Dkt. Tulia: Kama wasingeenda Mahakamani ningetangaza nafasi kuwa wazi

Ni kwa sababu wale wa CUF hawakwenda mahakamani sa hawa wakwenu wameenda huko, waache wapewe haki ya kusikilizwa maana mlidai bila kumsikiliza mtu ni udikteta. 😁
 
Lipumba hajaitwa kaomba kwenda kuonana na Mother.Na watasema walichoongea naye kwa ufasaa

Umeanza lini kufanya kazi ikulu?
Mama anakutana na wanasiasa wote,

Shida yenu chadema ni kujiona wakubwa sana
 
Hiyo ni sawa kulingana na ufupi wa akili yako, huwezi kuwaza nje ya box hilo!

Hata Baba yako angewaza hivi hivi kama mm, ww tangu umekuwa mwanachama Una kipi cha kusema umefaidika na uanachama wako?
 
Ni kweli ni jambo la kisheria..lakini ni pale tu chama kinapotambua uhalali wa uchaguzi unaopelekea wao kupata hivyo viti maalum, Chadema hadi leo hawautambui uchanguzi wa 2020, kwa hivyo wangetimiza takwa hili la sheria wasingekuwa na hoja ya kutotambua uchaguzi ule...hold on hivi yule mbunge wao mmoja anafanya nini bungeni....au chadema wanatambua ushindi wake! More confusion!
 
Je wabunge wa CUF walienda mahakamani hima? Kama walienda mahakamani kupinga kufukuzwa basi hapo kuna double standards! Bila hivyo hakuna.
 
Je ikionekana wamefukuzwa kihalali hizi Siku watakazoingia bungeni Hadi uamuzi huoni Kodi yetu itakua imeenda bure Kwa malipo yao
Ina tokana na kuheshimu utawala bora ndiyo sababu ya milolongo hiyo. Ingekuwa ni udikteta siku hiyo wangefukuzwa bungeni na kucharazwa viboko sita sita! Sasa wewe unataka kipi hapo?
 
CAG alipokagua hesabu za hiki Chama alisema Mbowe anatumbua kwenye Mikutano isiyo na tija?
 

Hivi sipendi anachoongea, anavoyongea au anayeongea?, hapa ndio sijaelewa.
 
Mwanzoni kabisa wakati wa hili sakata, tulielezwa kwamba katika hao 19 waliofukuzwa Chadema, ni 14 tu ndio waliokata rufaa, means kina dada 5 walikubaliana na hukumu ya chama chao, swali sasa; bungeni walikua wanafanya nini?
 
Mkuu nashukuru kwa kunifunga speed govenor naheshimu hisia zako, lakini hata ningefanya subira kama unavyoshauri, bado siwezi kubadilisha nilichosema.
Ni kweli kuna tatizo sana kwenye taifa letu, na matabaka yaliimarisha na uadui mkubwa ulojengwa na awamu ile! Kuondoa matabaka yale tu, tufikie uwanja na mapambano kuna kazi! Tukubaliane kwamba, Mbowe, pamoja na mapungufu yoyote anayoweza kuwa nayo, amebatizwa kwa moto kwenye ile kesi ya mchongo!
Sasa hivi mpambano Ni kuondoa matabaka, kurudisha nchi kwenye siasa za vyama vingi!! Tunapambana kukiwa na watu almost 100 percent, mjengoni ambao wameingia kwa mchongo! Watu wanaoamua hatima ya nchi yetu kwa sasa! Mazaa anaye sign mikataba, na kukopa mikopo, itakayo kuwa mizigo kwa watoto wetu na watoto wao! Mazaa na wanamchongo wa mihimili yote mitatu, ambao hatuna nia (wala uwezo, wa kuwatoa kwa mtutu wa bunduki!
Tunapaswa kuwa na subra ndugu yangu, Tindo! Hii mikutano na ikulu, hili la kupambana na wale COVID-19, na hata kukiwa na mchakato wa kuwa na 19 wengine, Au hata nafasi zozote kuingia mjengoni, tuzitumie Ni fursa! Kama watu wapo mle kimichongo tu, kwanini wapigania haki wa ukweli wasiwepo mle? Hii struggle haitakuwa kwa siku moja! Pengine wakati wetu wa kuishi utajengwa msingi tu, Lakini our nation will flourish! Kwa jasho, machozi na damu ya Watanzania, taifa letu litapata ukombozi wa pili. Hakuna haja ya kukata tamaa, ama kuvunjwa moyo wa umoja, let’s keep the fire burning!
 
Ukiachana na siasa chafu , za kishamba na za kipumbavu zinazosimamiwa na viongozi wa ccm, Tanzania ni moja ya nchi Tajiri sana. Kama focus ingewekwa kwenye utumiaji wa rasilimali tulizonazo kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Wewe ukiteuliwa Ubunge na Rais au Ndugai ungekataa ?
Mi sijapata kuona katika hii nchi yetu kabisa.
Mbatia akiwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi aliyeuliwa Ubunge na Kikwete mbona hakukataa.

Siasa za Tanzania hazijafikia hatua ya kutanguliza maslahi ya upinzani

Kama Mwenyekiti Mbatia na Katibu Mkuu kama Maalim Seif wanashindwa kuishi bila teuzi za CCM wewe utaweza ?

Wewe umemzidi uzalendo Maalim Seifu ?

Ndio maana Nchi hii kuitoa CCM madarakani inashindikana.

Karibu asilimia 99 ya wanamageuzi wanafikiria matumbo yao tu.

Hebu nijibu.

Mbowe ni Mwenyekiti wa kuchaguliwa au wa Milele ?

Ni kwanini haitoshi uchaguzi wa mwwnyekiti wakati muda wake imeisha ?

Katiba ya Chadema unaruhusu Mwenyekiti kutumikia awamu ngapi ?

Nenda kwa Mwenyekiti Marando, Lyatonga, Cheyo, Yule Mzee wa Ubwabwa Hashim Rungwe nk.

Mbona wote hawataki kuachia madaraka na wewe kama huoni vile

Halafu mnakuja kuwanyooshea vidole akina Mdee.

Siasa za Upinzani za hapa nchini ni za kujikimu na Njaa tu.
La wapinzani wangesha chukua Dola siku nyingi sana.

Ona wanavyohangaika watu wazito sana akina Lowasa, Sumaye, Membe, Lyatonga, W. Slaa, Mbatia, nk.
Sembuse akina Mdee.
Sembuse raia tu.

Kinacho waponza akina mdee ni wivu tu. Watu walitaka wawateue watu wao kwenye hizo nafasi.
 

Sielewi hata unaoongea nini zaidi ya kuona umepanic.
 

Kula lunch Kwa bill yangu

Very well said
 
Eti Nimepaniki
Na hutoweza kunielewa.
Kwakuwa umeziba masikio kusikiliza kwa makini nilicho kisema.

Nasema hivi, ukipanic lazima utaongea vitu vya ajabu, kwenye post yako umemtaja Marando, yeye ni nani ili nijue kama hujapanic? Isitoshe ulichoandika hakina mtiririko mzuri, na umechanganywa mambo mengi kwa pamoja, mpaka nimeshindwa kuelewa hoja yako ni nini hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…