Kwa taarifa yako kwa uchaguzi halali Leo hii ccm isingekuwa madarakani, na kama ingefanikiwa kuwepo isingekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi watakavyo. Na iwapo hizo pesa za wananchi zingetumika vizuri, Leo hii tusingekuwa na huu mgao ww umeme wa kipuuzi.
Ccm kukaa madarakani kwa shuruti sio jambo la Siri tena, liko wazi mno. Na hakuna chama chochote kitakachoshindwa kufanya wafanyacho ccm. Hiki sio kizazi Cha ccm, ndio maana inalazimisha kubaki madarakani kwa kisingizio Cha kujenga madaraja, sijui shule nk, kana kwamba kufanya hivyo ni jambo lisilowezekana na wengine.
Hiyo njia ya kura ni kama imeshapoteza uhalali kwa ule uhayawani tunaouona wakati wa uchaguzi, na ni mtu asiyejitambua tu anaweza kuendelea kwenda kupanga mstari kwenye kituo Cha kura eti anachagua kiongozi. Fuatilia chaguzi za marudio na zijazo zotakavyokuwa na wapiga kura wachache, na sababu hasa ni ccm kudharaulisha box la kura wakati kizazi hiki hakiitaki.