Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa umoja wa mabunge duniani(IPU) leo Octoba 27, 2023. Kura 303 zilipigwa huku mshindi akihitaji angalau nusu ya kura hizo(kura 152)

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Ms. Adji Diarra Mergane Kanouté(Senegal) kura 52
Ms. Catherine Gotani Hara(Malawi) kura 61
Ms. Marwa Abdibashir Hagi(Somalia) kura 11
Ms. Tulia Ackson(United Republic of Tanzania) kura 172

Dkt. Tulia Ackson anachukua nafasi Duarte Pacheco kutoka Portugal aliyechaguliwa mwaka 2020 baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kupitia mtandao kutokana na janga la COVID-19 lililokuwa linaikabili dunia.

Kwa miaka 25 sasa urais wa IPU umetawaliwa na wabunge kutoka Misri, Hispania, India, Italia, Namibia, Morocco, Bangaladesh, Mexico na Portugal.

Dr. Tulia Ackson anakuwa Rais wa 31 wa IPU na amechaguliwa kwenye bunge la 147 la IPU lililofanyika mjini Luanda, Angola kutoka Oktoba 23 mpaka Oktoba 27.

Rais wa IPU ni kiongozi wa kisiasa wa taasisi hiyo, anaongoza vikao vyote vya taasisi hiyo na anaiwakilisha kwenye matukio ya kimataifa. Rais wa IPU anaongoza muhula wa miaka mitatu. Rais lazima awe mbunge kipindi chake chote cha miaka mitatu ya Urais.

IPU ilianzishwa mwaka 1889 kama kundi dogo la mabunge na kukua kwa kasi kama taasisi ya kimataifa ikijishughulisha na kukuza demokrasia, usawa, haki za kibinadamu, maendeleo na amani.

IPU ina wanachama 180 kati ya nchi 193 zilizopo duniani. Mabunge yote yaliyoanzishwa kisheria na nchi zao au mataifa yanayotambulika na umoja wa mataifa yanarusiwa kuwa mwanachama wa IPU.

View attachment 2794625View attachment 2794748
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, akiwasili katika Ukumbi wa Bunge la Angola leo tarehe 27 Oktoba, 2023 wakati wa Mkutano wa 147 unaoendelea Jijini Luanda, Angola.
View attachment 2794749
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.
View attachment 2794755
Ni Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Tanzania ambaye ni Mgombea wa IPU akiomba kura.

Hicho cheo ni sawa na mtu kuwa class monitor au dada mkuu. Hakina tija yoyote Dunia hii. Labda kwake ni sifa, maana ndio cheo pekee anaweza kushinda bila wizi wa kura.
 
Acha unafiki wako .si mlikuwa mnasema hawezi kushinda? Naona aibu imewashika baada ya kuona amepita kwa kishindo huku shangwe ikitawala ukumbi mzima.
 
Kwa taarifa yako Wala sikufuatilia maana najua sio cheo serious. Huyo hawezi kushinda cheo chochote serious bila wizi. Nyie malimbukeni wa vyeo ndio mnaona ni bonge ya cheo. Kwangu naona ni kama kumsifia mtoto wako kuibuka mshindi wa kuwa class monitor.
 
SPIKA TULIA, RAIS MPYA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI (IPU)

Spika wetu Dkt Tulia Ackson ameshinda kwa KISHINDO nafasi ya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa Kura 172, Malawi 61, Senegal 59 na Somalia 11.

Hili ni goli letu tukufu Watanzania kisiasa, Kidiplomasia na kimahusiano duniani.

Kongole nyingi kwa wabunge wetu akina Neema Lugangira waliompambania usiku na mchana kuwashawishi wajumbe wampigie kura za ndio huko Angola.

Kwa wale mliopambana mitandaoni ama kwa kutuma jumbe hasi IPU Spika wetu asishinde, aibu iwatawale na mjifunze roho mbaya haijengi, na kizuri daima hujiuza.

Haya ni matunda ya Rais wetu Dkt Samia kuifungua nchi duniani.

Mungu ibariki Tanzania.

Suphian Juma Nkuwi.

View: https://twitter.com/SuphianJuma/status/1717890796202951079?t=JkJy56is_2KpA5kVftUl9Q&s=19View attachment 2794779

Yana mwisho
 
Congratulations RAIS WA DUNIA tulia AKSON katimize wajibu ila sikiliza sera za nchi wanachama wa Africa 🌍
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 27, jijini Luanda nchini Angola.

