Dkt. Tulia Ackson: Ilani inasema barabara ya Tanzam upembuzi yakinifu umekamilika Serikali inasema utafanyika mwakani. Tuiamini CCM au Wizara?

Thubutu aulize swali kama hili enzi za dhalimu!!! Hizi ni dalili tosha kwamba ndani ya maccm mama ana hali ngumu sana.

Hapana BAK, hizi ni dalili za kuwa sasa watu wamepata nafasi ya kuwa binadamu tena!! Mwendazake aliwafanya watu wawe nusu maiti; vichwa vilijaa pumba tu!! Mpaka Gwajima akawaaminisha Watu wajinga kuwa yeye angeweza kufufua maiti mithiri ya nabii Issa bin Mariam!!
 
Unadhani watu wasingekuwa waoga ndani ya Maccm na Serikali ya kumkabili kwa wingi bila woga kila alipokiuka katiba na taratibu za nchi angevimbisha kichwa na kufanya maovu mbali mbali aliyoyafanya Mkuu? Wapuuzi hao na walikuwa chanzo cha nchi yetu kupitia kipindi kigumu kuliko vyote tangu tupate uhuru. Watubu hadharani kwa kukaa kimya kuruhusu dhalimu aingamize nchi kwenye kila sekta na kuumiza Watanzania wengi sana.


 
Tulia siyo strategist. Alitegemea huruma za Mwendazake ndiyo amsaidie kuweka mafungu kama alivyomsaidia kupata ubunge wa Mbeya Mjini.

Strategist mzuri kwa nafasi yake kama NS angecheza na Budget officers wa Wizara ya ujenzi na fedha ili waiingize hiyo barabara kwenye mpango kazi wa 2020/21. Kipindi cha kufanya hayo ni miezi ya November- Jan 2021. Alidhani Mwendazake hatakufa, tunamsubiri 2025
 
Yaani Tulia hakuusoma mchezo!
 
ukiona hivyo taa ishawaka mbeya labda jimbo jingine litaftwe haraka au achague kujitoa kwenye list yawasomi wanaokalia mawazo yao chanya kisa chama
 
Afu nimeshangaa kwenye bajeti barabara kuu na za muhimu.kitaifa hazina pesa au zimepewa pesa kiduchu ila kibarabara uchwara cha kwenda Chato sijui nyamirembe port Chato ginery wametenga pesa nyingi

Huu ni upuuzi ,Kazi ya barabara kuu za kuunga mikoa na nchi bado afu huyu Waziri anafanya mambo ya kijinga.

Hicho kibarabara kinaweza kweli kulingana na barabara ya Mbeya Tabora)Singida? Au kama ile ambayo mbunge alitaka kupiga sarakasi?

Mh Rais ikiwezekana punguza pesa kwenye miradi ya reli peleka pesa kwenye barabara ndiko kwenye tija.
 
Ni kweli mkuu kila parameter ya uchumi huikosi Mbeya ila kwenye allocation ya funds haitendewi inavyostahiki,hizi sio akili ccm waelewe hili
 
Inajengwa kwa awamu wameishia Igawa sasa hv,wanatakiwa kwenda Mbeya then Tunduma border
Ile sio barabara ya kujengwa kwa awamu,ni moja ya barabara nyeti Sana kwa Nchi,unajenga kwa awamu kwani ni ya kwenda Chato kubeba punda?
 
Ile sio barabara ya kujengwa kwa awamu,ni moja ya barabara nyeti Sana kwa Nchi,unajenga kwa awamu kwani ni ya kwenda Chato kubeba punda?
Sasa si hela mwanawane ndio shida nadhani hapo.Unachosema upo sawa kabisa
 
Uko sahihi nikiwa na Drive kwenda kwetu Makete kupitia Mbeya(Uyole - Isyonje- Igoma- Kitulo) nikivuka Daraja la Igawa tu napunguza speed mpaka 60km/hr. Barabara ni chakavu sana
 
Mara ya mwisho umepita lini hio njia..?
 
Uko sahihi nikiwa na Drive kwenda kwetu Makete kupitia Mbeya(Uyole - Isyonje- Igoma- Kitulo) nikivuka Daraja la Igawa tu napunguza speed mpaka 60km/hr. Barabara ni chakavu sana
Ile barabara ilipuuzwa kwa makisudi na Mwendazake.
 
Mara ya mwisho umepita lini hio njia..?
Mwezi uliopita!
Igawa-Mbeya ni Mbovu sana,
Mbeya Tunduma ni Mbovu zaidi-pale, Iwambi-Mbalizi barabara ya kimataifa sasa ni one way , one lane!

Halafu tunasema serikali ipo, huku inajenga flyover baharini na Busisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…