Dkt. Tulia suala la bandari hata wazee huzeeka na upumbavu wao

SPIKA wa Bunge, Tulia Akson amewajia juu watanzania waosema bandari imeuzwa na kubainisha kuwa Mtu mpumbavu anazeeka na upumbavu wake.

"wako baba zangu, wako mama zangu, jambo la uhakika kama ambavyo vijana wenye busara wanazeeka wakiwa na busara, kama ambavyo wako watu wenye hekima wanazeeka na wakiwa na hekima na hata wapumbavu huzeeka na upumbavu wao"

"Kama nchi imeuzwa wewe umeuzwa shilingi ngapi? kabla ya bei yangu mimi maana mimi jamani wana mbeya wananithamini sana kwa hiyo mimi ni mtu wa thamani kwa hiyo bei yangu itqkuwa juu kidogo si ndiyo jamani sasa wewe wa kawaida bei yako shingili ngapi jibu huna?

unasema bandari imeuzwa haya sawa nimekubali swali shilingi ngapi ili nijue Mbeya mjini mgao utakuwa kiasi gani si wewe unaijua bei sasa kama bei hujui wewe sio sehemu ya sheria mimi nimesoma kama kuna vibao vinasema elimu mwisho hapa mimi sikuishia hapo nilieda mbali zaidi mimi sio tu mwanasheria msomi ahh, mimi ni mtafiti nilikuwa nafundisha sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam, ule mkataba msiwe na wasiwasi mimi mbunge wenu kama mwakilishi wenu nasema hivi tuko salama, Mbeya mjini tuko salama, tanzania tuko salama, na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan yeye yuko salama usimsikilize mtu.

Mtu mpumbavu wako baba zangu, wako mama zangu, jambo la uhakika kama ambavyo vijana wenye busara wanazeeka wakiwa na busara, kama ambavyo wako watu wenye hekima wanazeeka na wakiwa na hekima na hata wapumbavu huzeeka na upumbavu wao.

Source: Haroub TV.
[emoji7][emoji7][emoji7][emoji2956][emoji123]
 
Ni sawa tu, hata wapumbavu huzeeka na ujuha wao, ajibu Hoja,huo usalama anaousema upo wapi ndani ya mkataba, sio kuleta mbambamba.
Upo....

DP WORLD hawatojihusisha na mafuta....

DP WORLD hawatojihusisha na USALAMA babdarini....

DP WORLD hawatafukuza wafanyakazi waliowakuta na hawatoajiri wageni.....
 
Haya sasa, hata saa mbovu wakati mwingine inasema ukweli, so jibu hoja za hao wapumbavu ambayo wewe umewarefer kama wapumbavu
Hana JIBU jibu lake ndio hilo kuwaona km wapumbavu tu in short amewadharau
 
Kiburi cha madaraka tena ya kupewa.
Aibu sana huyu.

Nchi ni ya waTz wote. Waachwe wenye hofu wahoji . Tatizo ni nini
Ni kweli...

Tatizo ni hoja za kipumbavu kutoka kwa wazee tunaowajua na kuwaheshimu kwa werevu wao......[emoji1787]
 
Upo....

DP WORLD hawatojihusisha na mafuta....

DP WORLD hawatojihusisha na USALAMA babdarini....

DP WORLD hawatafukuza wafanyakazi waliowakuta na hawatoajiri wageni.....
Kwa muda gani hawatojihusisha ?
 
SPIKA wa Bunge, Tulia Akson amewajia juu watanzania waosema bandari imeuzwa na kubainisha kuwa Mtu mpumbavu anazeeka na upumbavu wake.

"wako baba zangu, wako mama zangu, jambo la uhakika kama ambavyo vijana wenye busara wanazeeka wakiwa na busara, kama ambavyo wako watu wenye hekima wanazeeka na wakiwa na hekima na hata wapumbavu huzeeka na upumbavu wao"

"Kama nchi imeuzwa wewe umeuzwa shilingi ngapi? kabla ya bei yangu mimi maana mimi jamani wana mbeya wananithamini sana kwa hiyo mimi ni mtu wa thamani kwa hiyo bei yangu itqkuwa juu kidogo si ndiyo jamani sasa wewe wa kawaida bei yako shingili ngapi jibu huna?

unasema bandari imeuzwa haya sawa nimekubali swali shilingi ngapi ili nijue Mbeya mjini mgao utakuwa kiasi gani si wewe unaijua bei sasa kama bei hujui wewe sio sehemu ya sheria mimi nimesoma kama kuna vibao vinasema elimu mwisho hapa mimi sikuishia hapo nilieda mbali zaidi mimi sio tu mwanasheria msomi ahh, mimi ni mtafiti nilikuwa nafundisha sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam, ule mkataba msiwe na wasiwasi mimi mbunge wenu kama mwakilishi wenu nasema hivi tuko salama, Mbeya mjini tuko salama, tanzania tuko salama, na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan yeye yuko salama usimsikilize mtu.

Mtu mpumbavu wako baba zangu, wako mama zangu, jambo la uhakika kama ambavyo vijana wenye busara wanazeeka wakiwa na busara, kama ambavyo wako watu wenye hekima wanazeeka na wakiwa na hekima na hata wapumbavu huzeeka na upumbavu wao.

Source: Haroub TV.
Imegawiwa bure ndo sentence sahihi
 
Nadhani kuna shida hakuna mtu.anapinga Dp World. kuwekeza .Kinachopingwa ni vipengele vibovu vilivyoko kwenye mkataba

Watu waache kuongea sababu wazeeeka? Kwani wazee hawana haki ya kuongea kuwa mtu akizeeka afunge mdomo?
Hakusema kila mzee asihoji....

Hakumaanisha kila mzee ni MPUMBAVU...

Mkataba na DP WORLD unakwenda kuliinua taifa kiuchumi[emoji120]
 
Wananchi ndio tunajua wapi ni wapumbavu na wepi ni machawa.
Mwananchi mmoja ni mimi....nimefahamu kuwa mh.Dr Tulia ni mwerevu sana ambaye anafahamu kuwa kuna baadhi ya wazee ni WAPUMBAVU[emoji120]
 
Kitu ninachoendelea kujifunza hapa nchini ni kuwa, ukipata nafasi yoyote ndani ya serikali ya CCM basi hakikisha akili yako kama hii tunayotumia kuhoji na kuuliza humu, kila siku ukiwa unatoka ndani ya nyumba yako unaiacha mlangoni.

Unaporudi unaichukua na kuingia nayo ndani, vinginevyo ni hatari sana, katiba haina maana kwetu.
 
Sasa hapo wewe SI ndiyo umeonekana kituko kabisa kuliko hao wazee?wazee wanamaswali Yao,toa majibu acha kushambulia.
 
Back
Top Bottom