Pre GE2025 Dkt. Willibrod Slaa aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na kesi

Pre GE2025 Dkt. Willibrod Slaa aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na kesi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.
Kwahio kwanini walimshikilia? Upumbavu mwingine Unakera Sana.
 
Je watamlipa muda waliompetezea? Hii nchi inaendeshwa na wasio na uwezo. Yani unamkamata mtu halafu baadae unasema DPP hana nia yakuendelea na kesi. 🚮
Amepewa dhamana boss. Hajashinda kesi. Mbona unaropoka hivi, mbele za watu. Hapa ulijiona unajua sana wakati unaandika😂😂😂😂.
 
Kwahio kwanini walimshikilia? Upumbavu mwingine Unakera Sana.
Wewe hadi leo hujui kwanini alikamatwa na hujui kwanini anaachiwa kwa dhamana na sababu umepewa hapo. It means angeendelea kukaa gerezani kama mahabusu maana hamna haja yeye kuhudhuria mahakama while mambo yake bado.
 
Safi sana
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Shauri Na.993 la mwaka 2025 lilidai Dkt. Slaa ameshtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter).

Leo February 27,2025, Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga .

Wakili Mrema ameieleza Mahakama kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.
View attachment 3251757

Amepewa dhamana boss. Hajashinda kesi. Mbona unaropoka hivi, mbele za watu. Hapa ulijiona unajua sana wakati unaandika😂😂😂😂.
Taarifa inasema kaachiwa huru,DPP hana nia ya kuendelea na kesi,wewe unakomenti kua KAPEWA DHAMANA,namna gani hapa?
 
Ukiambiwa tii sheria bila shuruti mwangalie Slaa

Maisha yangu yote toka nimfahamu Slaa sijawahi.muona ana ndevu kama za Osama bin Laden

Yaani hapo wanafanana kama mapacha na Osama bin Laden

Chezea kuwekwa ndani wewe. Tii sheria bila shurti
Your time is loading utakwenda tu na.wewe huko shimo la tewa
 
Taarifa inasema kaachiwa huru,DPP hana nia ya kuendelea na kesi,wewe unakomenti kua KAPEWA DHAMANA,namna gani hapa?
Ndio nakueleza ametoka kwa dhamana. Taarifa hiyo hiyo uliyosoma. Umeelezwa mahakama haina haja kuendelea na kesi. Kuna eneo umeandikiwa kashinda kesi?
Kwanini alipwe. Umri huo hufahamu grounds za mtu kulipwa endapo atashinda kesi. Kesi zipo aina tofauti. Slaa hana kesi ya kulipwa hata angeshinda hiyo kesi. Labda afungue kesi ya madai tena hyo kesi ashinde without reasonable doubts. Tusome jamani. Tuache story za vijiweni.
 
Back
Top Bottom