Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tandika kitanda mkuu ulale tuSlaa safi sana
Umemtetea vizuri lakini unajua fika kua kaongea pumbaJamani hebu muoneeni huruma Dr Slaa. Hivi kweli mlitaka asemeje? Ubalozi wenyewe hata kuapishwa bado, kupangiwa kituo bado! Au mnafurahi mnavyosikia anauza supermarket huko 'ke-nada'? Please, hebu tuwe realistic and fair.
Umemtag [B]idawa[/B] ukamsahau [B]MTAZAMO[/B]...kwa hao jamaa Dr Slaa aliyehamia Chadema akiutafuta ubunge eti ndiye alikuwa mpinzani wa kweli. Wakati wana mageuzi tunapigwa virungu tukidai mfumo wa vyama vingi Dr. Slaa alikuwa anakula kivulini kwenye kambi ya CCM. Alipotoswa akasetiriwa na Chadema na kuukwaa ubunge.
Naona anasahau aliyokuwa akiyadema yeye mwenyewe wakati akiwa KM wa Chadema. Tulikuwa tukisikia akilalama kila siku kufuatiliwa na hata kutaka kuuwawa! Ya Kanada anajua kwamba polisi wanafanya kazi na kutoa feedback na hasa kwa matukio ambayo ni high profile. Je anaweza kutuambia hapa kwetu polisi walishatoa ripoti kuhusu matukio kama hayo - yakiwemo yale ya Arusha na kwingineko.Balozi Mteule na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amesema tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida na ameitaka jamii kuliacha Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi na kutoa majibu.
Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds juu ya hali ya kisiasa ya Tanzania na mustakabali wa maisha yake baada ya kuondoka CHADEMA, amesema hafurahishwi na baadhi ya watu kuwataja hadharani watuhumiwa wa tukio hilo kwasababu linaharibu uchunguzi wa polisi.
“Mimi kinachoniudhi ni hii watu kusema hadharani kwamba kuna hiki na hiki tunasuspect (tunahisi) waliofanya ni fulani. Sheria inasema ukihisi nenda polisi katoe taarifa sio unaenda kwenye vyombo vya habari”, amesema Dkt. Slaa.
Amesema hawezi kuzungumzia kwa undani suala la Lissu kupigwa risasi, ikizingatiwa kuwa watu wengi wamepigwa risasi nchini na kazi ya kuwabaini wahalifu waliomshambulia ni ya polisi sio viongozi wa siasa au wananchi.
“Lakini kama binadamu hakuna anayependa binadamu yeyote aumizwe lakini matukio haya ya kuumizwa yametokea nchi hii kwa watu wengi sana. Na mimi sio chombo cha dola kujua kwamba unanyoosha kidole kwa kitu ambacho hatukiamini; mimi ni msomi”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza kuwa,
“Ukitoa taarifa za upelelezi unaharibu upelelezi. Mimi niko Canada mauaji yapo kila siku na watu wanapotea, wanapigwa risasi wakiulizwa polisi wanakwambia suala hilo liko kwenye upelelezi tukifikia hatua nzuri tutatoa taarifa”.
Na sisi tutaendelea kumficha dereva ili lulwamisha upelelezi.Dr Slaa kasema ni tukio la kawaida? Kama ni kweli ameongea haya maneno nitamtoa maanani moja kwa moja!
Nadhani anataka kutumika kuendesha propaganda kuwa Lissu hakushambuliwa kwasababu za kisiasa!
Ukisoma btn the lines, kusema ni tukio la kawaida, ni sawa na kudownplay tukio zima!
Ubalozi aliopewa, naona mojawapo ya masharti, ni “ubalozi wa propaganda dhidi ya Lissu”
Sasa karata ya serikali ya ccm dhidi ya Lissu ni Slaa!
Anamkumbuka khalid kagenzi huyu mtu? Asitufanye wajinga kama yeyeYeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?