Dkt. Ackson amechaguliwa kwa kupata kura 172 kati ya kura 303 zilizopigwa na anarithi mikoba ya rais aliyemaliza muda wake, Duarte Pacheco kutoka Ureno aliyekuwa rais wa IPU kwa mihula mitatu.
#EastAfricaTv
 
Mapokezi Makubwa yanamngoja JNIA, Lumumba, Dodoma na Mbeya. CCM hatuna shughuli ndogo.

Signed by;
Mwenezi.
 
Na hii ndio ilikuwa ahadi kuu ya DPworld kwake

Mtaongea sanaa maana aibu zimewashika mnashindwa muweke wapi masura yenu hayo yaliyojaa ushetani mtupu.maana mlikuwa mnakesha mkiomba ashindwe lakini Mungu amewakatalia na kuendelea kuwa upande wa Dr Tulia. Mtakufa kwa msongo wa mawazo au kupata uwendawazimu.
 
Niyuleeee aloruhusu wabunge wasio Halali KUINGIA bungeni? Yule alolipasua BUNGE enzi za vyama vingi bungeni? Alokuwa kiongozi wa bunge pindi mbunge kapigwa risasi na kunyimwa haki zake zote? Walipitisha Sheria zahovyo na baadae kujiuliza kama walisinziaa? Alipandishwa kibabe na mwendazake?
Ok Dunia hii hata "WAchOVU" (remove small letters) pia hushinda.
 
Mtaongea sanaa maana aibu zimewashika mnashindwa muweke wapi masura yenu hayo yaliyojaa ushetani mtupu.maana mlikuwa mnakesha mkiomba ashindwe lakini Mungu amewakatalia na kuendelea kuwa upande wa Dr Tulia. Mtakufa kwa msongo wa mawazo au kupata uwendawazimu.
Kwa wasojua Siasa za ki-ambaruti ndohiz sasa!!
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa umoja wa mabunge duniani(IPU) leo Octoba 27, 2023. Kura 303 zilipigwa huku mshindi akihitaji angalau nusu ya kura hizo(kura 152)

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Ms. Adji Diarra Mergane Kanouté(Senegal) kura 52
Ms. Catherine Gotani Hara(Malawi) kura 61
Ms. Marwa Abdibashir Hagi(Somalia) kura 11
Ms. Tulia Ackson(United Republic of Tanzania) kura 172

Dkt. Tulia Ackson anachukua nafasi Duarte Pacheco kutoka Portugal aliyechaguliwa mwaka 2020 baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kupitia mtandao kutokana na janga la COVID-19 lililokuwa linaikabili dunia.

Kwa miaka 25 sasa urais wa IPU umetawaliwa na wabunge kutoka Misri, Hispania, India, Italia, Namibia, Morocco, Bangaladesh, Mexico na Portugal.

Dr. Tulia Ackson anakuwa Rais wa 31 wa IPU na amechaguliwa kwenye bunge la 147 la IPU lililofanyika mjini Luanda, Angola kutoka Oktoba 23 mpaka Oktoba 27.

Rais wa IPU ni kiongozi wa kisiasa wa taasisi hiyo, anaongoza vikao vyote vya taasisi hiyo na anaiwakilisha kwenye matukio ya kimataifa. Rais wa IPU anaongoza muhula wa miaka mitatu. Rais lazima awe mbunge kipindi chake chote cha miaka mitatu ya Urais.

IPU ilianzishwa mwaka 1889 kama kundi dogo la mabunge na kukua kwa kasi kama taasisi ya kimataifa ikijishughulisha na kukuza demokrasia, usawa, haki za kibinadamu, maendeleo na amani.

IPU ina wanachama 180 kati ya nchi 193 zilizopo duniani. Mabunge yote yaliyoanzishwa kisheria na nchi zao au mataifa yanayotambulika na umoja wa mataifa yanarusiwa kuwa mwanachama wa IPU.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, akiwasili katika Ukumbi wa Bunge la Angola leo tarehe 27 Oktoba, 2023 wakati wa Mkutano wa 147 unaoendelea Jijini Luanda, Angola.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.
Ni Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Tanzania ambaye ni Mgombea wa IPU akiomba kura.
Ok
 
Back
Top Bottom