Pre GE2025 Dkt. Willibrod Slaa aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na kesi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Shauri Na.993 la mwaka 2025 lilidai Dkt. Slaa ameshtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter).

Leo February 27,2025, Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga .

Wakili Mrema ameieleza Mahakama kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Source: Millard Ayo, Nipashe
Kuna ndoto niliota jana kwamba huyu mzee kuanzia ishu ya kuropoka mpaka kukamatwa na kuwekwa lupango bila dhamana ilikuwa project ya kimkakati kwamba mzee aonekane yuko kinyume na bi-mkubwa ili Chadema waingie mtego wa kumuamini kwa mara nyingine wampokee na kumpa kiti ili akamalizie "kazi maalum" then akimaliza anapita hivi
Mpaka Chadema waje kustuka kwamba waliingizwa chaka na ccm inakuwa too late!
Ni ndoto tu lakini .
 
100%✓
 
DPP ni shetani kabisa na tunaongozwa na mashetani, unamtesa mtu ndani kumkomoa kisa haja sifia then una mwachia huru. Pumbavu kabisa
 
Mambo ya hovyo sana, eti sina haja ya kuendelea na hii kesi.

Halafu mtu anaachiwa hakuna fidia wala chochote, sheria za hovyo kabisa.
Incase kafia mahabusu na alikuwa hana hatia ingekuwaje?
 
Kuna mambo mengine yana fanywa na viobgozi wa EAC ni kuchekesha sana, wameona aibu wenyewe, kule besigye kaachiwa na Tz wakaona aibu pia wakakimbia kumwachia slaa, ni kesi kijinga tu za watu incompetence walioshika madaraka.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Shauri Na.993 la mwaka 2025 lilidai Dkt. Slaa ameshtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter).

Leo February 27,2025, Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga .

Wakili Mrema ameieleza Mahakama kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Source: Millard Ayo, TBC
Mungu Mwema 🙏
 
Back
Top Bottom