Dkt. Wilbroad Slaa: Viongozi wakubwa serikalini na CCM wapatao 38 wamenipigia kuniunga mkono katika kupinga uuzwaji wa bandari za Tanganyika

We tunajua kiasi cha pesa ulizochukua na tunajua umechukua kwa nani, ukiendelea tutawataja kwa majina yenu halisi. Huyo babu naye ameshalambishwa na kingine kinachomsumbua ni udini
Wewe Mwalimu uliyepo halmashauri ambae unahangaikia uhamisho unajipa ukubwa huu kweli? Jf nzuri sana kila mtu anajipa ukubwa
 
Hao 38 ni wazee wa vimemo wanufaika wa upigaji.

DP itazua wizi.

Wanaopinga DP ni wezi,wananchi wa kawaida wao wametulia tu
 
Endelea kuamini
 
Huyu inabidi watrepu simu zake, tuwajue hao wasaliti
 
Aibu sana kuuza nchi sema huyo mama anadanganywa mno nae anaingia mkenge tatizo la kuamini wahuni ndio hili hawakawii kukuingiza cha kike.

Halafu huyo mama akishagundua kuwa kadanganywa analazimisha kila mtu ahusike ile afiche aibu yake.

Kalazimisha bunge kupitisha huo ujinga na nec ya CCM.

Uungwana na kuchutama sio kufanya aibu yako binafsi kuwa ya kila mtu.
 
Hilo lipo wazi sana. Viongozi na wanaCCM wengi wa Tanganyika wanalaani sana huu mkataba wa DP, wanakosa tu ujasiri wa kusema wazi. Wengi wameamua kukaa kimya kwa sababu ya woga.
 
Hakika hii nchi imebarikiwa Sana. Ina nyumbu wa Serengeti na nyumbu wa mijini. Inahitaji ujasiri wa kiwango cha juu kumuamini mla mihogo.
 
Dr. Slaa ni mtu msomi na anajua anachokifanya hao watu watakuwa wamemruhu aseme hivyo jumla jumla
 
Binafsi nampenda sana Dk. Slaa tangu akiwa Chadema na alipokuja CCM nilifurahi sana kwasababu ni mtu mwenye msimamo thabiti. Lakini, kwenye suala la DP World simuungi mkono. Ninakibali Bandari yeti (zetu) kubinafsiwa ila tuwe na maslahi chanya kama nchi. Lakini kusema tusibinafsishe eti kwasababu ya blah, blah,blah, HAPANA!!!
 
Acha dharau za chini chini! Dr Silaa alisha acha upadiri na ana mke sasa! Tafafhari P
 
Huyu Slaa anabwabwa tu. Rais ampe ubalozi wa antarctic au maryupol atuondolee kelele.
 
Mawazo mazuri ya bwana Silaa kuhusu bandari yazingatiwe tu hayana ubaya
 
Mwongo tu huyo.


Kuna mkataba upi na DP World?
 
Mmm usivyoaminika nani ampigie simu mtu asiyeaminika anayenunulika si bora wenyewe waongee tu wajulikane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…