Dkt. Yahaya Nawanda apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Ulawiti, aachiwa kwa dhamana

Dkt. Yahaya Nawanda apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Ulawiti, aachiwa kwa dhamana

Ameburuzwa kwenye Mahakama ya Mkoa wa Mwanza akikabiliwa na kosa moja la Ulawiti

Amepandishwa leo July 9 baada ya makelele mengi ya wadau kutaka haki itendeke

Bado haijajulikana kama ataswekwa Rumande au atapata dhamana.

====

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shitaka moja la kumwingilia kinyume na maumbile Tumsiime Ngemela (21) katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.

Mshtakiwa huyo amefikishwa katika mahakama hiyo mapema leo Julai 9, 2024 na kusomewa shitaka hilo ambalo anadaiwa kulitenda Juni 2, 2024 katika eneo hilo kinyume na kifungu cha sheria cha 154 kifungu kidogo (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Erick Maley, Waendesha mashtaka wa kesi hiyo ambao ni Wakili wa serikali Magreth Mwaseba na Martha Mtiti waliitaja kesi hiyo kuwa ni kesi namba 1883 ya mwaka 2024.

Hatahivyo mshtakiwa alikana shtaka hilo na yuko nje ya dhamana baada ya kukamilisha masharti aliyokuwa amewekewa ambayo ni kuwa mtumishi wa serikali pamoja na bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh 5 milioni.

Baada ya kukamilisha masharti hayo, Mshtakiwa yupo nje ya dhamana hadi Julai 16, 2024 ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa hoja za awali huku upande wa mlalamikaji ukitakiwa kwenda na mashahidi.

Pia soma
Vipi yule wa Kilwa na Manyara?
 
Kama ingekuwa nchi kama Marekani ambako kuna makampuni ya uchunguzi yaliyosajiliwa kampuni mojawapo ingepewa kazi na wakili wa mtuhumiwa kuchunguza credibility ya huyo binti yaani matendo yake ya nyuma , kama aliwahi kudanganya kwa masuala ya kisheria, ikithibitika aliwahi kuongopa basi kesi ingetupwa. Rejea kesi ya Rais wa zamani wa banki ya Dunia ilikuwa kama hii. Kuna binti mfanyakazi wa hoteli alimpakazia kuwa amembaka, Huyo binti anatoka Africa Magharibi, basi hiyo kampuni ikafanya uchunguzi ikaonekana huko nyuma huyo binti wakati anaomba visa kuingia Marekani aliwahi kudanganya hivyo sio credible; kwa,msingi huo kesi ya ubakaji dhidi ya Rais huyo wa zamani wa benki ya dunia ikatupwa.
Yaani uliyetoa post haujui maana ya credibility na una ufahamu mdogo sana wa kesi za jinai. kwa kukusaidia;

1. credibility ya shahidi huwa haipimwi na previous conducts, wala bad character, inapimwa kwa kuaassess the coherence of the testimony of that witness WAKATI ULE ANAPOONGEA NA SIO KABLA AU BAADA, kwa lugha nyepesi kwa msio wanasheria, mahakama inakuwa inamwangalia usoni ione amenyooka mtiririko wake au anapindapinda and two, when the testimony of that witnesses is considered in relation to the evidence of other witness including that of the accused person.

kwahiyo watapima mtiririko wa ushahidi kuanzia upenzi wake wa zamani naye, walipoachana kwa kuomba sodoma, alipompigia simu ili waombane msamaha waanze ukurasa mpya, alipofika kwenye gari akakimbilia siti za nyuma na akamwingizia nyuma, au hata kama alisema rudi siti ya nyuma nitaingiza mbele halafu akailazimishia nyuma, alipompa pesa na kusema umasikini unautaka mwenyewe awe anatoa tako awe anampa pesa, aliporeport polisi mapema, alipowasiliana na mama, RC kwenda kuomba radhi kwa mama, RC kuhonga mihela kwa binti 10m na mama 3m, kuwapigia misimu marafiki wa binti.

