IMG_1646118231993.jpg
 
Mtu illiterate anaongoza chama tangu mwaka 2003 hadi leo....halafu mnashangilia tu.
haalafu eti wanajiita chama cha Demokrasia Chadema!!!

matokeo ya kung'ang'ania uenyekiti akaanza kukitumia chama kafanya mambo ya kihalifu na hatimaye ameangukia kwenye mokono ya dola.
 
Sasa mzee wetu akisikia na hii yaJoinTheChain si atazimia kabisa.
 
Kuishi bila kupigana vita ya kuwa na kipato huru huwa inaleta laana.Imagine kizee kama hiki kinapambana ili kipate teuzi kiweze kupata ugali.

I gonna risk everything to posses my own stream source of income.Haya maisha ya kuja kuongea pumba uzeeni ili niweze kuishi siyawezi.
 
Kuishi bila plan ndiko huku sasa @70+ age bado unaishi kwa kutegemea teuzi ili utibu njaa..
 
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno kuwa 'Mbowe si gaidi' ambayo hutolewa na baadhi ya wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Amesema wananchi wanatakiwa kuiachia mahakama ambayo ndio chombo cha haki.

“Katika masuala yaliyoko mahakamani ninaona kwanza kuna sura inatumika, kwenda kule Mahakamani kama sehemu ya siasa kitu ambacho mimi sikubaliani nacho.

“Hivyo sijaenda kwa kuwa ni kitu ambacho sikubaliani nacho, sikubaliani na principal ambayo inatumika, mnaenda kule kisha mnaanza kujipiga picha na mpo kwenye mitandao, hiyo ni siasa, mimi sichezi hizo siasa.

“Mimi nikiamua kumtembelea Mbowe nitaenda nyumbani kwake, sitaki kufanya kitendo cha Mbowe kuwa gerezani kuwa siasa, kama ni kumuombea nitauombea kwa nafsi yangu.

“Niliudhika tangu siku ya kwanza na yale maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema Mbowe siyo gaidi?

“Wanatakiwa kuachia chombo cha haki kitoe maamuzi siyo wananchi.

“Lakini sina chuki na Mbowe wala sina uadui, nimeshakutana na Mbowe mara kadhaa airport, tukakumbatiana, tukabadilishana namba japo hakuna aliyempigia mwenzake,” anasema DK SLAA.

Source: MwanaHalisi

Huyu anatafuta kukumbukwa katika uteuzi Ubalozi umeisha, mke kapokonywa. Hivi kwani kesi ikiwa mahakamani inafanya watu wasiwe na uwezo wa kupembua kama mtu ana hatia au la. Mahakama ni kweli ina dhamana ya kutoa hukumu lakini haizuii wananchi kuchambua kesi kwani sio mahakama pekee yenye uwezo wa kudadavua kesi.

Hata mimi japo siipendi CHADEMA na siiungi mkono hata kidogo lakini katika kesi hivi kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na cross examination iliyofanywa naamini kabisa Mbowe na wenzake hawana hatia.
 
Nakumbuka kwa stage aliyofikia slaa ya upadri, na akauacha wanasema mtu huyu ahaminiki, hivyo simshangai!
 
Dr. Slaa ni Moja ya watu wanaochukizwa na wananchi kumtetea Mbowe: amedai anakwazika akisikia watu wanasema Mbowe Siyo Gaidi huku akitaka mahakama iachwe ifanye kazi yake.

Wakati akiumizwa na wapenda haki kusimamia haki ameshindwa kueleza anajisikiaje anaposikia Watu wa chama chake CCM wakisema adharani kwamba Mbowe ni Gaidi kinyume kabisa na status ya kesi mahakamani.

Kwa wanaopenda haki nadhani Dr. Slaa amepuliza kipenga Cha watu kumkera zaidi na zaidi Kwa kutamka Mbowe Siyo Gaidi.

Mmhhh mbona kama mkao wa mkono wa kushoto wa huyu mzee sijauelewa hivi!!? Au mzee ako na tatzo kiafya labda?
 
Tangu tumchukue CHADEMA imepoteana imekuwa kinara wa michango kuzidi vikundi vya kufa na kuzikana mitaani kwetu🤪

Utakuwa kijana wa juzi basi,kwani Bingwa wa michango ni nani kama siyo CCM.
Mpaka Mbio za Mwenge tumechangia sana tena kwa lazima.

Hivi Viwanja mnavyoita vya CCM kila Mkoa tumechangia sana ni nguvu za Wananchi mpaka kufikia hapo.
 
Pamoja na kupewa ubalozi nongwa imejaa roho mwa mtumishi a bwana
 
yana mhusu kwa sababu DR.Slaa ni mzalendo wa kweli, anaipenda nchi yake sio kama Mbowe mhalifu na msaliti mkubwa kwa nchi.
mbowe ange kuwa raia wa china unajua nini kingemtokea.
Yeye ni mwanaCCM, Mbowe ni Chadema. Sasa mambo ya Chadema na Mbowe ni ya nini kwake?
 
Mchumia tumbo tu,,, hana lolote...

Halafu kuongea wakati wa kula sio adabu... Atakuja akosee kama ndugai aanze kulaumu watu
 
Back
Top Bottom