Dkt. Tulia: Kama wasingeenda Mahakamani ningetangaza nafasi kuwa wazi

Una uhakika si wewe tu
 

Acha uongo, chama kisipopeleka wabunge kinapoteza hiyo haki. Hakuna Cha kuvunja sheria. Ndio maana serikali iliamua kuingia na kuwasupport kina Halima maana ilijua chadema haitwapeleka Bungeni.

Sasa makelele ya nn?
 
ishu sio kama chadema waligoma , ila nani aliwapeleka??nani alisaini barua zao??serikali inaenda kuwa uchi maana lzm waileze mahakama barua ilitoka wapi??
 
Tulia ukilala unasali kwa roho na kweli? Hujajifunza tu ya Job? Cheo ni dhamana na WAKATI SI MILELE!
Yuko wapi Job leo hii
Yuko wapi Sabaya
Yuko wapi Bashite....
Yako wapi mafirauni yote yaliyotamba kwa nyakati zao?
job analipwa na kulindwa mpaka kifo.
sabaya anatoka jela na mahela bado anayo.
bashite bado yuko mtaani na ana hela

endeleeni kukomaa na katiba mpya ili watu kama hawa wasiwe na bahati baada ya kumaliza dhamana zao za uongozi.
 
kuna watu hili swala linawauma kuliko hata ugumu wa maisha yao.halafu ni wanaume sasa.

hii nchi mambo mengi tu yanakwenda kihuni huni,ije kuwa wabunge wa 19 waliokuwanwa chadema!!!si tuliwaambia nyinyi hao wako kazini mkawa mnakaza mavisogo,haaya sasa si ndugai,tulia,samia au mahakama ambayo inaeleweka kwenye swala lao.

pambaneni.
 
Kuna utaratibu wa kuwapata hao wabunge wa viti maalum unaofanyika katika chama husika. Je walifuata utaratibu wa chama chao kupata hizo nafasi? Mambo hayaendi kiholela kama unavyofikiri.
 
Hakuna sheria Ruzuku ya UN na EU sijui hawapati mpaka ikidi ya upinzani itimie .Mama kumwita Mbowe kwa meridhiano sio mchezo na kumwomba akubali kuchukua ruzuku mikataba baba inawatoa kwenye mstari
 
Sasa nyie wenye uwezo mrefu WA akili si mnaona mlivyotupwa nje
Ufupi wa akili yako ni kwamba, unafikiria leo tu! Hujui kwamba mwisho wa ubaya ni aibu! Kwamba hatimaye haki itashinda, hawa watakosa uanachama, hata wakiendelea na ubunge kwa hii miaka michache, wataishia kuwa kama Lijuhalikali!
Hujui kwamba ccm na Tulia wanaweka reference ya kutozingatia haki consistently na chadema wanaweka reference ya kupambana na ufisadi! Pia hujui kwamba chadema haitafuti kuwashinda kina Mdee Leo tu, bali kupata ushindi mkubwa Juu ya mfumo kandamizi wa ccm siyo Leo tu, Hata huko mbeleni!
Akili yako Ni fupi kwa sababu unajua sprint tu, hujui marathon! Pia kwamba chadema ilipaswa kutii wapeleke wabunge wa viti maalumu, Ni upumbavu, Lakini hatupaswi kukulaumu wewe, elimu yetu na ccm wanapaswa kubeba zigo la lawama kwa kuzalisha akili chakavu Kama hizi!
 

Uanachama sio ishu ww, si Bora ale ubunge wake amalize akafanye mambo yake ? Kwani Jambo la kufanya ni siasa Tu?
 
Hakuna sheria Ruzuku ya UN na EU sijui hawapati mpaka ikidi ya upinzani itimie .Mama kumwita Mbowe kwa meridhiano sio mchezo na kumwomba akubali kuchukua ruzuku mikataba baba inawatoa kwenye mstari

Kamwita na lipumba nae kamwita kwasababu hiyo?
 
Sina muda wa siasa za kusujudia mtu, bali nataka siasa za haki na uwajibikaji fullstop.
Unadhalilisha nafsi yako kwa kuongea na huyo sukumagang mjinga, anayejitia moyo kupitia frustration zako Tindo! Una msimamo dhabiti lakini huna subra!
 
Uanachama sio ishu ww, si Bora ale ubunge wake amalize akafanye mambo yake ? Kwani Jambo la kufanya ni siasa Tu?
Hiyo ni sawa kulingana na ufupi wa akili yako, huwezi kuwaza nje ya box hilo!
 
