Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Hayo yamepita tugange tuliyonayo na yajayo sasa.Tuwaombee Mwenyezimungu watoke salama.Nakila aliehusika na ushenzi ule Mungu umuadhibu vikali bila huruma.Hata kama ni baba au mama!
 
Kuna mengi mazito hatukuyajua , Mungu ameanza kutufunulia japo kuna ambao waliyajua kutoka awali lakini kwa kuwa walikuwa wanufaika wakaamua kukaa kimya.

Hatimaye muda ni msemakweli
 
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno kuwa 'Mbowe si gaidi' ambayo hutolewa na baadhi ya wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Amesema wananchi wanatakiwa kuiachia mahakama ambayo ndio chombo cha haki.

“Katika masuala yaliyoko mahakamani ninaona kwanza kuna sura inatumika, kwenda kule Mahakamani kama sehemu ya siasa kitu ambacho mimi sikubaliani nacho.

“Hivyo sijaenda kwa kuwa ni kitu ambacho sikubaliani nacho, sikubaliani na principal ambayo inatumika, mnaenda kule kisha mnaanza kujipiga picha na mpo kwenye mitandao, hiyo ni siasa, mimi sichezi hizo siasa.

“Mimi nikiamua kumtembelea Mbowe nitaenda nyumbani kwake, sitaki kufanya kitendo cha Mbowe kuwa gerezani kuwa siasa, kama ni kumuombea nitauombea kwa nafsi yangu.

“Niliudhika tangu siku ya kwanza na yale maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema Mbowe siyo gaidi?

“Wanatakiwa kuachia chombo cha haki kitoe maamuzi siyo wananchi.

“Lakini sina chuki na Mbowe wala sina uadui, nimeshakutana na Mbowe mara kadhaa airport, tukakumbatiana, tukabadilishana namba japo hakuna aliyempigia mwenzake,” anasema DK SLAA.

Source: MwanaHalisi

View attachment 2720207
Anamjua Mbowe
 
Kuna mengi mazito hatukuyajua , Mungu ameanza kutufunulia japo kuna ambao waliyajua kutoa awali lakini kwa kuwa walikuwa wanufaika wakaamua kukaa kimya.

Hatimaye muda ni msemakweli
Tulikuwa nyumbu kweli kweli
 
Back
Top Bottom