Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303

Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303

Wewe endelea na mibangi yako mpaka utakapoanza kuokota mimakopo majalalani
Huna faida hata kwenye maisha yako mwenyewe....umeijuwa lini CCM wewe kuwa na papara kiasi hicho kama mavi yakuharisha? Hilo lichama chakavu lina wenyewe , ndiwo wale wanateuliwa bila kwanika namba zawo za simu mitandaoni.Wewe baki na mavi yako ukishiba magimbi na parachichi huko kijijini kwenu.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa umoja wa mabunge duniani(IPU) leo Octoba 27, 2023. Kura 303 zilipigwa huku mshindi akihitaji angalau nusu ya kura hizo(kura 152)

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Ms. Adji Diarra Mergane Kanouté(Senegal) kura 52
Ms. Catherine Gotani Hara(Malawi) kura 61
Ms. Marwa Abdibashir Hagi(Somalia) kura 11
Ms. Tulia Ackson(United Republic of Tanzania) kura 172

Dkt. Tulia Ackson anachukua nafasi Duarte Pacheco kutoka Portugal aliyechaguliwa mwaka 2020 baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kupitia mtandao kutokana na janga la COVID-19 lililokuwa linaikabili dunia.

Kwa miaka 25 sasa urais wa IPU umetawaliwa na wabunge kutoka Misri, Hispania, India, Italia, Namibia, Morocco, Bangaladesh, Mexico na Portugal.

Dr. Tulia Ackson anakuwa Rais wa 31 wa IPU na amechaguliwa kwenye bunge la 147 la IPU lililofanyika mjini Luanda, Angola kutoka Oktoba 23 mpaka Oktoba 27.

Rais wa IPU ni kiongozi wa kisiasa wa taasisi hiyo, anaongoza vikao vyote vya taasisi hiyo na anaiwakilisha kwenye matukio ya kimataifa. Rais wa IPU anaongoza muhula wa miaka mitatu. Rais lazima awe mbunge kipindi chake chote cha miaka mitatu ya Urais.

IPU ilianzishwa mwaka 1889 kama kundi dogo la mabunge na kukua kwa kasi kama taasisi ya kimataifa ikijishughulisha na kukuza demokrasia, usawa, haki za kibinadamu, maendeleo na amani.

IPU ina wanachama 180 kati ya nchi 193 zilizopo duniani. Mabunge yote yaliyoanzishwa kisheria na nchi zao au mataifa yanayotambulika na umoja wa mataifa yanarusiwa kuwa mwanachama wa IPU.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, akiwasili katika Ukumbi wa Bunge la Angola leo tarehe 27 Oktoba, 2023 wakati wa Mkutano wa 147 unaoendelea Jijini Luanda, Angola.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.
Ni Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Tanzania ambaye ni Mgombea wa IPU akiomba kura.
Akili, za, CCM, hovyo kabisa, asilimia 56! Ndio kishindo?
Kwenye watu kumi, wanne hawakumpa kura! So pathetic
 
Kila la kheri zake... Ni macho yangu au ni kweli nimemuona January Makamba...
 
Tunaweka kumbukumbu sahihi. Kuwa Jimbo la Mbeya Mjini tumetoa Rais wa Mbunge yote duniani. Tofaut na Mbunge Mstaafu ambae watu wanadai hajui hata kuandika.
Nataka nijue kuwa wewe uliishia darasa la ngapi? Ulimalisa hata darada la nne au uliishia chekechea? Nauliza tu!
 
Dr Tulia ni Mtetezi wa wasio na sauti pia

kuna Waziri Mmoja Bungeni juzi alijipa kazi ya kuamua nyimbo ipi ina maadili na ipi haina maadili wakati wenye Mamlaka Basata wameiruhusu

alajikuta anawaonea Wakuu wa shule kwa kosa la Watoto kucheza nyimbo ambayo haijawahi kuzuiwa na Mamlaka husika
 
Tunaweka kumbukumbu sahihi. Kuwa Jimbo la Mbeya Mjini tumetoa Rais wa Mbunge yote duniani. Tofaut na Mbunge Mstaafu ambae watu wanadai hajui hata kuandika.
Sawa ila nawewe weka vyeti vyako hapa ili tutofautishe na mbunge wa zamani kuliko kumkashfu mtu kisa kukosa nidhamu kuwa wewe jitoto la kugombolewa.
 
Tunaweka kumbukumbu sahihi. Kuwa Jimbo la Mbeya Mjini tumetoa Rais wa Mbunge yote duniani. Tofaut na Mbunge Mstaafu ambae watu wanadai hajui hata kuandika.
Mabunge yote kama ili la Tanzania! Mambogani unatuletea wewe
 
Back
Top Bottom