Dkt. Tulia Ackson ateuliwa na CCM kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Dkt. Tulia Ackson ateuliwa na CCM kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

roho zinawaumaaaaaa

Kwa Sasa CHADEMA haipo bungeni ndio tuone ujinga wake. Maana wanapataga umaarufu kwa kuinyonga
Hili lilitarajiwa na nimekuwa nikiandika hapa...

Mosi, hakuna aliyekuwa anamzidi Tulia kwa uzoefu...

Pili, imekuwa kama ni utaratibu wa CCM kumrithisha naibu wa Spika nafasi ya Uspika inapokuwa wazi..

Tatu, imekuwa ni nafasi pekee ya kuweza kuwa na wanamama wawili katika mihimili ya JMT

Hamna kitu wameweka kibaraka was ikulu ili bunge liendelee kuwa dhaifu. Very stupid indeed.
 
Hongera Dr.

I saw this coming.

Rais Mwanamke.

Spika Mwanamke.

Waziri wa Ulinzi Mwanamke.
Tupate na jaji mkuu mwanamke tujue tumrwakabidhi nchi wanawake moja kwa moja

USSR
 
Pascal Mayalla komaaa na huyuhuyu akupigie debe kwenye teuzi zijazo. Ulimtabiria na kumpiga debe sana humu tangu zamani.

It's now or Never!
Ni utaratibu wa CCM siku zote Naibu spika ndiyo huwa anakuwa Spika! Hakuna jipya! Kama kuna mtabiri wa kweli humu tupeni jina la atakae kuwa Naibu spika,na hapo ndiyo pagumu!!
 

Akiongea na wanahabari, msemaji wa chama cha mapinduzi Shaka Hamdu shaka amesema chama cha mapinduzi kimeptisha Tulia Acksoni kuwa mgombea wa kiti cha uspika wa jamhuri ya muungano wa Tanzani

Pamoja na mambo mengine pia kama kuu imempongeza Rais Samia kwa ujenzi wa vyumba vya MADARASA nchi nzima

Pia soma: Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


PERSONAL DETAILS
Surnname:
Mwansasu
Middle Name: Ackson
First Name: Tulia
Salutation: Hon. Dr
Marital Status: Married
Date of Birth: 23 Dec. 1976
Place of Birth: Tukuyu Mbeya.
Sex: F
Email: tuliaj@gmail.com
Postal Address: 35093 Dar es Salaam


EDUCATION BACKGROUND
1984 - 1990 Mabonde Primary School Primary Education
1991 - 1994 Lolera Secondary School CSE
1995 - 1997 Zanaki Secondary School ACSE
1998 - 2001 University of Dar es Salaam LLB
2001 - 2003 University of Dar es Salaam LLM
2005 - 2007 University of Cape Town Ph. D

EMPLOYMENT EXPERIENCE
2011 - 2015 University of Dar es Salaam Senior Lecturer
2009 - 2015 University of Dar es Salaam Associate Dean
2001 - 2001 Attorney General's Office Trainee

HOBBIES
Reading Books
Physical Exercises


Katika Kijiji cha Bulyaga, Kata ya Tukuyu, wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwenye familia ya Akson Mwansasu, alizaliwa binti kitinda mimba.

Ilikuwa ni kiu ya mama ambaye licha ya kuwa na watoto wengine 10, alitaka kutulia kwa kupata mtoto wa kike na ndipo alipozaliwa binti huyo katika uzazi wa 11 na kupewa jina la Tulia.

Mama akatulia baada ya Mungu kumtuliza kwa binti Tulia ambaye pia alitulia tangu alipoanza kuisaka elimu na kuonesha mwanamke anaweza, akianza safari yake katika Shule ya Msingi Mabonde, Tukuyu, Rungwe mkoani Mbeya.

Matokeo ya darasani yalifanya Wizara ya Elimu impangie kuendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Wasichana ya Loleza iliyoko jijini Mbeya, barabara ya kwenda Mtaa wa Ghana alikohitimu kidato cha nne.

Akapasua tena na kujiunga na Shule ya Wasichana ya Zanaki ambako alimalizia masomo yake ya kidato cha sita mwaka 1997. Kwa hiyo, utaona kwamba elimu yake ya sekondari alisoma katika shule za Serikali za wasichana na kufanya vema.

Mwaka 1998 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitivo cha sheria na kufanikiwa kuhitimu chuoni hapo. Alitunukiwa shahada ya sheria mwaka 2001.

Mwaka huohuo wa 2001, Chuo hicho Kikuu cha Dar es Salaam kilimtaka kubaki chuoni hapo kwa ajili ya kufundisha sheria, hivyo alifundisha huku akiendelea kusaka shahada ya uzamili.

