Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Anaonewa kivipi? Hii ina tofauti gani na suala la vyeti vya kughushi serikalini? Serikali si ndio iliyochukua hatua baada ya kutambua kuwa imedanganywa? Kwa nini haikusema haihusiki na kuachia bodi ya mtihani ndio iwachukulie hatua wakati wakiendelea kufanya kazi? At the very least Spika alipaswa kushirikiana na Chadema kujua ukweli ili kama kuna nyaraka zilighushiwa, wahusika wachukuliwe hatua za kisheria ili wengine wasithubutu kufanya hivyo tena.Mkuu Fundi Mchundo , vitu vingine sio vya kuuliza ni kutaka tuu kumuonea Spika. Uchaguzi unasimamiwa
Atachukuaje hatua ya kuwanyang'anya ubunge kwa sababu Chadema wamewafukuza kwa kosa la kujipeleka bungeni bila ridhaa yao bila kutaka kujua ofisi yake iliwapokeaje? Mpira uko squarely kwa Spika na sio mtu mwingine. Spika alitakiwa achukue hatua kulinda heshima ya institution ya Bunge ambayo watu wachache wanataka kuiharibu. Suala la uhalali wa utaratibu waliofuata Chadema kuwafukuza wakina Halima kweli halimhusu. Lakini la utaratibu wa kuwapokea bungeni ni la Spika na si mwengine. Spika anapaswa kujiuzuru kama alipokea nyaraka alizojua ni za kughushi na kuzitumia kuwaapisha wakina Halima maana inaonyesha hana integrity anayopaswa kuwa nayo. TAKUKURU nao walitakiwa kujiingiza mapema kabisa.
Lakini sishangai. Boniface Jacob alinyang'anywa umeya kwa barua kutoka "Chadema" iliyomvua uanachama hata baada ya Chadema kusema kuwa haijawahi kuandika barua kama hiyo! Kulikuwa na majaribio ya kuwapa fomu wagombea kutoka "Chadema" ambao Chadema ilisema kuwa hakikuwachagua. Hili nalo ni muendelezo wa mambo kama haya. Halafu mnakazania kuwatetea watu ambao ni dhahiri hawakuingia kihalali bungeni. Kushindwa kwa Spika kuweka wazi nyaraka zilizowasilishwa kuwatambulisha kwake ni ushahidi tosha.
Amandla...
Nguruvi3 JokaKuu