Nasema hivi, ukipanic lazima utaongea vitu vya ajabu, kwenye post yako umemtaja Marando, yeye ni nani ili nijue kama hujapanic? Isitoshe ulichoandika hakina mtiririko mzuri, na umechanganywa mambo mengi kwa pamoja, mpaka nimeshindwa kuelewa hoja yako ni nini hasa.
Hoja yangu ni kwamba Mpaka sasa Upinzani umefanikiwa katika kuwashibisha baadhi ya viongozi wa wake tu.
Na sio kuyafikia malengo ya upinzani ya
1.Kuwa na Wabunge wengi wa kuchaguliwa
2. Kuchukua Dola.
Hayo ndiyo malengo ya Upinzani.
Siasa za Upinzani za Tanzania zimejaa Ubabaishaji tu kwa viongozi wake kutaka kujilimbikizia mali na kung'ang'ania Madalaka.
Ndio maana Nchi jirani kama Kenya, Malawi, Zambia, Congo, nk Zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa ktk Siasa za Upinzani.
Upinzani wa Viongozi kama Mbowe Marando na Mrema, ni wa kutaka kuitwa Ikulu na Kunywa Chai tu.
Na kusubiri teuzi toka CCM
Kesho utasikia wamehamia CCM.
Ndio maana Watanzania wengi hawapigi kura za Uraisi.
Kwakuwa
Wameichoka CCM na pia
Hawamwoni Mpinzani wa kumkabidhi Hazina Yao.
Wanabaki kujiandikisha na kuchukua Vitambulisho tu vya kusajiria laini za Simu.