Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Sikutegemea kusikia haya kwa ndugu yetu Slaa. Kusema tukio la TL ni la kawaida. Kila mtu anaishangaa Tz kwa tukio hili isipokuwa yeye. Shame on him. Asiwe na chuki kama babu yake. Nimemsifu kwa kusema hali ya democrasia ni mbaya. Sasa alishindwa vipi kusema ukweli kwa hili ama limekuwa kubwa mno kumeza.
 
Mwenyezi Mungu huumbua wanafiki. Kwa matamshi yake anajifunua hadharani tabia yake kwa wote kumfahamu. Inasikitisha sana anakoelekea katika lindi la aibu na kudharaulika.
 
Nikifaninisha tukio la Lissu na la ndugu zangu waliopoteza uhai Kibiti, na polisi waliopoteza uhai kwa kushambuliwa wakiwa katika malindo yao naona tukio la Lissu ni la kawaida tu. Viachwe vyombo husika vifanye kazi yao katika uchunguzi wa matukio haya.
Matukio hayafananishi bali yanatafutiwa suluhisho.
 
an empty stomach is not a good political advisor...Yeye alipokuwa Mbunge siku aliita waandishi wa Habari chumbani kwake na kudai amewekewa vinasa sauti chini ya uvungu wa kitanda. Huyu Mzee angekaa kimya ili abaki na heshima yake iliyobaki (kama ipo)
 
FikraPevu Kumbe bora alikosa Urais maana njaa aliyo nayo angeuza nchi na kuwa msaliti mkubwa na ndumila kuwili wa mageuzi.

Kumbe kuingia Chadema haikuwa ni kwa sababu ya mageuzi bali alipotemwa upadri akakikmbilia siasa CCM nako walipomtema akakimbilia Chadema na kulaghai watu ni mwanamapinduzi kumbe njaa.

Nako alipochokwa akaenda kwa wazungu wakamtema ndo amekimbilia CCM. Ndiyo maana ndoa na kutunza familia nako kumemshinda
 
Huyu mzee anaitumikia njaa kwa kiwango kilichotukuka.
 
Tunaomba video clip ya mahojiano kwenye rundiga, tunataka tuone uso wake wakati akitamka haya.
 
Duniani Viongozi wa siasa chungu mzima wamepigwa risasi, polisi wakaachiwa wafanye kazi, wakaridhika, ama kama hawakuridhika kama ya kina Kennedy, wanajijuwa wenyewe..
Ila hapa TZ bana...! Ni shida..
 
Slaa ametoa maoni yake,km unaushahidi nenda polisi katoe taarifa then wahusika wapelekwe mahakamani.hata chadema kwa luwasa wanasema hvyo hvyo km unashahidi luwasa ni fisadi nenda mahakamani
 
We dokta mbona unasema urongo wakati wewe mtu wa dini? Lini jaribio la kuua likawa la kawaida nchini kwetu? Tangu utawala wa Mwalimu, Mzee Ruksa, Mzee Mkapa na Kikwete tuambie je huu utamaduni wa watu kupotea na hata kupigwa risasi mchana kweupe je ulikuwapo? Dokta hebu tumwogope Mungu jamani. Hata kama unatetea basi basi siyo kwa kiwango hiki cha lami.
 
Ni la kawaida kwa namna gani? Kwa hiyo watu wa kariba ya Lissu wawe wanapigwa risasi kwa kuwa ni kawaida? Kwa hiyo ni uamaduni kupigwa risasi ki hivyo? Hayo mambo ni mysterious bora wanasiasa kuacha kuzungumzia ili hali si tukio la kawaida kwa nchi kama Tanyania
 
Yeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?
Hayo n matukio ya kupigwa risasi nayo eeee
 
Yeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?

Mkuu keshafika bei huyo.. Inabidi aseme kinachomfurahisha bosi wake wa sasa..!!
Mark my words....
 
Si kila kiongozi wa dini ni wa Mungu,wengine ni watumishi wa shetani tangu kuumbwa kwao.Wana ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu hatari.
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Ushahidi upo wa kutosha.
Polisi wameshindwa kuchukua hatua.
Leteni FBI au Scotland Yard kazi haitachukua week itakamilika.
 
Back
Top Bottom