Sio kahongwa, nimeambiwa kumbe siri ya watu kuweka namba zao ni kukusanya maokoto.
Yaani unaandika makala ndefu ndefu za kusifia kisha wahusika wakisoma na nikuambie ukweli, hawa viongozi wa nchi hii ni washamba kweli kweli!
Hapo kijana ana pigiwa simu na namba asiyo ijua na kuambiwa unafanya kazi nzuri ya kizalendo "keep it up" chukua kidogo hicho kwa ajili ya bando na endelea na uzalendo wako!
Ghafla simu inapokea laki tatu hadi tano kwa hawa kina
Lucas mwashambwa ambao ni wakongwe na ndivyo wanavyo ishi.
Watu mnawaona wajinga na kuwakebehi lakini wao wameamua potelea mbali mradi kuna maokoto. Ni kama ambavyo mnaweza kuwasema sana makahaba lakini hawaachi na hakuna aibu sababu ya kipato.