vitu vitakavyounga mkono hapo huu mtiririko ni corroboration ya ushahidi wa mama, cctv footage, printouts za mitanao ya simu kuonyesha mameseji na namna alivyokuwa anapiga simu, ushahidi wa daktari PF3.

kwa taarifa yako, previous bad conduct kwenye ushahidi ni irrelevant. nakupa homework kasome s.56 ya Evidence Act, kwa mshitakiwa hata kama ana bad character huwezi kusema asiaminiwe, sembuse kwa shahidi. kwa mtiririko alioeleza binti, hajawahi kusema uongo. hata ile kesi ya Mpanda alipokuwa chini ya miaka 18 ya kutorokea kwa mwanaume, jamaa alitoka kwa technicalities tu ila ni kweli alimtorosha akaishi naye kinyuma. na kuishi ninyumba au umalaya wake wa kipindi cha nyuma haupunguzi uzito wowote ule wa tuhuma kwamba siku ya tukio alimlawiti.

dogo hii ndio sheria, tumekuwepo humu kwa miaka mingi mno.
 
Haya mambo ndo yanachochea ushoga na kuwaharibu wanawake.
Kumlawiti mwanamke ni aina nyingine ya ugonjwa wa akili, ingawaje kuna watu wengine humu huwa wanashadadia haya mambo ya kumla mwanamke tigo kisa ana chura.....tujitahidi sana kujiepusha na mambo yanayoweza kutuletea aibu kama haya.
 
Ameshitakiwa kwa kesi ndogo tuu, consensual relationship na sio ubakaji, hii ni kesi very light, akipata wakili mzuri, hakuna kesi hapo!.
Sheria ya Kanuni ya adhabu

Kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 154 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kinasema kwamba, mtu yeyote ambaye (a) anamuingilia mtu yeyote kinyume na maumbile au, (b) anamuingilia mnyama kimwili au (c) anamruhusu mwanaume kumwingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume na maumbile atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini.

Defence yake ni "binti ni mpenzi wake, katika kukuru kakara, ikapotea tuu njia, ndio ikapenye uwani, but it was not planned, its an accident!. Ukifanya jinai ya actus reus bila mens rea, japo ni kosa, lakini huna hatia!.
Hii kesi imeisha kabla haijaanza!.
Niliwahi kusema humu

Simtetei Dr. Nawanda, ila binti anaweza kuwa ni tatizo?.​

P
Sijui ulisikiliza maelezo ya huyo binti.

Alisema kabla ya hapo walikua na ugomvi kuhusiana na swala hilo hilo na liliwafanya watengane kwa muda.

Siku ya tukio akamwita anajua yamekwisha jamaa akaibua hoja upya na kufanya yake.

Binti hakuridhia na ndio kisa cha kwenda polisi.

Hivyo hayo unayoyaleta hapa utakua umeyatoa kichwani kwako.

Usipotoshe.
 
Of course, ni maswali mazuri ya kujiuliza. Lakini je, ndiyo ushahidi kuonyesha kwamba "alilawiti"?
Ndio, ni ushahidi mzito sana kama jaji ataona hakuna mtu yeyote nyuma ya huyo binti na wala hakushitaki hiyo kesi kujipatia pesa kwa udanganyifu.
 
Ameburuzwa kwenye Mahakama ya Mkoa wa Mwanza akikabiliwa na kosa moja la Ulawiti

Amepandishwa leo July 9 baada ya makelele mengi ya wadau kutaka haki itendeke

Bado haijajulikana kama ataswekwa Rumande au atapata dhamana.

====

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shitaka moja la kumwingilia kinyume na maumbile Tumsiime Ngemela (21) katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.

Mshtakiwa huyo amefikishwa katika mahakama hiyo mapema leo Julai 9, 2024 na kusomewa shitaka hilo ambalo anadaiwa kulitenda Juni 2, 2024 katika eneo hilo kinyume na kifungu cha sheria cha 154 kifungu kidogo (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Erick Maley, Waendesha mashtaka wa kesi hiyo ambao ni Wakili wa serikali Magreth Mwaseba na Martha Mtiti waliitaja kesi hiyo kuwa ni kesi namba 1883 ya mwaka 2024.

