Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303

Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303

Sasa hivi hapa nchini demokrasia ikichezewa tunaambiwa ni ili nchi ijengwe. Sasa huko Africa kusini nchi haikuwa inajengwa na hao makaburu?

Narudia tena, tena sio wizi, Bali mchakato wa uchaguzi uliporwa kabisa, na ushahidi upo. Kwa kukusaidia ingia kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi kama matokeo ya uchaguzi ule yapo. Sikatai kuwa hakuna sehemu ccm ilishinda kihalali, lakini asilimia kubwa ulikuwa ni uchafu wa dhahiri.

Wapinzani hawajaja na mawazo mbadala kwa mtazamo wa kiccm. Wananchi ndio wanaoamua kipi wanataka, na sio utashi wa ccm. Ndio maana tunataka uchaguzi wa halali ili matakwa halisi ya wananchi yafahamike, na sio matokeo yatangazwe kwa utashi wa genge liitwalo ccm. Na uchaguzi ukiwa wa halali hakuna uwezekano wa ccm kufikia 2/3 ya kura za nchi hii, na haitakaa ipate zaidi ya hapo. Na uwezekano ni kutoka madarakani kabisa kutokana na mabadiliko ya kizazi.
Kwa maandishi yako naona mna miaka mingi mbeleni ya kulialia humu jukwaani.
 
Ulitakaje labda?
Tuanza kuitazama dunia halisi na sio kila kitu kudai mnaibiwa kura. Serikali inafanya mambo mengine usiku na mchana na yanagusa moja kwa moja maisha ya wananchi, kudai kuwa serikali haikubaliki kwa wananchi ni kujifariji tu.
 
Sijawahi kusoma hizi "toilet paper" zako mwanzo hadi mwisho zaidi ya kichwa cha habari ambacho niligundua hakiendani na maudhui yanaoandikwa baada.

Pia unavyohitimisha tu inaonyesha kichwani hazimo sawa sawa jina lako tu unaanzia na herufi ndogo ! na uzalendo bandia wa kutuwekea namba za simu humu sijui unataka michango ya chakula?

Hazina tofauti na matoilet paper awamu ya 5 zile Tanzanite na Jamvi la habari
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa umoja wa mabunge duniani(IPU) leo Octoba 27, 2023. Kura 303 zilipigwa huku mshindi akihitaji angalau nusu ya kura hizo(kura 152)

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Ms. Adji Diarra Mergane Kanouté(Senegal) kura 52
Ms. Catherine Gotani Hara(Malawi) kura 61
Ms. Marwa Abdibashir Hagi(Somalia) kura 11
Ms. Tulia Ackson(United Republic of Tanzania) kura 172

Dkt. Tulia Ackson anachukua nafasi Duarte Pacheco kutoka Portugal aliyechaguliwa mwaka 2020 baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kupitia mtandao kutokana na janga la COVID-19 lililokuwa linaikabili dunia.

Kwa miaka 25 sasa urais wa IPU umetawaliwa na wabunge kutoka Misri, Hispania, India, Italia, Namibia, Morocco, Bangaladesh, Mexico na Portugal.

Dr. Tulia Ackson anakuwa Rais wa 31 wa IPU na amechaguliwa kwenye bunge la 147 la IPU lililofanyika mjini Luanda, Angola kutoka Oktoba 23 mpaka Oktoba 27.

Rais wa IPU ni kiongozi wa kisiasa wa taasisi hiyo, anaongoza vikao vyote vya taasisi hiyo na anaiwakilisha kwenye matukio ya kimataifa. Rais wa IPU anaongoza muhula wa miaka mitatu. Rais lazima awe mbunge kipindi chake chote cha miaka mitatu ya Urais.

IPU ilianzishwa mwaka 1889 kama kundi dogo la mabunge na kukua kwa kasi kama taasisi ya kimataifa ikijishughulisha na kukuza demokrasia, usawa, haki za kibinadamu, maendeleo na amani.

IPU ina wanachama 180 kati ya nchi 193 zilizopo duniani. Mabunge yote yaliyoanzishwa kisheria na nchi zao au mataifa yanayotambulika na umoja wa mataifa yanarusiwa kuwa mwanachama wa IPU.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, akiwasili katika Ukumbi wa Bunge la Angola leo tarehe 27 Oktoba, 2023 wakati wa Mkutano wa 147 unaoendelea Jijini Luanda, Angola.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.
Ni Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Tanzania ambaye ni Mgombea wa IPU akiomba kura.
Screenshot_20231028-215308_1.jpg
 
Tuanza kuitazama dunia halisi na sio kila kitu kudai mnaibiwa kura. Serikali inafanya mambo mengine usiku na mchana na yanagusa moja kwa moja maisha ya wananchi, kudai kuwa serikali haikubaliki kwa wananchi ni kujifariji tu.
Serekali sio ccm, hata likiingia jeshi madarakani litaunda serekali. Tunasema uchaguzi halali ccm haitaweza kuunda serekali na kupitisha chochote watakavyo. Hakuna kizazi Cha kuipa kura zaidi ya 50%. Huo wizi ama uporaji wa mchakato uko wazi Wala sio wa kutafuta, na uchafu wa uchaguzi ushahidi upo.

Sheria inataka matokeo ya uchaguzi yawepo kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi, ingia Uniambie kama utaona matokeo ya uchaguzi uliopita. Kama ulikuwa ni uchaguzi wa haki kwanini wasite kuweka matokeo?
 
Back
Top Bottom