Dkt. Tulia: Kama wasingeenda Mahakamani ningetangaza nafasi kuwa wazi

Mkuu Fundi Mchundo , vitu vingine sio vya kuuliza ni kutaka tuu kumuonea Spika. Uchaguzi unasimamiwa
Anaonewa kivipi? Hii ina tofauti gani na suala la vyeti vya kughushi serikalini? Serikali si ndio iliyochukua hatua baada ya kutambua kuwa imedanganywa? Kwa nini haikusema haihusiki na kuachia bodi ya mtihani ndio iwachukulie hatua wakati wakiendelea kufanya kazi? At the very least Spika alipaswa kushirikiana na Chadema kujua ukweli ili kama kuna nyaraka zilighushiwa, wahusika wachukuliwe hatua za kisheria ili wengine wasithubutu kufanya hivyo tena.

Atachukuaje hatua ya kuwanyang'anya ubunge kwa sababu Chadema wamewafukuza kwa kosa la kujipeleka bungeni bila ridhaa yao bila kutaka kujua ofisi yake iliwapokeaje? Mpira uko squarely kwa Spika na sio mtu mwingine. Spika alitakiwa achukue hatua kulinda heshima ya institution ya Bunge ambayo watu wachache wanataka kuiharibu. Suala la uhalali wa utaratibu waliofuata Chadema kuwafukuza wakina Halima kweli halimhusu. Lakini la utaratibu wa kuwapokea bungeni ni la Spika na si mwengine. Spika anapaswa kujiuzuru kama alipokea nyaraka alizojua ni za kughushi na kuzitumia kuwaapisha wakina Halima maana inaonyesha hana integrity anayopaswa kuwa nayo. TAKUKURU nao walitakiwa kujiingiza mapema kabisa.

Lakini sishangai. Boniface Jacob alinyang'anywa umeya kwa barua kutoka "Chadema" iliyomvua uanachama hata baada ya Chadema kusema kuwa haijawahi kuandika barua kama hiyo! Kulikuwa na majaribio ya kuwapa fomu wagombea kutoka "Chadema" ambao Chadema ilisema kuwa hakikuwachagua. Hili nalo ni muendelezo wa mambo kama haya. Halafu mnakazania kuwatetea watu ambao ni dhahiri hawakuingia kihalali bungeni. Kushindwa kwa Spika kuweka wazi nyaraka zilizowasilishwa kuwatambulisha kwake ni ushahidi tosha.

Amandla...

Nguruvi3 JokaKuu
 
Ila kunataratibu kwenye vyama zinabidi zifuatwe ili kupokea wabunge wa viti maalumu je zikifuatwa. Siyo mtu yoyote anajipeleka tu bungeni .
 
Ila kunataratibu kwenye vyama zinabidi zifuatwe ili kupokea wabunge wa viti maalumu je zikifuatwa. Siyo mtu yoyote anajipeleka tu bungeni .

Kwani wao ni wajinga mpaka wajipeleke Tu? Mbona hawakujipeleka after tume Tu kutangaza
 
Speaker kama gari lililotangulia kituoni katoa hukumu kabla hukumu haijatoka ndio ujuwe nchi hii hakuna mahakama wala haki. Angewafukuza asubuhi na kuwarudisha mchana baana ya hukumu kidogo angeonekana malaika ila kawahi kusoma script.
 

Tatizo watu wa mitandaoni ujuaji ni mwingi
 

Hayo ni mambo ya kawaida Kwa siasa za Africa hakuna jipya hapo
 
Mkuu Fundi, kama kungekuwa na ithbati ya Chadema kuandika barua Msajili wa vyama kwa chuki aliyo nayo dhidi ya Chadema asingekaa kimya.
Tume ya uchaguzi (NEC) kwa utendaji wake wa maagizo ya chama tawala wasingekaa kimya

Tuhuma za forgery ni mbaya sana kuliko tuhuma alizoitiwa Pascal Mayalla au CAG Assad, Bunge

Lakini, NEC, Bunge wote kimyaa kana kwamba wamekubali tuhuma za forgery
Kwamba institution hizo hazioni kashfa ya kughushi nyaraka? Real?

Sasa Bunge lina kashfa nyingine, Spika kawaruhusu COVID19 kwa hisia zake asubuhi ya jana
Hukumu ya mahakama imetoka jioni, Spika alitoaje kauli ya suala la mahakamani kabla?
 