Hatahivyo mshtakiwa alikana shtaka hilo na yuko nje ya dhamana baada ya kukamilisha masharti aliyokuwa amewekewa ambayo ni kuwa mtumishi wa serikali pamoja na bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh 5 milioni.

Baada ya kukamilisha masharti hayo, Mshtakiwa yupo nje ya dhamana hadi Julai 16, 2024 ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa hoja za awali huku upande wa mlalamikaji ukitakiwa kwenda na mashahidi.

Pia soma
Baadae kesi itafutwa
 
Kwa nini aliwapa pesa huyo binti na mama yake?
Kwa nini alimwandikisha huyo binti barua inayosema alikuwa anatumika kisiasa?
Kwa nini mkuu wa mkoa wa Mwanza alikuwa anaingilia kesi ya huyo binti?
Huyo binti alipopimwa hospitali matokeo yalikuwa ni yapi?
Hii kesi inaweza kuisha vizuri kwa Nawanda kama haya yote hayakutokea au kwa kuvuruga tu ushahidi wote huu.
umefikiria vizuri sana.

1. kwanini aliwapa pesa (kuna ushahidi wa printout za voda na bank naamini watazitoa hwezi kwepa hilo, bank huwa haidanganyi, ruge alisema ogopa Mungu na tech).

2. kwanini alimwandikisha binti? binti ashatoa explanation why? imebaki kwake namwanda, aje aeleze mahakamani kama yeye hakuwa na uhusiano na binti ilikuwaje wamchukue na kumpeleka hotelini na kumwandikisha, na kwani amtaje yeye na si wengine, basi atataja na hao anaohofia kuwa wanamtuma binti kama ana ushahidi.

3. kwanini mkuu wa Mko mwanza aliingilia kesi? kwa ninavyoifahamu mahakama, watajiuliza, kama binti angekuwa anadanganya, kweli Mkuu wa Mkoa mwanza au namwanda baada ya kuandikisha barua, kwanini hawakummpeleka mahakamani kwa kusema uongo kwa mtu mkubwa kama yeye? kwanini walimute? wataishia kukiamini kile binti amekieleza.

4. binti alipopimwa ilionekana alilawitiwa, na zaidi ya yote, kwenye kesi kama hizo, cha muhimu huwa uwezekano wa penetration, sio lazima michubuko au shahawa kuonekana kwenye anus au k, penetration however slight inatosha hata bila kuchubua.

5. kinachombana, ni kwanini alianza kuhonga, kupiga simu kwa rafiki zake, kwa mama alienda n.k kama hakuwa na mahusiano naye. adi sasaivi naamini jamhuri wameshajihakikishia kwamba hakuna ubishi kwamba RC alikuwa na mahusiano na binti, na yeye naamini hatakataa manake watauliza iweje binti kama huyu akutaje wew mtu mkubwa namna hii asitaje wengine kama hamkuwa mnajuana naye kabla? na haujachukua hatua yeyote hata baada ya kusemekana amesema anatumika kisiasa kwa barua ambayo polisi waligoma kuitambua.

6. watamwuliza, kama haukutenda kosa, ilikuwaje uhangaike hivyo na usikanushe hata kwa vyombo vya habari tu. kweli RC utuhumiwe na kitoto kama kile halafu unyamaze tu kimya hadi leo kama haukutenda, inawezekanaje? jamaa yetu kimemramba. kwa wanaojua sheria, hapo ameenda.

zaidi sana, nilishawahi kushindwa kesi kwa namna hii hii, jamhuri walikuja na selemani makumba vs republic, kesi inasema ushahidi wa victim ni wa kuaminika zaidi kwasababu yeye ndiye aliexperience tukio hivyo binti akinyooka tu, umeisha. bye bye X-RC.
 
Back
Top Bottom