Dkt. Slaa: Tunapinga uwekezaji wa DP World sababu Mkataba wake una sura ya wizi na ufisadi

Dkt. Slaa: Tunapinga uwekezaji wa DP World sababu Mkataba wake una sura ya wizi na ufisadi

Fuatilia yatakayojiri kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo Dr. Salaa, Askofu Mwamakula pamoja na Mawakili Mwambukusi na Madeleka watakuwa wazungumzaji wakuu, leo Julai 12, 2023 saa 4:00 asubuhi.

Ni kuhusu suala la DP World.

View attachment 2685517

===



Askofu Mwanamkula anazungumza
Juni 6, 2023 baada ya kusikia minong'ono ya mkataba kuwa na miaka 100, nilichukua jukumu la kuishairi serikali itoke kufafanua suala hili, baadae Bunge lilitoka kusema mkataba ungejadiliwa Bungeni.

Baadae Mkuu wa Mkoa wa DSM alitoa kauli kumuonya Dr. Slaa, baadae Dkt. Nshala katishiwa maisha, baadae Wakili Mwabukisi naye katishiwa maisha.

Tumeona pia jeshi la polisi limemuita Dkt. Nshala kumhoji kuhusu matamshi ya mkataba, tulidhani watamhoji ili awape ushirikiano kuhusu suala lake la kutishiwa maisha.

Mimi kama Askofu natoa tahadhari, mtanzania yeyote anayetoa maoni kuhusu mtakaba, kama akidhurika, akitekwa au kuuawa kwa namna yoyote viongozi waliotoa maoni ya kutisha pamoja na Serikali watawajibika. Mungu atawafedhehesha watu hao kuanzia aliyetoa wazo, anayepanga mkakati, anayetoa amri na ayetekeleza amri ya kuwadhuru watu wanaoongea, kulalamika na kudhurika kuhusu mkataba huu.

Kanisa linaangalia, lakini haliridhiki na yanayoendelea japo sio kila Askofu atasimama kama mimi kusema. Tuache kuteka na kufedhehesha watu wanaotoa maoni kuhusu jambo hili.

Mwarabu hakwepeki
 
Mbona kipind cha magufuli hukusema hivo?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
President Magufuli alikua ni serial dictator, alitaka asikilizwe yeye tu na hili liliwezeshwa na uoga wa kizuzu wa watanzania, street battles hawaziwezi ila ni warriors wa key board's kulalama kutwa
 
Nyinyi endeleeni kuwasikiliza tu wenzenu wanalipwa na makampuni yanayowatuma yanayoelekea kupoteza ulaji bandarini nyinyi mmebaki kukesha mitandaoni kuwasikiliza badala ya kwenda mashambani na kwenye shughuli zitazokuingizieni kipato na familia zenu.
Kazi yao ndo hiyo kupiga siasa tu. Watu wanafanya kazi wao wanaendekeza maneno matupu tu.
 
Nyinyi endeleeni kuwasikiliza tu wenzenu wanalipwa na makampuni yanayowatuma yanayoelekea kupoteza ulaji bandarini nyinyi mmebaki kukesha mitandaoni kuwasikiliza badala ya kwenda mashambani na kwenye shughuli zitazokuingizieni kipato na familia zenu.
wacha ukweli usemwe. Tuna akili ya kuchuja pumba na mchele.
 
uhuru wa miguu na mikono
Akili imefungwa mnyororo.

Bora nchi achukuwe mchaga tu.
 
Dr Mwakyembe kiukweli katika issue ya Richmond taifa litakukumbuka

Nawaona vijana wa Mbeya waliobobea kwenye Sheria wakiendeleza moto ule ule

Huyu Mwambukusi anasema Rais Samia awe makini na Mawaziri wanaomsifia anaupiga mwingi kwani 2025 Watamgeuka kwa haya yanayotokea sasa

Huko Mbeya mko Wakweli sana, Mungu wa mbinguni awabariki!
 
Huyu Mdude Chadema anajiamini sana aisee 😂

Zamani kujiamini huku lazima baba yako awe Mganga kama Akina Mzindakaya au awe mchawi kabisa

Mdude anadai Levo aliyofikia wa kumtisha ni Majenelari tu Lakini siyo na Akina Nape

Duh, Mungu atulinde kwa kweli, huyu Mdude Chadema Alikuwa anasalimia tu Mkutano wa Dr Slaa na Waandishi wa habari!
 
Huyu Mwanasheria kijana wa Mbeya, anaonyesha ni namna gani vijana wakitanzania tunapaswa kuwa, Heko watu wa Mbeya kwa kuwa na kijana kama huyu.

Baada ya haya yote Zawadi yake ni kumpa ubunge na mimi nitamuweka kwenye baraza langu la mawaziri soon nikiwa Rais.
 
Sheria mama inakataza rasilimali za nchi kujadiliwa nje ya mipaka yetu, lakini muswada huu unaenda kuifuta, maana yake sasa kesi zote za rasilimali zetu zitajadiliwa kwenye Mahakama za nje.
Sheria mama Ina Tatizo gani? Kwa kweli wakipitisha sheria hii wabunge, tutajua kweli Wana Nia ovu na rasilimali za nchi!! Yaani rasilimali zetu zijadiliwe Nje ya nchi? Hii inatofauti gani na habari ya Ufaransa kudhibiti Hazina ya nchi za kiafrika zilizowahi kuwa makoloni yake?

Watueleze wamekuwa blackmailed na nani ili tufanye plans za kuwanasua kwenye mtego huo.

Mimi si mtaalamu wa sheria wala masuala ya Bunge. Yawezekana maelezo yangu haya yanatokana na umbumbumbu wangu huo. Kwa hiyo, ninaomba nisamehewe huku nikipewa maelezo yatakayonifanya niache fikra za namna hii.

Asante.
 
Back
Top Bottom