Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

ila niseme tu, Mheshimiwa Magufuli (r.i.p) nahisi alikuwa na kitu flani spesho sana....kama huku kwetu tungesema alimeza nyongo ya simba ambayo hufanya mtu aogopwe kupita kiasi. aisee aliogopwa yule mheshimiwa bwana tuache utani; hakuna hata aliyejaribu kufanya fyoko zaidi ya kushangilia tu kwa kila alilofanya au kusema!

kama si hivyo na kuogopwa kule kulisababishwa tu na uraisi wake, basi niseme uraisi tanzania una nguvu ya ajabu sana nae alijua vema kuzitumia nguvu hizo!!
Hilo linaelezeka.
Mtu mwenye mikono ya damu ni wa kuogopa.
 
Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia amemtaka Waziri wa Ujenzi kuangalia namna ya kuiwezesha TAZARA kuwa na treni ya umeme.
Dr. Tulia amesema Tanzania ni moja na Wananchi wa pande zote wanahitaji maendeleo hivyo Kanda ya Nyanda za Juu Jusini wamechoka kuwa washangiliaji.

Kadhalika Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi na Huduma stahiki kama ilivyo katika majiji mengine na badala yake Mbeya imekuwa kama Halmashauri.

Tulia amesema miundombinu ya Mbeya ni mibovu sana na miaka yote wamekuwa wakipewa bajeti ndogo isiyokidhi chochote.

Dr. Tulia alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.

Source: Bungeni
Na sisi wa huku Mafia tunataka kuwa kama Dubai bana!
 
Uzuri hakuchaguliwa na wanambeya hata aongee ujinga hamna shida
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

ila niseme tu, Mheshimiwa Magufuli (r.i.p) nahisi alikuwa na kitu flani spesho sana....kama huku kwetu tungesema alimeza nyongo ya simba ambayo hufanya mtu aogopwe kupita kiasi. aisee aliogopwa yule mheshimiwa bwana tuache utani; hakuna hata aliyejaribu kufanya fyoko zaidi ya kushangilia tu kwa kila alilofanya au kusema!

kama si hivyo na kuogopwa kule kulisababishwa tu na uraisi wake, basi niseme uraisi tanzania una nguvu ya ajabu sana nae alijua vema kuzitumia nguvu hizo!!
Katiba yetu ni mbovu sana.

Ndiyo inayompa mamlaka na nguvu kubwa rais wetu ya kuamua na kufanya jambo lolote lile kwa kadri apendavyo na aonavyo inafaa.

Itoshe tu kusema katiba yetu ni mbovu na inapaswa wanasiasa wapenda nchi wapiganie katiba mpya mpaka kieleweke.
 
Kwahiyo katiba mpya ndio suluhisho?

Pale Kenya haijawasaidia chochote wako kwenye BBI mahakamani!
 
Kwahiyo katiba mpya ndio suluhisho?

Pale Kenya haijawasaidia chochote wako kwenye BBI mahakamani!
Katiba mpya sio tu ni suluhisho bali ni zaidi ya suluhisho.

Uwepo wa katiba mbovu inayompa mtu mmoja mamlaka makubwa ya kuamua kila kitu inaweza kupelekea hata wengine kushindwa kutimiza baadhi ya vipengele vya katiba wanavyotakiwa kutimiza.

Mfano,mwendazake amekaliliwa akiwaambia wakurugenzi ole zao wawatangaze wapinzani ushindi hali ya kuwa yeye ndiye anayewateua na kuwalipa mishahara.

Unafikiri kwa mazingira hayo mkurungenzi atakuwa na uthubutu wa takwa la kikatiba la kumtangaza mshindi wa uchaguzi wakati kashapigwa biti?

Tuachane na hii katiba ya mtu mmoja kuwa mungu.

Trump alitaka kuleta ujinga wake US kutokana na katiba bora ya US kila mmoja anajua alichokipata.
 
Kwa kweli tumepata uhuru sasa!
 
Back
Top Bottom