Anaonewa kivipi?
Bunge linaletewa wabunge na NEC. Sio kazi ya Bunge kujua mbunge yoyote amepatikanaje
 
Bunge linaletewa wabunge na NEC. Sio kazi ya Bunge kujua mbunge yoyote amepatikanaje
Not true. Kazi kubwa ya Spika ni kuhakikisha kuwa wabunge ambao wako ndani ya Bunge ni legitimate. Kazi yake ni kulinda integrity ya Mhimili huu kwa wivu mkubwa. Kama kuna tuhumq kuwa kuna mbunge ameingia humo kwa njia ambayo si halali ni wajibu wake kutafuta ukweli wa tuhuma hizo ili kama ikithibitika kuwa tuhuma hizo ni kweli, amchukulie hatua huyo criminal na kama si kweli amchukulie hatua aliyetaka kuchafua taswira ya Bunge ambalo tunaliita Tukufu.

NEC inapeleka orodha ya majina ya watu waliopendekezwa na vyama vyao kuwa wabunge wa viti maalum pamoja na ushahidi kuwa kweli hivyo vyama viliwapendekeza. Sasa kama hizi nyaraka ziliwasilishwa kwa Spika na sasa kuna tuhuma kuwa zilighushiwa kwa nini Spika hataki kui task NEC ithibitishe uhalisia wa tuhuma hizo? Kukaa kwake kimya ndio kunatufanya wengine kuwa alikuwa complicit in the whole charade. Na ndio maana kuna uwezekano kuwa hamna cha barua wala nini kutoka NEC ikimtaarifu Spika kuhusu uamuzi wa Chadema. Spika kwa ukimya wake ndio anazidi kuchafua sura ya Bunge. Utamlaumuje Chadema kwenye hili?

Amandla...

Nguruvi3 JokaKuu
 
Hivi Paskali, utasemaje kuwa Spika hawajibiki kujua uhalali wa mbunge ambae Chama chake kinasema kuwa hakijawahi kumpendekeza?
Hivi mtu akiuuzia gari, akakupa makaratasi yote yanayohitajika kuwa alilinunua kutoka kwa fulani lakini akatokeza mtu akasema kuwa hilo gari ni lake lakini hajawahi kumuuzia aliyekuuzia. Utasema kamuulize aliyeniuzia na utakataa kumuonyesha makaratasi ambayo yule tapeli alikupa? Mbaya zaidi, utakataa kabisa kuwasiliana na yule tapeli kujua ukweli huku ukisisitiza kuwa gari ni lako? Tutaachaje kuamini kuwa ulikuwa ni mchongo kati yako na yule tapeli ili mumdhulumu jamaa gari lake?

Amandla...
Pascal Mayalla Nguruvi3 JokaKuu
 

Hivi vitu unavyompa Paskali vyote ni vyenye ncha kali, usidhani hajui ukweli huu unaompa, ila nongwa yake dhidi ya CDM haibebi huu ukweli wako.
 
Hivi kuna Binadamu anayeweza kukataa kupewa Ubunge ale maisha kwa miaka mitano ?
Yuko wapi Nasari ?
Wilbord Slaa ?
Kafulila ?
Hadi marehemu Maalim Seif ilikuwa kila akishindwa uchaguzi anaingia na kukubali uteuzi za CCM.

Nani aliwahi kupewa cheo na CCM akagoma ?

Akina mdee walikosa kazi za kueleweka baada ya kuanguka Ubunge.
Wanateuliwa na Ndugai mnataka wagome mnataka wakale wapi, mgechukua majukumu ya kuhudumia familia zao.

Siasa za Tanzania ni za kutafuta chakula tu. Wala hakuna upinzani wa kikweli kweli.
La Upinzani ungekuwa kwakweli CCM ingusha ondoka madalakani siku nyingi sana.

Wako wapi akina Marando, Lamwai, Mbatia, Lyatonga nk. Wazee wa Mageuzi ?
Wote wanasubiri teuzi toka CCM.

Waacheni akina Halima Mdee wale chakula.
Muda wa teuzi ukiisha watarudi Chadema.

Ndivyo Siasa zetu zinavyo enda.
 
Unadhalilisha nafsi yako kwa kuongea na huyo sukumagang mjinga, anayejitia moyo kupitia frustration zako Tindo! Una msimamo dhabiti lakini huna subra!

Mkuu nashukuru kwa kunifunga speed govenor naheshimu hisia zako, lakini hata ningefanya subira kama unavyoshauri, bado siwezi kubadilisha nilichosema.
 

Uko sahihi, kama unafanya siasa za tumbo ungeenda ccm kabisa, maana huko tumbo ndio mbele. Ww inaonekana ni mzee ndio maana huamini katika mabadiliko, hivyo haya yanayoendelea kwako unaona ni sawa na hutaki yabadilike maana umefikia mwisho kutaka mabadiliko kutokana na umri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…