Uchaguzi 2020 Dodoma: Anthony Mavunde azomewa na wananchi

Uchaguzi 2020 Dodoma: Anthony Mavunde azomewa na wananchi

"Wee nenda, hautuhusu, hatujakuchagua, ingia kwenye gari yako uondoke...". Maneno mazito kweli kweli. Eh, hata Dodoma? Watapata sana taabu kwa unyang'anyi wao. Yaani, yaani.... ngoja tuone kati ya umma na jeshi nani ana nguvu. Bila shaka mwisho wao utakuwa mbaya sana kama ulivyo mwisho wa madikteta wote.

CCM kama ni mgeni ambaye amekwishapitisha siku zake za kuwa mgeni lakini hajitambui. Hata mkifanya mema vipi, kama watu wamekwisha wachoka haitasaidia. Mtajenga sana mabarabara, mabwawa, SGR... lakini hayatawaingiza katika mioyo ya watu. You have overstayed. Mtatakiwa kuiba kura tena 2025.
Umma hauna nguvu ya kushinda jeshi hata siku moja,na katika nchi yoyote.
Ni swala la kiubinadamu tu, kwakua kuua hakupendezi. Ila macho yakifumbwa na ikatakiwa ipimwe nguvu Kati ya majeshi na umma, hakuna anaeweza kusalimika.
 
Eti CCM bila Aibu bila kumuogopa mungu wapo wanaosherekea eti ushindi, hapo ndipo utajua makao makuu ya shetani Duniani ni CCM
Hahahah ila jamaa unachukia ccm kinoma, pole asee chama chenyewe miaka yote ndo kinashinda tu, pole asee.
 
Habari wakuu!

Jana, Oct 30 2020 Mbunge aliyeshinda jimbo la Dodoma mjini kwa tiketi ya CCM, ndugu Anthony Mavunde ameshindwa kuongea na wananchi wa Dodoma mjini baada ya kundi kubwa kuanza kumzomea.

Kitu hicho kilimpelekea kuingia kwenye gari na kuondoka kwa aibu kubwa.

Wananchi hao walisikika wakisema " WE NENDA, HATUKUTAKI , HATUJAKUCHAGUA, PANDA GARI UENDE ZAKO"

Hali iliyozua maswali mengi mtandaoni kwamba inakuwaje kuzomewa na kundi kubwa vile tena kipindi alipoenda kutoa shukrani kuchaguliwa?

Hii inaashiria nini tuendako? Na Dodoma si ngome ya CCM?

Je, wananchi wanatuma ujumbe gani kwa hili tukio?

Kusema wenye nchi ni wananchi?

Nisiwachoshe kwa maswali tazama mkasa mzima hapo chini.

View attachment 1616367
Kwangu mimi hapa ninapata maswali zaidi kuliko majibu! 1.Kama ni kikao Mhe.Anthony Mavunde Mbuge mteule kakiita mwenyewe mimi nisiyemtaka sitakwenda kwenye kikao hicho maana nina hiari ya kwenda au kutokwenda 2. Kwa nini niitike wito harafu nikafanye fujo?! Mimi ninahisi washindani wake walikwenda makusudi ili wakavuruge kikao chake! Hii siyo sawa, unless kuna maelezo ya ziada. Inajulikana hakuna aliyepata ushindi wa asili 100, walioshindwa wakubali matokeo, ndiyo ustaarab!
 
Naanzisha hashtag tutembee nayo from now...
👇
#WE_NENDA_HATUKUTAKI_HATUJAKUCHAGUA.
 
Kwanini msiwe wabunifu hata kukopy kwa nchi jirani mf. Kenya?
Eti tukopy Kenya nenda wewe kacopy kama itakusaidia au umeambiwa nchi hii ilipata uhuru kwa kukopy?staili hatukumtoa mkoloni kwa vita hiyo miaka ya 60 aliondoka kwa staili hii hii na ndivyo atakavyo ondoka mkoloni mweusi ccm.
 
Mbinu ile ile ya Wapinzani....."Rweikiza azomewa....", "JPM azomewa Bukoba..." aina hii ya 'siasa' itawachukua miaka mingine 100 kupewa uongozi..!
Kwanini msiwe wabunifu hata kukopy kwa nchi jirani mf. Kenya?
Ili tukio lilitokea kabla ya uchaguzi.Lakini mleta mada anasema baada ya uchaguzi.Halafu ni watu wachache tu waliokuwa wanafanya Fuji.Moderators taratibu watu wanaanza kushusha credibility ya Jf.Toeni taarifa za uwongo.
 
Sasa, sasa, saa ccm kwisha habari yao. Kwahiyo, kwahiyo kwahiyo tusitafutane ubaya. Mi naanda mawe mengi ili niingie nayo uwanjani wakati jpm atakapokuwa anaapiswa ili, ili, ili nimdungue
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
 
kuandamana kupo kwa aina nyingi na hii ni moja wapo kuonesha hisia za wananchi..... Pole kwa MAVUNDE.... CCM tunapaswa kujua kwa miaka mitano hii upinzania hauna cha kupoteza so wananchi watafanya lolote kwenu kama hamtotimiza mliyo ahidi.

