Juzi kati natoka maeneo fulani, na pikipiki napigwa mkono na mshikaji, nikasimama, akaniuliza unaelekea wapi nikamjibu akasema nae anaenda maeneo hayo nimsogeze, nilivyomcheki nikaona fresh wacha nimsaidie dizaini ni kama mwanachuo aliyemaliza miaka kadhaa mtaani life limempiga.
Nikamruhusu akalie chombo, njiani sikutaka maswali mengi, nikafika sehemu ninapoishia mimi, ye anaendelea na safari, kushuka anaanza kuleta stori, mwisho nikajua ni askari akanionesha na pingu kuna mwizi gani sijui anaenda kumkamata, nikajisikia vibaya sana kwanini nilimpa lifti kenge yule., nikatamani hata nimdai nauli, nikaona sio fresh.
Akaomba tubadilishane namba za simu nikamchomolea.
We kenge uliyepandia maeneo ya mikwambe pale, ukaja shukia mjimwema una bahati hukujitaja mapema nisingekupa lifti.