Pre GE2025 Dkt. Willibrod Slaa aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na kesi

Pre GE2025 Dkt. Willibrod Slaa aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na kesi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Roho za watesaji zimefarijika sana baada ya kumemtesa Slaa bila sababu.
 
Dr.Slaa moto ni ule ule🔥
Hapana.
Hii inafungua ukurasa mpya.
Huo "moto" unao usema wewe ulikuwa ni moto wa kupikia ugali, sasa unatakiwa moto wa kupikia maharage.
Moto unao endana na udhalimu na udhalilishaji wanao uonyesha serikali na chama chao.
 
Amepewa dhamana boss. Hajashinda kesi. Mbona unaropoka hivi, mbele za watu. Hapa ulijiona unajua sana wakati unaandika😂😂😂😂.
Nadhani una tatizo kwenye ubongo wako. Soma hiyo 👇
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.
 
Tehetehe...... Naona kasahau mkanda wa suruali gerezani, kidevu kimechakaa kama msagishaji wa mashine ya unga
Huwa ni raha sana kushabikia uonevu hadi pale utakapoangukia upande wako.

Wakati Gen Z wanauwawa na kutekwa June 2024 mawaziri na viongozi wa serikali walisema wale vijana ni wahaini hivyo wanastahili yote hayo.

Hadi pale mtoto wa waziri wa utumishi wa umma Justine Muturi alipotekwa na kutoonekana kwa siku zaidi ya 3 huku akiwapigia simu viongozi wa vyombo vya usalama kama polisi, mkurugenzi wa usalama wa taifa na mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai hao wote walimjibu hawamshikilii mwanae.

Hadi pale alipopata nafasi kuonana na rais Ruto ikulu ndio kumuelezea ndipo akapigiwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa na akakiri kijana wa waziri wanamshikilia na rais akatoa order aachiliwe ndio mkurugenzi wa usalama wa taifa akasema baada ya saa 1 atakuwa ameachiliwa haya yote yalikuja kuwa waziri baada ya waziri kuzungumza kwenye vyombo vya habari na ghafla akaonekana msaliti , je ni vijana wangapi walitekwa na wazazi hawajui walipo sababu hawana access na rais?

Narudia tena ni rahisi furahia uonevu hadi pale utakapoangukia upande wako.

View: https://youtu.be/D_GjnYQOhFo?si=UpPAGHzyvqdEOYJq
 
Ipo siku DPP atatulaza selo maksudi ili atembee na wake zetu majumbani,

Afu akishamaliza anatuachia huru turudi majumbani mwetu maana hajiskii tena Kuendelea na kesi
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Shauri Na.993 la mwaka 2025 lilidai Dkt. Slaa ameshtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter).

Leo February 27,2025, Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga .

Wakili Mrema ameieleza Mahakama kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Source: Millard Ayo, Nipashe
Kupata vichekesho kama hivi andika napita KWENDA no 15777
 
Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachilia huru Dk. wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Shauri Na.993 la mwaka 2025 Dk. Slaa alishtakiwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X zamani Twitter

Leo February 27,2025 wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga .

Wakili Mrema alieleza mahakamani hapo kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.
 
Attachments

  • aa90bbc0-8fc4-4225-a1b2-8782587fafc5.jpeg
    aa90bbc0-8fc4-4225-a1b2-8782587fafc5.jpeg
    91.9 KB · Views: 1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Shauri Na.993 la mwaka 2025 lilidai Dkt. Slaa ameshtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter).

Leo February 27,2025, Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga .

Wakili Mrema ameieleza Mahakama kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Source: Millard Ayo, Nipashe
Huo ulikuwa ni Uonevu tu.

Je, huyo DPP atamlipa fidia huyo Dkt. Slaa kwa kumpotezea muda na mateso?
 
Back
Top Bottom