CCM AGAIN....
 
Habari wakuu!

Jana, Oct 30 2020 Mbunge aliyeshinda jimbo la Dodoma mjini kwa tiketi ya CCM, ndugu Anthony Mavunde ameshindwa kuongea na wananchi wa Dodoma mjini baada ya kundi kubwa kuanza kumzomea.

Kitu hicho kilimpelekea kuingia kwenye gari na kuondoka kwa aibu kubwa.

Wananchi hao walisikika wakisema " WE NENDA, HATUKUTAKI , HATUJAKUCHAGUA, PANDA GARI UENDE ZAKO"

Hali iliyozua maswali mengi mtandaoni kwamba inakuwaje kuzomewa na kundi kubwa vile tena kipindi alipoenda kutoa shukrani kuchaguliwa?

Hii inaashiria nini tuendako? Na Dodoma si ngome ya CCM?

Je, wananchi wanatuma ujumbe gani kwa hili tukio?

Kusema wenye nchi ni wananchi?

Nisiwachoshe kwa maswali tazama mkasa mzima hapo chini.

View attachment 1616367

Kumbuka, kuvuruga mkutano huhitaji hata 10% ya audience. Those in the minority tend to be the noisiest!
 
Miaka 5 mateso jasho damu....vikwazo
Acha vikwazo vije kuliko Kuamrishwa na akina Amsterdam,hatutaki na hatujazoea ujinga huu . Hawajatupa pesa ya uchaguzi ni pesa yetu wenyewe kwa hiyo acha tuteseke. Na wala siyo kuteseka ni kufanya kazi ili uishi kuliko kutegemea kupewe .Kuna siku utaamrishwa ufanye ya aibu kama ambavyo Zitto na Membe walivyokuwa wanatangaza 'bata' baada ya ushindi wao na kuongoza nchi.Hilo bata lingewatokea puani.Mngevuliwa mpaka nguo za ndani .Unaogopa nini vikwazo wewe ni mwanaume ? au ulitahiriwa hospitalini ?
 
Meanwhile, under the Constitution, the legitimacy of presidential elections results cannot be questioned in any court of law regardless of the irregularities, illegality or fraud, leaving civil disobedience as the only way to reject flawed poll results.

My take.
Go out tomorrow for a nationwide protest.
Sijua wanasheria wetu wako wapi, hivi hiki kipengere sijui kama huwa hawaoni kama ni unconstitutional maana kina breach fundamental rights and Freedoms guranteed under the law. The right to free, fair and credible election. Kwenda mahakamani na kuomba muongozo wa hii breach of fundamental rights and freedom sio ku-question legitimacy of presidential elections results. Kwa maana nyingine kama kuna breacheas yeyote ya hiyo fundamental freedoms, athari yake ni kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi bila mkwaruzo...cha kutakiwa ni kwenda tu mahakamani kusema kwamba NEC wame- breach fundamental rights and freedoms zinazohusiana na uchaguzi juu ya free, fair and credible election na sio mambo mengineyo... tuone mahakama itasimamia upande gani kama inakubaliana na breaches hizo za fundamental rights and freedom za uchaguzi...Wanasheria, amkeni na changamkeni...hata UN sec council iliwahi kubwagwa na mahakama ya ulaya- someni Kadi case 1-2- summary yake ni hii: Kadi Case – Constitutional Core Values and International Law – Finding the Balance?
 
Acha vikwazo vije kuliko Kuamrishwa na akina Amsterdam,hatutaki na hatujazoea ujinga huu . Hawajatupa pesa ya uchaguzi ni pesa yetu wenyewe kwa hiyo acha tuteseke. Na wala siyo kuteseka ni kufanya kazi ili uishi kuliko kutegemea kupewe .Kuna siku utaamrishwa ufanye ya aibu kama ambavyo Zitto na Membe walivyokuwa wanatangaza 'bata' baada ya ushindi wao na kuongoza nchi.Hilo bata lingewatokea puani.Mngevuliwa mpaka nguo za ndani .Unaogopa nini vikwazo wewe ni mwanaume ? au ulitahiriwa hospitalini ?
Yaani tupate vikwazo kwa ajili ya waroho wa madaraka wachache?
 
Mbinu ile ile ya Wapinzani....."Rweikiza azomewa....", "JPM azomewa Bukoba..." aina hii ya 'siasa' itawachukua miaka mingine 100 kupewa uongozi..!
Kwanini msiwe wabunifu hata kukopy kwa nchi jirani mf. Kenya?
Mbinu ipi au unaropoka tu unajua Kenya waliamua kumwaga damu sababu ka hizi hizi za maccm kupora uchaguz,huu Ni mwanzo tu
 
Back
Top Bottom