Speaker kama gari lililotangulia kituoni katoa hukumu kabla hukumu haijatoka ndio ujuwe nchi hii hakuna mahakama wala haki. Angewafukuza asubuhi na kuwarudisha mchana baana ya hukumu kidogo angeonekana malaika ila kawahi kusoma script.
Jaji Mgeta aliomba muda wa kupitia shauri mchana na kutoa tamko jioni , wakati huo huo Spika wa Bunge Tulia Akson alishajua shauri limeamuliwaje asubhi ya siku hiyo

Kuna vilevi duniani lakini ulevi wa madaraka ni ulevi mbaya sana.
Anayefanya haya tunaambiwa ni mcha mungu sana kwa imani ana PhD na ni Mwalimu wa sheria wa chuo kikuu UDSM, na alishakuwa naibu mwanasheria mkuu wa nchi ya Tanzania, sasa anasimamia mhimili wa kutunga sheria zinazohusu watu milioni 55.
 
Yes coz chama kilivunja sheria ya kutotiii kupeleka wabunge wa viti maalum, Kwa sababu zao binafsi

Acha uongo, chama kisipopeleka wabunge kinapoteza hiyo haki. Hakuna Cha kuvunja sheria. Ndio maana serikali iliamua kuingia na kuwasupport kina Halima maana ilijua chadema haitwapeleka Bungeni.
 
Ni huzuni kwa kweli kwa Taifa na nasema hili kwa uchungu nikiona tunashindwa kuheshimu sheria zetu wenyewe na wanaovunja ndio viongozi wakubwa waliopewa dhamana. Mimi niseme wasi sina maslahi yoyote katika hili siko CCM wala Chadema na sijawahi kupiga kura maisha yangu yote ila inauma ukiona sheria zinavunjwa kwa makusudi kwa kiburi tu kama sheria hizi mbaya wana uwezo wa kuzibadilisha hata kama mabadiliko mabaya lakini tutaheshimu ni sheria lakini sio kuona watu wote wajinga hili ndio linaumiza kuliko yote.
 
Wanatii sheria ya viti maalum bila ridhaa ya chama?
Chama hakijawapeleka huko viti maalum kisha wao wanatii sheria ya viti maalum!
Very strange!

Nchi imepitia mengi!

Nasikitika Kwa sababu credibility yao machoni pa jamii imeharibika!
Watetea matumbo!
 
Hili somo la history kuwa binadamu alianza kama sokwe linawezekana kukawa kuna kiukweli fulani........
 
Tulia ukilala unasali kwa roho na kweli? Hujajifunza tu ya Job? Cheo ni dhamana na WAKATI SI MILELE!
Yuko wapi Job leo hii
Yuko wapi Sabaya
Yuko wapi Bashite....
Yako wapi mafirauni yote yaliyotamba kwa nyakati zao?
Wote hao, sasa hivi wanaweza kuwa ku
Wa napelekewa moto huku wakiwa wameufiata...Mavi ya kale....hayanuki!!
 
Kama uchaguzi ulikuwa batili. Mwenyekiti anaendaje kuonana na Rais batili, mnaandika barua kwa bunge batili, kwa muktadha huu itakuwa na nyie ni batili

Mwenyekiti kaenda kuonana na rais ili kuweka mazingira vizuri baada ya rais aliyeendesha uovu na uharibifu wa uchaguzi kuelekea motoni. Chama kimeandika barua kwa bunge la majizi ya kura kuwa wabunge wa Covid sio wanachama wake tena.
 
Mkuu hii inasikitisha mno. Nawashangaa watu wanaoona tatizo kubwa ni utaratibu uliotumiwa na Chadema kuwafukuza wakina Halima wakati mtu hata kuinsinuate kuwa institution kama Bunge ni corrupt ni jambo la hatari mno. Nilitegemea Bunge lipigane kufa na kupona kujisafisha kwenye hizi tuhuma.

Dokta amejiharibia kwenye hilo. Ndio ubaya wa kuchagua upande wakati mtu unapaswa kuwa neutral and beyond reproach. Namkumbuka Spika wa House of Commons John Bercow alivyokuwa ana hakikisha kuwa serikali haiburuzi upinzani ingawa mwenyewe alikuwa Conservative.

Amandla....
 
Hii nchi imejaa wapumbavu wengi z sana!
Ulitaka raisi akae hotel ya uswahilini huko new York?

Halafu nyie washamba mnateseka sana for nothing. Hapa Tanzania tu kuna hotel zina bei kubwa kuliko hiyo. Kuna ubaya gani?
Chawa kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…