Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia Ackson achukua fomu ya Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM. Asindikizwa na mumewe

Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia Ackson achukua fomu ya Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM. Asindikizwa na mumewe

Nani kakudanganya kwamba Idadi ya Wasafwa pale mjini ni kubwa kuliko Wanyakyusa?,Jimbo la Mbeya mjini limekuwa likiongozwa na wabunge wanyakyusa kabla na pia baada ya ujio wa vyama vingi mfano Mh Mwamfupe,Mh Mwaiseje nk,

Then ndipo wakaja Mpesya na sasa Mh Sugu ambao ni makabila tofauti na Kyusa, na hata madiwani wengi pale mjini ni Wanyakyusa, wasafwa, Kinga nk,hivyo kikezo cha ukabila hakina nguvu sana kama unovyoelezea bali sifa za mgombea pia zina nafasi yake.Mh Sugu sio Msafwa lkn alishinda kwa kishindo vipindi viwili tena akimshinda mgombea wa Kisafwa.
basi ndio ivyo tena sugu kazoeleka kuliko hata mpesya, inafikia hatua wananchi wa hapa walimwita raisi wa mbeya, Nakumbuka ule mgomo wa wamachinga ilibidi aitwe yeye autulize maana hata rc alishindwa.

Mbeya mjini jimbo hili naona sugu asimikwe tu awe mbinge wa milele na hakuna tatizo😁😁
 
Ukiwa na Jicho Kali na lililotukuka kabisa la Kisaikolojia ukimuangalia huyo Mumewe hapo nyuma utagundua kuwa ' anapelekeshwa ' hadi Huruma.
ni bahati kwamba hilo jicho ulilonalo wengi hatuna kwahiyo hatuoni, achana na mahusiano ya watu.
 
Kwani sugu deni la crdb si kashalimaliza,kama bado hapo ndio mtihani ulipo.
 
Nitake radhi mkuu. Kumjua mtu sio kosa ninasema hivyo kwa sababu nimewahi kufanya nae kazi na ni rafiki yangu. Mimi sio mwanasiasa na usiingize siasa kwenye komenti yangu
Nakutaka radhi mkuu nisamehe kwa bure[emoji120]
 
Vikwazo ni vingi sana
1. Jinsia yake sio rahisi kuchagulika huku kwetu hizo ni mila na desturi
2. CCM ipo huko kondoa lakini mpaka leo kuna watu wanakosa mpaka sabuni ya kufulia nguo
3. CCM Mbeya ilishajifia miaka mingi, mnatutukana kuwa walevi na wavuta bangi basi nyie mtachaguliwa na wasiovuta wala kulewa
4. Tumejipanga maana ukisema ataleta maendeleo hata isimani kwa lukuvi hakuna kitu
5. Mbeya sio wajinga tunajielewa sana, 2015 jiwe aliambuliwa 10% ya kura zote

Sisi hatupelekeshwi tunajielewa huyo betina aende Rungwe kwao hawezi kupata ubunge kwenye aridhi ya Wasafwa
Nimekupata mkuu.... kisawa sawaaa anyway October sio mbali nitafutahi kusikia chadema tumetetea dola yetu
 
Hatimaye Siku Tuliyoisubiri imewadia Mhe. Mbunge na Naibu Spika Dkt Tulia kachukua fomu ya kugombea Ubunge wa Mbeya 2020-2025 kilichobakia tunasubiri kuapishwa kwake mjengoni mwezi wa kumi na 11.



View attachment 1506787

Hatimaye aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mbunge wa kuteuliwa,Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson ameonesha dhamiri yake yak taka kumn’goa Mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi alimaarufu “SUGU”.

Alikuwa ni majira ya saa 1.55 alfajiri Mheshimiwa huyo aliposhuka katika gari nambari za usajili T.675 Land Cruiser Prado Tx akiwa ameambatana na Mume wake James Mwanyekule na kuingia katika Ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya na kupokelewa na Katibu wa Chama hicho Wilaya,Gervas Ndaki.

Saa 2.08 asubuhi leo Julai,14,2020 amekabidhiwa fomu hiyo baada ya kupata maelekezo na taratibu za chama cha Mapinduzi ambapo kwa sehemu kubwa kwa mara ya kwanza Mume wake Mheshimiwa huyo alitumia fursa hiyo kumpigia chapuo kuwa anayo maono ya Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla hivyo wanambeya waitumie fursa hiyo ya kumtumia.

“Mimi siyo Mwanasiasa lakini siku zote za maisha yetu Mke wangu kipenzi amekuwa na ndoto na maono ya kuwatumikia wanambeya na watanzania wote kwa ujumla,name ninamuunga mkono na sote tumuunge mkono,amesema

Safari ya Tulia kuelekea kuwa Mbunge tena lakini kwa sasa kwa sura ya kupigiwa kura na wapiga kura wake imeanza leo rasmi(Julai,14,2020 majira ya saa 2.08 alfajiri)Mbeya wanahitaji Kiongozi bora na siyo bora Kiongozi.
Huyu akikosa ubunge atadata,manake kaingia gharama nyingi sana kwanza kulipia show ya Rayvanny Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine wakaingia bure bado hizo foundation zake mixer marathoni.

Wakimchinja huyu wamtafutie daktari wa saikolojia amweke sawa.
 
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Ungemjua huyo jamaa wala usingesema hayo maneno. Ndoa yao iko vizuri sana na wote ni vigogo katika Serikali hii tukufu na pia wote wana mpunga mrefu ni familia ambayo mume na mke wote wako vizuri kiuchumi na kimadaraka
Umeambiwa anapelekeshwa wewe unakuja na ngonjera za vigogo sijui Wana hela... Mengi alikuwa na hela Jaki alikuwa akimpelekesha.
 
*Matokeo ya Kura za* *maoni ngazi ya* *ubunge Mbeya* *mjini* .. *idadi* *ya* *Kura* (924)

*1Tulia Ackson* =843
2.Vikita =01.
3.Mwakipesele =11
4.Mwakaloge =2
5.Mwaifani =3
6.Bwiga =1
7.Fugale =1
8.Mabula =16
9.Mwademba= 2
10.Wagombea wengine(23) = 00
 
*Matokeo ya Kura za* *maoni ngazi ya* *ubunge Mbeya* *mjini* .. *idadi* *ya* *Kura* (924)

*1Tulia Ackson* =843
2.Vikita =01.
3.Mwakipesele =11
4.Mwakaloge =2
5.Mwaifani =3
6.Bwiga =1
7.Fugale =1
8.Mabula =16
9.Mwademba= 2
10.Wagombea wengine(23) = 00
Hizo kura 843 alizopata Tulia Ackson zote amezilipia kila moja Tsh 100,000 ambazo aligawa Jumapili tarehe 19/ 07 siku ya kuamkia uchaguzi. Yasemekana ametumia jumla ya Tsh 100 Milioni.
 
Hizo kura 843 alizopata Tulia Ackson zote amezilipia kila moja Tsh 100,000 ambazo aligawa Jumapili tarehe 19/ 07 siku ya kuamkia uchaguzi. Yasemekana ametumia jumla ya Tsh 100 Milioni.
Ubunge mtamu sana

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom