Dodoma: Afisa Mipango Miji asimamishwa kazi kwa kushindwa kutenda haki kwa Wananchi

Dodoma: Afisa Mipango Miji asimamishwa kazi kwa kushindwa kutenda haki kwa Wananchi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobasi Katambi ametangaza kumsimamisha kazi,Hadson Magomba,ambaye yupo kitengo cha mipango miji katika jiji la Dodoma kwa kushindwa kutenda haki kwa wananchi.

Katambi ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko yaliyotolewa na Mdala Mazengo wakati wa mkutano wa hadhara uliohusu kupokea malalamiko juu ya kudhurumiwa ardhi katika kata ya Ipagala Jijini Dodoma huku akitoa agizo la siku saba kwa mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi kuunda tume huru maalum ya uchunguzi dhidi ya dhuruma ambayo amefanyiwa Mdala Anna Mazengo kwa kudhurumiwa viwanja vyake na kupewa mtu mwingine.

Katika mkutano huo Mdala Anna ambaye ni mjane toka mwaka 1985 na mwenye watoto kumi huku watoto wawili wakiwa walishafariki dunia amesema kuwa aliporwa maeneo yake katika maeneo ya swaswa extation yenye ukubwa wa ekari sita.

Mdala Anna amesema kuwa pamoja na kuwa na eneo kubwa lakini afisa kitengo cha mipango miji wa Jiji la Dodoma ambaye alimtaja kwa jina la Hadson Magomba,alimnyanyasa kwa kutompa eneo lake huku akishindwa kumpa haki yake na kubadilisha matumizi na eneo hilo kuwapatia watu wengine.

"Mimi ni mjane tangu mwaka 1985 na mwenzangu aliniachia watoto kumi japo watoto wawili wameisha tangulia mbele ya haki,watoto waliobaki ninawatunza na nilikuwa na maeneo mbalimbali hasa maeneo ya swaswa zaidi ya heka sita.

" Cha kushangaza baadaye maeneo yangu yalitwaliwa na wakati yanatwaliwa nilikuwa na vielelezo vyote na nilijaribu kufuatilia lakini niliambulia vitisho na maneno ya kejeri na matusi.

"Nilienda katika kitengo cha mipango miji ili kuweza kusikilizwa lakini matokeo yake niliambulia kurushiwa barua na kama mbwa na Hadson Magomba jambo ambalo nilishindwa kupata msaada" alisema Mdala Anna.

Aidha Mdala Anna alisema kuwa kinachomshangaza ni kuona maeneo yake ualiyotwaliwa bila fidia anaona nyumba zikijengwa jambo ambalo alidhani labda ni nyumba za walimu jambo ambalo si kweli kumbe ni nyumba za watu binafsi.

Kutokana na malalamiko hayo Katambi ametoa agizo la kumsimamisha kazi Afisa wa kitengo cha mipango miji ya Jiji la Dodoma Hadson Magomba, huku akimwagiza mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi kuunda tume uchunguzi dhidi ya ofisa Huyo ndani ya siku saba.

Katambi alisema kuwa tume hiyo inatakiwa kuundwa na watumishi kutoka ofisi ya mkuu wa Wilaya,Ofisi ya TAKUKURU,Kamati ya ulinzi na usalana pamoja na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini.
 
Kama 1985 alikuwa na watoto 10 ina maana hao watoto ni watu wazima Sana na Wana familia zao wanajitafutia riziki. Watoto ndo wa kumwangalia huyo Bibi siyo Bibi kulea hayo mababa na mamama.
 
agizo la siku saba kwa mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi kuunda tume huru maalum ya uchunguzi dhidi ya dhuruma ambayo amefanyiwa Mdala Anna Mazengo kwa kudhurumiwa viwanja vyake na kupewa mtu mwingine.
INASIKITISHA SANA KUONA BADO KUNA WATU WALIOKABIDHIWA MAJUKUMU NA SERIKALI WANENDELEA KUTUMIA VYEO VYAO HIVYO KUNENEPESHA TUMBO ZAO!!!

SERIKALI HII IMEONYESHA UMAKINI MKUBWA KTK KUTETEA DHULMA DHIDI YA WADHULUMIWA, LAKN BADO KUNA SALIA MASWALI, JE, NI LINI DHULMA HIZO ZITAISHA KABISA?
JE, HAO WATENDAJI WALIOSHIKA VITENGO WAO BADO HAWAJAHISI KWAMBA NGAZI ZA JUU ZA UONGOZI SERIKALINI ZIPO MAKINI, NA KWAMBA ZINAFUATILIA KILA PEMBE NDANI YA TZ? HAWAOGOPI?

NICHUKUE FURSA HII KUWANASIHI WALE WALIOFANYA MADUDU HASA KTK SEKTA YA ARDHI, WAREKEBISHE WALIPOHARIBU KABLA MAMBO HAYAJAWAGEUKIA.
TUMECHOKA NA DHULMA HIZI NA TUNAIOMBEA SERIKALI IENDELEE KUSIMAMA IMARA DHIDI YA WALAFI.
 
Karibu uraiani afisa mipango miji

Ova
 
Hapo DC amefanya jambo jema sana kuunda tume huru, kwani sio kila anayelalamika anakuwa mkweli, na au anayelalamikiwa anakuwa ndie mkosaji,
 
Kama 1985 alikuwa na watoto 10 ina maana hao watoto ni watu wazima Sana na Wana familia zao wanajitafutia riziki. Watoto ndo wa kumwangalia huyo Bibi siyo Bibi kulea hayo mababa na mamama.
kwa hiyo kama watoto wake ni wakubwa ndio asidai haki zake? hiyo ardhi ni mali yake, sio ya watoto wake ndio maana anaipigania
 
Imeandikwa kila mtu atavuna alichokipanda..

Wakati Laizer anatangazwa kuwa billionaire mpya huku afisa mipango anaenda kuwa kapuku uraini.

Fundisho; jifunze kumheshimu mtu kutokana na nafasi yake alivyo maana hujui kesho atakuwa Nani na Wapi na wewe utakuwa Nan na utakuwa Wapi.
 
Back
Top Bottom