Dkt. Tulia Ackson akutana na Rais Putin kujadiliana namna bora ya kuimarisha amani duniani

Halijiwezi kwasabab ndani ya serikali ya Congo kuna viongozi ambao wana asili ya Rwanda Bhrundi Uganda na pia Tanzania
DRC walifocus zaidi ukanda huo wa Kinshasa ila mashariki ni kama walipatenga,,,,,,ukiangalia wanajeshi wao wengi upande wa mashariki discipline hamna, vifaa shida hata malipo shida ndo maana wengi morale na vita hawana na pia rahisi kutumika na maadui sababu ya shida zao
Ukipata muda angalia hio video,,,kuna mwanajeshi wa serikali ukanda huo ukisikia mshahara anaolipwa aibu, ndo maana yeye na mkewe wamefocus sana kwenye biashara ya bangi na mzigo wanachukuaga pia hadi kwenye maeneo yanayoshikiliwa na waasi, wao kikubwa maisha yasonge


View: https://youtu.be/REu0M_naDIs?si=BjcXQ3fiynGFQjCV
 
Namfurahia sana madame Spika wetu Dr.Tulia Akson kwa namna anavyofanya bidii sana katika mazoezi ya kua makamu wa Rais na baadae mwanamke wa pili Tanzania na Rais kamili, Amer Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania 🐒

well done comrade Dr Tulia Akson 💪
 
Yaani Waafrika wote tunashoindwa kutatuwa matatizo yetu wenyewe?

Mimi nasema ili Kongo pakae sawa, wageni wote waondoke, waachwe wenyewe wauwane mpaka wafikie mwisho wa kuuwana. Wasiingilliwe na yeyote.
Unadhani nani wa kuwaondoa pale wakati Wana nguvu pale...Russia ai intervine.
 

Inachekesha sana. Sijui wanazungumza nini katika levels gani globally. Inawezekana wanajadili issue za ukaidi wa Mpina 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Anatafuta ukatibu mkuu wa umoja wa mataifa
 
Hiyo picha imekaa vizuri Tulia yuko vizuri kichwani yuko peke yake na balozi tu ujumbe wa urusi watatu.Putin ,Speaker na mkalimani wa kirusi na kingereza

Sii kama ile ya ziara ya Rais Samia Korea kusini wakorea watatu watanzania karibu 30

Hii mechi ya Urusi iko vizuri kuliko ile ya Korea kusini

Tanzania kwenye vitu serious itume watu wenye akili

Nimependa hii picha ya majadiliani

Ile picha ya majadiliano Korea kusini ilikuwa aibu kwa nchi halafu hata haikuwa high level kama hii

Angalia mtoto wa kike wa kinyakyusa akiongea kwa confidence kwa raisi wa Taifa kubwa duniani la Russia kwa kujiamini na utulivu ki executive

Putin hasikilizi wajinga wajinga ndio maana katulia vinginevyo angemtuma tu spika wa bunge Duma au waziri wa mambo ya nje Lavrov aongee naye sio yeye personality
 
Jimbo la mbeya ,Sugu analitaka, ili tulia abakie na bunge la dunia
Na bunge la dunia hupewi iwapo wewe si mbunge katika nchi yako, kwa maana nyingine, Sugu hata akishinda kwa kura milioni saba, hawezi kutangazwa
 
Kwa hiyo tutegemee soon jeshi letu imara kwenda kumsaidia kazi Putin?

Nategemea baada ya hapa gharama ya ngano na mafuta itashuka.

Halafu Tanzania ifanye Kirusi kuwa lugha ya taifa, maana ni kama kinaendana sana na Kiswahili.

Inglishi ifutwe kabisa, inawachanganya sana Wabongo.
 
Inapendeza sana...
Very professional, hakuna mahali chama tawala wala serikali yake imetajwa kwa kusifiwa...

Kumbe ameshawatembelea na kuzungumza na Israel na Palestine kimya kimya...

Na akitoka hapo anaenda kuzungumza na Ukraine...


Cc: Mahondaw
Asante kwa taarifa lo
 
Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Mhe. Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo tarehe 12 Julai, 2024 ambapo katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.
Teh teh teh 😃 😃 kazi kweli kweli
 
Na Samia pale alikuwa anaongea na nani? Rais wa Korea?

Samia atawaumiza sana mioyo, lakini mkubuke tu, kazi ya Allah haina makosa.
 
Inachekesha sana. Sijui wanazungumza nini katika levels gani globally. Inawezekana wanajadili issue za ukaidi wa Mpina 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Ikiwa unachosoma hukielewi basi hata kusikiliza huwezi?

Kuna video na kinachozungumzwa siyo siri. Umekurupuka bila kuisikiliza wala kuitazama video.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…