Akiwa bado anafundisha chuoni hapo, mwaka 2003 alimaliza masomo kabla ya kufanya mtihani wa uwakili wa kujitegemea mwaka 2004. Mwaka 2005 alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini kufanya shahada ya uzamivu na kufanikiwa baada ya miaka miwili. Tulia alitulia na kwa sasa ni dakta wa sheria.

Mwaka 2008 alikwenda chuo cha Max Planck Institute for International and Social Law cha Munich, nchini Ujerumani alikokuwa akifanya ‘post doctoral research’.

Mwaka 2009 alirudi nchini katika ajira yake ya awali ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria, nafasi ambayo alikuwa nayo mpaka mwaka 2014.

Akiwa Makamu Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria alifanikiwa kushika nafasi hiyo kwa vipindi viwili tofauti, hii yote ni kutokana na taratibu zake kuwa ni mkataba wa miaka mitatu ingawa unaweza kuteuliwa tena baada ya kumalizika kwa mkataba wa awali.

Kutoka wajumbe wa elimu ya juu, Dk. Tulia alikuwa miongoni mwa wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete wa Awamu ya Nne katika Bunge la Katiba lililofanyika kwa awamu mbili.

Awamu ya kwanza lilifanyika kuanzia Februari 18, 2014 hadi Aprili 25, 2014. Kwa siku 21 za kwanza alikuwa miongoni mwa wajumbe waliotunga kanuni za Bunge hilo lililoongozwa na Mwenyekiti Samwel Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan.

Utungaji wa kanuni hizo ulikuwa ni wa ‘vuta nikuvute’ hasa kwa wanasheria waliokuwa wakioneshana umahiri wa kuchambua sheria mbalimbali hadi kufikia kupata kanuni ambazo upinzani hawakuzifurahia sana ingawa mambo yalisonga.

Mwaka huohuo wa 2014 aliteuliwa na Chuo Kikuu cha Bayreuth cha nchini Ujerumani ili kufanya utafiti kuhusu hifadhi za jamii, utafiti uliojulikana kama Awarded the Alexander Von Humboldt Research Fellowship.

Alipaswa kufanya utafiti huu kwa kipindi cha miaka mitatu tu, ambapo alianza Machi mwaka huu na kuwapo nchini Ujerumani hadi Agosti aliporudi kwa ajili ya likizo fupi.

Hata hivyo, utafiti huo aliufanya kwa kipindi cha miezi sita tu, kwani akiwa katika mapumziko, ndipo alipoteuliwa tena na Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9, mwaka huu.

Amekuwa naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miezi miwili tu kutokana na Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli, kutengua uteuzi huo na kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, akiwa ni mbunge wa kwanza kati ya nafasi 10 za wabunge aliopewa Rais kwa mujibu wa sheria.

Kati ya kazi nzito alizofanya akiwa Mwanasheria Mkuu ni kuongoza jopo la mawakili wa Serikali katika kesi maarufu kwa jina la mita 200, kwani kulitokea mvutano baina ya vyama vya upinzani na Serikali katika kutafsiri sheria ya umbali wa wananchi kukaa mara baada ya kupiga kura.

Mahakama Kuu ilitafsiri sheria hiyo kwa kuagiza wapigakura kukaa mbali kwa zaidi ya mita hizo baada ya kuridhishwa na hoja za upande wa Serikali ambako Dk. Tulia alikuwa kinara kwa kutaka korti iamue hivyo.

Alhamisi Novemba 19, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipiga kura ya kumchagua Tulia kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo. Uchaguzi huo ulifanyika mapema asubuhi ndani ya Ukumbi wa Bunge. Katika uchaguzi huo, Dk. Tulia (CCM) alipata kura 250 kati ya 351 za wabunge wote, huku mpinzani wake, Magdalena Sakaya (CUF) akipata kura 101.

Dk. Tulia ambaye ameolewa na James Andilile na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume
Mihimili miwili mikuu ya utawala sasa rasmi mikononi mwa akina mama kutoka kwa akina baba. Kutoka kwa JPM na JYN mpaka "era" ya sasa ya SSH na TAM. Akina mama ni zamu yao ya kuidihirishia Afrika ya kuwa wanakiaminika wanaweza.
 
Hivi kweli mkuu, kuna nani wewe unadhani anaweza kupingana na executive? nchi hii Tanzania. kwa uhalisia kabisa.
Binafsi, ningeshangaa sana kama wasingempitisha Dr. Tulia.

Kwa kauli yako hakuna haja ya kuwa na bunge, maana hakuna wakuiface executive.
 
Back
Top Bottom