Dkt. Tulia Ackson ndiyo tishio la Katiba Mpya, awe makini!

Dkt. Tulia Ackson ndiyo tishio la Katiba Mpya, awe makini!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Dkt. Tulia Ackson ambaye ni spika wetu ndiyo kwa sasa tishio kubwa sana kwa katiba mpya na mwenendo wa sheria na maendeleo kwa nchi yetu.

Huyu spika ambaye aliingizwa baada ya kutetea sana Uraisi wa kifalme kwenye vikao vya katiba kiasi kwamba akapewa ubunge na Rais wetu ambaye alitaka kugeuza nchi yetu kuwa ya ki dikteta kama Urusi.

Kwasasa amekuwa anatafuta wale wana CCM ambao wanajua hawataweza kushinda kihalali na yeye akiwa mojawapo. Amekuwa akionyesha makucha yake kwa kujaribu kutafuta wabunge bila mafanikio ambao nao ni kama yeye ambao wanatamaa ya madaraka lakini hawapedwi na sio wanasiasa wenye mvuto kwa wananchi.

Amekuwa anajiaminisha kama vile ana nguvu bila kujua kwamba nguvu yake ni ndogo kuliko anavyo fikiria. Lakini yeye na katibu wa zamani Bushiru pamoja na Covid-19 hawatatosha kubeba haya matakwa yake.

Akiendelee hivi atatolewa kwasababu Rais kasha fanya maamuzi ya kwamba yeye anataka kuwa historia kwa vizazi na sio tu kuwabeba wabunge. Rais kachukuwa uamuzi sahihi wa kuweka historia baada ya kuona Magufuli walivyo mbadilikia kwa muda mfupi. Huyu spika awe makini sana kama mmegundua hata waongeaji wa Chama wamekaa mbali na matamko yake.

Huyu ndiye wale madikteta uchwara ambaye inabidi achague upande mapema

Niongee Chadema wanamsubiri Lema kwa kazi moja kubwa. Lema anajulikana sana na uwezo mkubwa wa kupata itelegensia ya ndani ya CCM na kuanzia mwezi wa nne tutaanza kusikia madudu ya Tulia. File lake linamsubiri Lema arudi. Ndiyo maana Chadema wamenyamaza kwanza

Lazima tujue hii katiba mpya Rais Samia ndiye atapata sifa zote na sio Chadema. Hivyo kupigana na katiba nzuri na mpya Rais Samia hatakubali na uzuri Chadema wanajua hilo. Hivyo tutaanza kusikia katiba ya Mama Samia baada tu ya makubaliano ya vifungu muhimu. Hivyo kupinga katiba itakuwa kumpinga Mama
 
Tangu awm5 nilimwona ni kitisho kwa mengi na pia ni mwepesi kuusoma upepo na kwenda nao,akiamua kulingana na anapo amini katika maslahi,iwe kwa imani au kwa mrengo inaweza kuwa shida kwa upande mwingine,🤔
 
Akiendelee hivi atatolewa kwasababu Raisi kasha fanya maamuzi ya kwamba yeye anataka kuwa historia kwa vizazi na sio tu kuwabeba wabunge. Raisi kachukuwa uamuzi sahihi wa kuweka historia baada ya kuona Magufuli walivyo mbadilikia kwa muda mfupi. Huyu spika awe makini sana kama mmegundua hata waongeaji wa Chama wamekaa mbali na matamko yake.
Hili na mimi nimeliona. Hata hivyo msaliti wa Taifa akina Ali Safi wa Nkasi, akina yule aliyekuwa mtangazaji Tbc na wenzake waliotaka kusaliti wananchi Karma iliwamaliza.
 
UMEONGEA MAMBO MEENGI,LKN HUJASEMA LOLOTE,NI UPUUZI UJINGA NA LUJIISHA UPEPO,KATIBA KATIBA.MNATAKA KATIBA YA WATANZANIA AU KATIBA YA WANASIASA?,
 
Rais Samia akikubali tu mchakato wa Katiba mpya nitam support kwa udi na uvumba...Usikubali mama kudanganywa, weka historia yako ambayo hakuna atakayeweza kuifuta. Katiba mpya ni hitaji la kila anayejali future ya nchi yetu walafi wachache wasikupotoshe
Ameeni na Mungu wa Mbinguni amuwezeshe kuzidhinda nguvu za ibilisi
 
Back
Top Bottom