Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa umoja wa mabunge duniani(IPU) leo Octoba 27, 2023. Kura 303 zilipigwa huku mshindi akihitaji angalau nusu ya kura hizo(kura 152)
Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Ms. Adji Diarra Mergane Kanouté(Senegal) kura 52
Ms. Catherine Gotani Hara(Malawi) kura 61
Ms. Marwa Abdibashir Hagi(Somalia) kura 11
Ms. Tulia Ackson(United Republic of Tanzania) kura 172
Dkt. Tulia Ackson anachukua nafasi Duarte Pacheco kutoka Portugal aliyechaguliwa mwaka 2020 baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kupitia mtandao kutokana na janga la COVID-19 lililokuwa linaikabili dunia.
Kwa miaka 25 sasa urais wa IPU umetawaliwa na wabunge kutoka Misri, Hispania, India, Italia, Namibia, Morocco, Bangaladesh, Mexico na Portugal.
Dr. Tulia Ackson anakuwa Rais wa 31 wa IPU na amechaguliwa kwenye bunge la 147 la IPU lililofanyika mjini Luanda, Angola kutoka Oktoba 23 mpaka Oktoba 27.
Rais wa IPU ni kiongozi wa kisiasa wa taasisi hiyo, anaongoza vikao vyote vya taasisi hiyo na anaiwakilisha kwenye matukio ya kimataifa. Rais wa IPU anaongoza muhula wa miaka mitatu. Rais lazima awe mbunge kipindi chake chote cha miaka mitatu ya Urais.
IPU ilianzishwa mwaka 1889 kama kundi dogo la mabunge na kukua kwa kasi kama taasisi ya kimataifa ikijishughulisha na kukuza demokrasia, usawa, haki za kibinadamu, maendeleo na amani.
IPU ina wanachama 180 kati ya nchi 193 zilizopo duniani. Mabunge yote yaliyoanzishwa kisheria na nchi zao au mataifa yanayotambulika na umoja wa mataifa yanarusiwa kuwa mwanachama wa IPU.
========
Ndugu zangu Watanzania,
Mungu ni mwema, asanteeee sana kwa maombi yenu watanzania wenzangu kwa dada yetu na speaker wetu Dkt. Tulia Ackson.
Habari njema ni kuwa tayari ameibuka kidedea kwa kishindoo kikuu kilichoitetemesha Dunia kwa kupata kura 172 huku anayemfuatia kwa mbali kama kama kichuguu na mlima akiambulia kura 61.huu ni ushindi kwetu sote watanzania tunapaswa kuendelea kuishangilia kwa furaha zote na kujivunia dada yetu aliyetuheshimisha kama Taifa.
Ameonyesha uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kujenga hoja zenye ushawishi na mvuto kwa wapiga kura.kwa hakika Mungu wa Dr Tulia ni mkubwa sana na Anaendelea kuonyesha maajabu na kumtendea makubwa sana Dr Tulia.Mungu anamakusudi maalumu ya kumuumba Dr Tulia,ndio maana mnaona namna ambavyo Anaendelea kupata kibali cha kukubalika,kupendwa,kuungwa mkono na kuchaguliwa kila jina lake linapotua na kuwekwa mezani.
Binafsi nilimuombea sana dada yangu Dr Tulia,usiku na mchana nilifanya kazi ya kumuomba Mungu amsaidie.niliwaomba watanzania wenzangu tuunganishe maombi yetu kwa ajili ya kumuombea speaker wetu ,maana nilijuwa ushindi wa Dr Tulia ni ushindi wetu sote watanzania. Kwa imani nilijuwa ni lazima Dr Tulia Ashinde kwa kishindo na niliandika hata humu jukwaani kuwa Dr Tulia ndiye Rais ajaye wa IPU. Nilisema kwa uwezo wake mkubwa alio nao,Elimu yake,uwezo wa kujenga hoja na kupangua hoja kwa hoja ni vitu na mambo yanayombeba sana Dr Tulia.
Ndugu zangu Watanzania kwa namna Dr Tulia alivyogusa maisha ya wana Mbeya na nyanda za juu kusini nilikuwa naona kabisa ni lazima Mungu awe na Dr Tulia. maandiko kutoka katika biblia yanasema kuwa agusaye na kuwasaida maskini amemkopesha Mungu na kwamba atamlipa kwa mema na mazuri. Dr Tulia amesaidia watu wengi sana waliokuwa katika hali ya umaskini,amesaidia vijana,yatima,wazee ,wajane na watu wegi wenye uhitaji kwa kuwapa misaada ya kila aina na hatimaye kuwafanya kupata matumaini kutoka katika hali ya kukata Tamaa,imeinua matumaini ya wengi na kugusa mioyo ya wengi iliyokuwa imekata Tamaa.
Tabia njema ya Dr Tulia,ucha Mungu wake, kumtumikia na kumtumainia Mungu wake vimeendelea kuwa nguzo na ngao ya mafanikio kwa Dr Tulia. Ambaye amekulia na kutoka familia ya kipato cha chini kabisa huku wazazi wake wakiwa maskini.lakini aliendelea kumuamini Mungu na kupambana mpaka hapo alipofika leo hii kupata heshima ya Dunia.huu ni ushuhuda wa kuwa Mungu anaweza Muinua yeyote na kumketisha juu mahali waketipo wafalme.leo Dr Tulia ameinuliwa kwa mara nyingine tena na kumketisha mahali ambapo mtoto kutoka familia ya kipato cha chini au maskini kabisa cha kutegemea kuuza mchicha na vibama hawezi kuamini kuwa anaweza kufika alipofika Dr Tulia.
Mungu huwainua wanyonge na kuwapa nguvu,huviinua vitu vinyonge na kuvitia nguvu,huwainua wale wadhalauliwao na kuwapa heshima kuu ili watu wajuwe ya kuwa Mungu ni Mungu tu na ndiye awezaye kumfanya yeyote yule kuwa chochote na yeyote na kuweza kushika nafasi yeyote ile. Mungu siyo kama mwanadamu ambaye huwapanga watu katika matabaka,Mungu ni wa wote.
Usikate Tamaa ewe Mtanzania mwenzangu upitiaye magumu, kudhalilishwa,kudharauliwa na wenye mali,kunyanyasika na kubezwa.mtumainie na kumwamini Mungu tu kuwa ipo siku anaweza kukuinua na kukuweka juu.pia katika kuinuliwa kwako usiache kusaidia wenye shida,uhitaji.mpende kila mtu na mheshimu kila mtu maana huwezi kujuwa baraka zako zimebebwa na nani na zitapita kwa nani maana Mungu hutenda miujiza kupitia watu.hivyo usimdharau mtu kwa kuwa hujuwi kesho yake itakuwaje kulingana na Agano lake na Mungu wake tangia akiwa Tumboni mwa mama yake.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
View attachment 2794625View attachment 2794748
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, akiwasili katika Ukumbi wa Bunge la Angola leo tarehe 27 Oktoba, 2023 wakati wa Mkutano wa 147 unaoendelea Jijini Luanda, Angola.
View attachment 2794749
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.
View attachment 2794755
Ni Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Tanzania ambaye ni Mgombea wa IPU akiomba kura.