Dkt.Tulia, Dkt. Mwigulu, Dkt. Nchimbi, Paul Makonda na January Makamba ni hazina kwa Tanzania ijayo

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Haiba, hulka, maono, mipango, mitazamo na utendaji wao una viashiria, sifa, vigezo na uelekeo wa nafasi za juu katika uongozi wa nchi. Hii ni kwa mujibu wa haki, maoni na mtazamo wangu huru kikatiba..

Nachelea kuwasihi wananchi na waTanzania wote kwa ujumla, kutafakari jambo hili muhimu sana kwa mustakabali wa ustawi wa Taifa letu, baada ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, kipenzi cha waTanzania kukamilisha ngwe yake ya pili uongozini 2025-2030...

Nje ya watajwa hao, ni kupoteza muda, nguvu na rasilimali tu πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kwa nini hujifunzi kuandika kwa kanuni zake?JF ni jukwaa kuuubwaaa juu ya jukwaa.Unataka utafsirikaje?Usiandike tu kama upo chumbani "unachana" nywele.Badilika.Siyo ombi.
 
Nyie ndio mna sababisha jf kuonekana sio kwa sasa
 
Kwenye Heading malizia kabisa na Dr Makonda itapendeza zaidi
 
Mwigulu toa.
Makonda toa.
Makamba toa.
Huwezi kuwa sirias mleta mada.
 
Mheshimiwa, uko wapi.....
 
Unamaanishaa nini,akili mbumbumbu umeniacha aliyeelewa anisaidie.
 
mafisadi wakubwa na Matapeli wataifa hao
 
Hapo mwanasiasa hazina ni Dr Tulia peke yake, hao wengine ni machawa na wapenda sifa tu.
 
Toa makonda katika list yako. Yule hamna kitu zaidi ya kick na mbwembwe tu. Hakuna anachoanzisha akakimaliza huwa kinaishia njiani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…