Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Maskini mzee wa watu Jela na huo uzee wote si atakufa kwa ukurutu?
 
Mungu akubariki kwa kulifukuwa hili kaburi.

JF ni mkataba ya Taifa, wanafki wote wataumbuka mchana kweupe.

Na Mimi nasisitiza Dr Slaa kupewa kesi ya uhaini ni jambo la kawaida.

Hili ni swala lake binafsi na familia yake, Watanzania tuendelee na shughuri zetu.

Ukipanda Mahindi usitegemee kuvuna mihogo, kuimba ni kupokezana.
Unamgeuka Dr.kabla jogoo hajawika [emoji1787]
 
Naipenda sana Nchi yangu hata kama kuna matatizo siwezi kuiombea mapinduzi ya kijeshi.

Huyu Mzee wa Kinyaturu alienda too far na sijui kama ataweza kubeba mtondoo na uzee wite huo
 
Ninalo.

Na yeye ameanza kupata stahiki zake kadiri ya uhitaji.

Nadhani akitoka(kama atajaaliwa)atatuhabarisha vema.

Maana kwake hata kupigwa risasi ni jambo la kawaida sana.
Malipo ni hapa hapa Duniani. Aliwabeza Lissu na Mbowe, hakuwatia Moyo wala kuwaona Magerezani. Watu walizofanya Siasa pamoja from Zero to Hero
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Stupid, Leo unasemaje
 
Balozi Mteule na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amesema tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida na ameitaka jamii kuliacha Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi na kutoa majibu.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds juu ya hali ya kisiasa ya Tanzania na mustakabali wa maisha yake baada ya kuondoka CHADEMA, amesema hafurahishwi na baadhi ya watu kuwataja hadharani watuhumiwa wa tukio hilo kwasababu linaharibu uchunguzi wa polisi.

“Mimi kinachoniudhi ni hii watu kusema hadharani kwamba kuna hiki na hiki tunasuspect (tunahisi) waliofanya ni fulani. Sheria inasema ukihisi nenda polisi katoe taarifa sio unaenda kwenye vyombo vya habari”, amesema Dkt. Slaa.

Amesema hawezi kuzungumzia kwa undani suala la Lissu kupigwa risasi, ikizingatiwa kuwa watu wengi wamepigwa risasi nchini na kazi ya kuwabaini wahalifu waliomshambulia ni ya polisi sio viongozi wa siasa au wananchi.

“Lakini kama binadamu hakuna anayependa binadamu yeyote aumizwe lakini matukio haya ya kuumizwa yametokea nchi hii kwa watu wengi sana. Na mimi sio chombo cha dola kujua kwamba unanyoosha kidole kwa kitu ambacho hatukiamini; mimi ni msomi”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza kuwa,

“Ukitoa taarifa za upelelezi unaharibu upelelezi. Mimi niko Canada mauaji yapo kila siku na watu wanapotea, wanapigwa risasi wakiulizwa polisi wanakwambia suala hilo liko kwenye upelelezi tukifikia hatua nzuri tutatoa taarifa”.
safi sanan balozi
 
nami naunga mkono kauli ya dr slaa kwamba swala likiwa polisi tuwaachie polisi wafanye kazi yao, kwanza kukamatwa ni jambo la kawaida mbona mdude anakamatwa kila siku, mzee ameyatimba na kwa kali zake za awamu ya tano ndio mana tunashindwa leo kumuonea huruma, aacha aonje kibaridi cha rumande ili atofautishe utamu wa asali vs jiwe
 
Ila Lissu ana busara sana. Nenda kamhoji hata sasa hivi anasemaje kuhusu kushikiliwa kwa Dr.Slaa, atakwambia;"Siyo sawa hata kidogo, wanataka kunyamazisha sauti za kutetea rasilimali za taifa letu, hatukubali!"

Kwa ufupi, T.A.Lissu hatalipa baya kwa baya kwa kauli zile za Dr.Slaa juu ya assassination attempt on him.
 
Back
Top Bottom