Dkt. Tulia Ackson alilenga nini kupotosha kuwa mhimili mmoja ni mkubwa kuliko miingine? Alijikosha, alijipendekeza?

Yupo sahihi na kihalisia ndivyo ilivyo. Ametujulisha tu hali halisi. Cha msingi labda tupambane tuondokane na hali hiyo. Lakini kusema hayupo sahihi ni kufukia kichwa mchangani.
 
Kila nikijaribu kukumbuka na kutafakari zaidi kuhusu kauli za huyu Mama alizozitoa mbele ya Rais wa JMT kuwa mihimili yote haiko sawa, kwamba mhimili wa dola ni mkubwa zaidi kuliko miingine. Hii kauli binafsi naichukulia kua ni ya kujikosha na kujipendekeza, si kauli ya kutamka kwenye media mbele ya macho ya umma.

Spika wa aina ya Dkt Tulia hata kama kuna jambo linalohatarisha ustawi wa taifa ikatokea likafanywa na serikali ataangalia tu wala hatofanya uamuzi wowote kwa vile dola ndio mhimili mkuu? Maana Dola siyo Mungu wala malaika kwamba haikosi.

Tunatambua kua kwa katiba yetu hii iliyopo dola ndiyo kila kitu lakini usiifanye mihimili miingine kutokujiamulia mambo yake ya uhuru, lakini kila mhimili una mipaka ya majukumu yake huru bila kuingiliwa na mwingine. Huyu alimaamisha kwamba Ndungai alikosea kwa kauli zake? Alikuwa anamaanisha kua mhimili wa bunge si lolote wala chochote?

Tukiwa na bunge chini Spika aina ya Dkt Tulia ni hatari sana kwa ustawi wa taifa na kwa maslahi vya taifa. Niwashauri wanaccm wenzangu, hata kama kuna wakati tunatakiwa kulinda maslahi vya chama lakini Dkt Tulia hafai kabisa . Huyu mwanamama anataka kulitia bunge Kibogoyo liwe kama mihuri wa gogongea kupitisha hoja za serikali hata kama hazifai.

Hawa ndio wasomi wetu, wapo radhi kupotosha ili kulinda maslahi yao binafsi.Haijalishi wewe ni CCM au upinzani, tafadhali kemea watu wa aina hii kwa maslahi ya taifa letu. Tuachane na watu aina ya Tulia hawatufai.
Dola ndio mhimili mkuu wacheni ubushlawyer. Tulia ni mwanasheria kasema sawa. Mihimili mingine ina wajibu zake za kikatiba japo mhimili mkuu inabidi kuheshimu bila kuingilia mihimili minginem mihimili mingine ina wajibu kuheshimu dola bila kuingilia kazi zake kama ilivyobanishwa na katiba.
Kama dola sio mhimili mkuu nyie bushlawyers jibuni hili.
Jeshi wakipindua au nchi ikivamiwa kwa nini wanakimbilia kuteka ikulu na ndio kilele cha wao kupindua au kuteka nchi? Sijawahi kuona au kusikia jeshi au adui eti wameteka mahakama kuu au bunge kisha kutangaza wamechukua madaraka kutawala nchi hiyo. 🙄
 
Hii ndio hulka ya ma- dr na ma- propesa wa Tz ni majanga matupu. Ndio maana kuna wakati namuona msukuma ana nafuu kuliko hawa watu 😄
 
Tulia alikuwa anaongea legally na administatively.

Nchi ina dola ambayo ina mihimili mitatu, executive ambayo inatoa mkuu wa nchi, amri jeshi mkuu na kiongozi wa serikali. Huyu ana mandate ya kukusanya kodi na kuwagawia mahakama ili wajiendeshe, kuwagawi bunge ili wajiendeshe.

JPM aliwahi kumjibu Paskali Mayalla kuwa, kuna mhimili "ulijichimbia chini zaidi".

Rais kama mkuu wa nchi, picha yake inakaa mahakamani kwa nafasi ya ukuu wa nchi. Rais picha yake iko bungeni kwa nafasi ya ukuu wa nchi. Lakini hakuna picha ya spika mahakamani, wala hakuna picha ya jaji mkuu bungeni au ofisi yoyote ya serikali.

