Dkt. Tulia Ackson akutana na Rais Putin kujadiliana namna bora ya kuimarisha amani duniani

Dkt. Tulia Ackson akutana na Rais Putin kujadiliana namna bora ya kuimarisha amani duniani

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Screenshot 2024-07-12 093045.png

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Mhe. Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo tarehe 12 Julai, 2024 ambapo katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.

Screenshot 2024-07-12 093130.png

Kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Dkt. Tulia amesema “Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala”.


 
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Rais wa Urusi, Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo tarehe 12 Julai, 2024 ambapo katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.
 
Inapendeza sana...
Very professional, hakuna mahali chama tawala wala serikali yake imetajwa kwa kusifiwa...

Kumbe ameshawatembelea na kuzungumza na Israel na Palestine kimya kimya...

Na akitoka hapo anaenda kuzungumza na Ukraine...


Cc: Mahondaw
 
Nilijua bongo tunajiunga brics
Itakua poa xnaa akimpa hayo maombi ikishindikana walete hata kambi zao za jeshi tz
 

Habari ndugu wananchi wa mikoa ya​

ARUSHA na KILIMANJARO...,​

Kwa mahitaji ya...,​

1.Vyumba (SINGLE SELF , DOUBLE SELF , AU VYA KAWAIDA) ,​

2. Nyumba NZIMA ZA KUPANGA ,​

3. Fremu za biashara KWA MIJI YA MOSHI na ARUSHA ,​

4. MAJENGO mazuri na yanayofaa kwa kuweka​

4.1 Ofisi za taasisi,​

4.2 GODOWN ,​

4.3 KARAKANA (WORKSHOP) ,​

4.4 Sehemu au Jengo la kila aina ya shughuli za kiuchumi 5.MASHAMBA Kwa ajili ya kilimo , ufugaji​

6.Viwanja kwa ajili ya makazi vipo​

6.FULL FURNISHED APARTMENTS ZENYE KILA KITU NDANI ....​


kwa MOSHI na ARUSHA WASILIANA NAMI..​

0672701329/0756294771​




NB. MAELEKEZO YA KINACHOFANYIKA BAADA YA MTEJA KUKUBALI NA KURIDHIKA NA PRODUCT NI KUKUTANISHWA NA MMILIKI HALALI ................


DALALI Lexus SUV
Hii nini tena huku?
 
mhh spika anakimwaga naimagine ningekua mimi apo

Ni kupoteza muda. Labda kama lengo ni kupiga picha.

Putin ameshasema kuwa hayupo tayari kuacha vita ya uvamizi, labda aachiwe maeneo yote ya Ukraine aliyoyavamia. Kakataa kuwasikiliza hata marafiki zake mataifa makubwa kama China na India, halafu akamsikilizeTulia!!

Tulia amefanikiwa kupata picha na posho isiyo haba.
 
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Mhe. Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo tarehe 12 Julai, 2024 ambapo katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.Kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Dkt. Tulia amesema “Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala”

Chanzo na jionee:


View: https://youtu.be/KLkGw9pwbao?si=EtkIJ-rpRE3dgZzv
 
Back
Top Bottom