Pengine siku tukipata katiba mpya kama tunataka, tuwe na mfumo kama Israel, Uingereza au Ujerumani. Rais awe mkuu wa nchi ceremonious ila tuwe na waziri mkuu ambae atakuwa ni kiongozi wa serikali na CinC ambae bado nafasi yake ya kukusanya kodi na mahakama na bunge kuleta "bakuli"' bado kunamfanya kiongozi wa serikali kuwa na uzito sana ukilinganisha na wenzie kwenye judiciary na legislature.

Kwa umasikini ulio nchini na fursa zilizo nchini, tungekuwa na think tank ya nini tufanye walau nchi yetu iongeze export earnings izalishe ajira ipuze imports kwa kukuza uwekezaji nchini.

Haya tunayoyajadili, hao wakuu wa bunge, serikali na mahakama, posho zao za ustaafu zimenona kweli. Ni lini walala hoi nao wataona fursa ya kuzalisha wakauza kwa bei nzuri kwa soko linaloeleweka na bei nzuri ili hata wakitaka nao kusomesha watoto wao Feza wawe na financial muscles.

J3 njema.
Hata kwa katiba ya sasa serikali inatakiwa ipate kibali cha kukusanya kodi yoyote kutoka bungeni na bunge ndilo linatakiwa liridhie mipango yote ya serikali. Bahati mbaya sana bunge letu limekuwa la kugonga muhuri tu mambo ya serikali badala ya kuwa msimamizi na muwajibishaji wa serikali.

Katiba ya JMT, 1977
136.-(1) Fedha hazitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa ajili ya matumizi ila kwa mujibu wa masharti yafuatayo:- (a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na idhini hiyo iwe imetolewa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote; (b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa ama na sheria ya Matumizi ya Serikali iliyotungwa mahsusi na Bunge au sheria iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 140 ya Katiba hii.

138.-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria na sheria iliyotungwa na Bunge.
 
Kuna sheria inayotaka picha ya Rais kuwekwa bungeni na mahakamani?
Kwa nini picha ya Rais inawekwa hata kwenye kampuni binafsi za watu?
Tulia alikuwa anaongea legally na administatively.

Nchi ina dola ambayo ina mihimili mitatu, executive ambayo inatoa mkuu wa nchi, amri jeshi mkuu na kiongozi wa serikali. Huyu ana mandate ya kukusanya kodi na kuwagawia mahakama ili wajiendeshe, kuwagawi bunge ili wajiendeshe.

JPM aliwahi kumjibu Paskali Mayalla kuwa, kuna mhimili "ulijichimbia chini zaidi".

Rais kama mkuu wa nchi, picha yake inakaa mahakamani kwa nafasi ya ukuu wa nchi. Rais picha yake iko bungeni kwa nafasi ya ukuu wa nchi. Lakini hakuna picha ya spika mahakamani, wala hakuna picha ya jaji mkuu bungeni au ofisi yoyote ya serikali.

Pengine siku tukipata katiba mpya kama tunataka, tuwe na mfumo kama Israel, Uingereza au Ujerumani. Rais awe mkuu wa nchi ceremonious ila tuwe na waziri mkuu ambae atakuwa ni kiongozi wa serikali na CinC ambae bado nafasi yake ya kukusanya kodi na mahakama na bunge kuleta "bakuli"' bado kunamfanya kiongozi wa serikali kuwa na uzito sana ukilinganisha na wenzie kwenye judiciary na legislature.

Kwa umasikini ulio nchini na fursa zilizo nchini, tungekuwa na think tank ya nini tufanye walau nchi yetu iongeze export earnings izalishe ajira ipuze imports kwa kukuza uwekezaji nchini.

Haya tunayoyajadili, hao wakuu wa bunge, serikali na mahakama, posho zao za ustaafu zimenona kweli. Ni lini walala hoi nao wataona fursa ya kuzalisha wakauza kwa bei nzuri kwa soko linaloeleweka na bei nzuri ili hata wakitaka nao kusomesha watoto wao Feza wawe na financial muscles.

J3 njema.
 
Hakuna Sehemu Tulia kakosea alichosema Tulia ndio uhalisia nyingine ni porojo tu, raisi ni mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu, mkuu wa Serikali na zaidi ni mwenyekiti wa chama, unamlinganisha na CJ au Spika kweli?.

Hawa hazi zao ni sawa na mawaziri tu, kwanza hata shughuli zao za kila siku zinategemea wizara kwa mfano Mahakama inaitegemea wizara ya katiba na sheria hali kadhalika bunge
 
Kila nikijaribu kukumbuka na kutafakari zaidi kuhusu kauli za huyu Mama alizozitoa mbele ya Rais wa JMT kuwa mihimili yote haiko sawa, kwamba mhimili wa dola ni mkubwa zaidi kuliko miingine. Hii kauli binafsi naichukulia kua ni ya kujikosha na kujipendekeza, si kauli ya kutamka kwenye media mbele ya macho ya umma.

Spika wa aina ya Dkt Tulia hata kama kuna jambo linalohatarisha ustawi wa taifa ikatokea likafanywa na serikali ataangalia tu wala hatofanya uamuzi wowote kwa vile dola ndio mhimili mkuu? Maana Dola siyo Mungu wala malaika kwamba haikosi.

Tunatambua kua kwa katiba yetu hii iliyopo dola ndiyo kila kitu lakini usiifanye mihimili miingine kutokujiamulia mambo yake ya uhuru, lakini kila mhimili una mipaka ya majukumu yake huru bila kuingiliwa na mwingine. Huyu alimaamisha kwamba Ndungai alikosea kwa kauli zake? Alikuwa anamaanisha kua mhimili wa bunge si lolote wala chochote?

Tukiwa na bunge chini Spika aina ya Dkt Tulia ni hatari sana kwa ustawi wa taifa na kwa maslahi vya taifa. Niwashauri wanaccm wenzangu, hata kama kuna wakati tunatakiwa kulinda maslahi vya chama lakini Dkt Tulia hafai kabisa . Huyu mwanamama anataka kulitia bunge Kibogoyo liwe kama mihuri wa gogongea kupitisha hoja za serikali hata kama hazifai.

Hawa ndio wasomi wetu, wapo radhi kupotosha ili kulinda maslahi yao binafsi.Haijalishi wewe ni CCM au upinzani, tafadhali kemea watu wa aina hii kwa maslahi ya taifa letu. Tuachane na watu aina ya Tulia hawatufai.
Alikuwa sahihi na ataendelea kuwa Sahihi siku zote. Danganyaneni tu lakini hivi vitu havilingani na havitalingana
 
Hakuna Sehemu Tulia kakosea alichosema Tulia ndio uhalisia nyingine ni porojo tu, raisi ni mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu, mkuu wa Serikali na zaidi ni mwenyekiti wa chama, unamlinganisha na CJ au Spika kweli?.

Hawa hazi zao ni sawa na mawaziri tu, kwanza hata shughuli zao za kila siku zinategemea wizara kwa mfano Mahakama inaitegemea wizara ya katiba na sheria hali kadhalika bunge
Kojoa ulale mihimili iko sawa
 
Katiba inasema Rais ni Mkuu wa nchi. Sura ya pili, ibara ya 33, kifungu cha kwanza.

Which means Rais yuko juu ya kila kitu na kila mtu, anaweza kumtaka hata mkeo kinguvu, kama chifu wa makabila. Tulia Ackson yuko sahihi.

Mkenge mwingine huu aliotuingiza Nyerere, u-chifu wa kwao.

Siku ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mwaka jana mwanae Makongoro alisema babu yake alikuwa chifu, na bibi yake (aliyemzaa Mwalimu) alitakwa kuolewa kinguvu na chifu Burito, kijiji cha mwanamke kikasema binti hataki, Chifu Burito akasema anhaa, nakata huduma zote za kijamii kwenda Busegwe, Busegwe wakaambiana kijiji is bigger than kibinti kimoja, wakamwachia, binti Mgaya akaja kuchukuliwa mzega mzega kwenda Butiama, akamzaa Mwalimu kinguvu. Some serious stuff but typical Makongoro, he was laughing like a drunken sailor.

Ndo huu Urais wa ki-chifu aliotuletea Mwalimu. And he had brass set, anadiriki kusema angetaka angeweza kuwa dikteta, katiba inamruhusu. Mbona hukuibadilisha? Miaka 29. Baba wa Taifa uchwara wa dunia ya tatu.
 
Mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu, mkuu wa serikali ni sawa na jaji mkuu au spika? Acheni ujinga wenu, Chuki zenu kwa Samia zisiwatoe ufahamu
 
Nani anakagua Gwaride? Nani anapigiwa saluti na mkuu wa majeshi? Rais ni zaidi ya mihimili yote
 
Sikujua kama watu wengi hivi hawana elimu ya uraia. Separation of powers haina maana ya kuwa mihimili ipo sawa.
 
Back
Top Bottom