Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Alikuwa sahihi tu....

Ninakumbuka maneno yake..."Mimi si mwanasiasa....".

Bungeni kuna wanasiasa...
Bungeni kuna siasa.....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Alifuata nn siasani? Ili uwe balozi nyumba kumi, mtendaji, diwani, mbunge, wazir, Rais ni lazima uwe mwanasiasa!! Je CCM alikua anatafuta nn? C angejitoa ili tujue hakua mwanasiasa? Weka vitu ambavyo ni reasonable!!
 
Bunge linapitisha azimio hili ili kumridhisha nani? Adhabu ya wabunge waliopitisha wote hawa asirudi bungeni mbunge hata mmoja wananchi wawakatae katika uchaguzi mkuu ujao. Huu ndio usaliti mkubwa wa nchi. Nani kawaloga wabunge wetu. Hii mikataba ya aina hii haitaishia kwenye bandari tu itatakiwa isainiwe kwenye miradi mingine pia ambayo kwa hoja kama hii haina ufanisi. Wenye ufanisi ndio hao wanaoingia mikataba na nchi yetu. Fikirieni hao wenye ufanisi watakapokuja na wataalamu wao waliobobea kwenye fani hizo, kuna mwananchi ataambulia post za juu kama si kuishia kufanya vibarua tu, kwa elimu na ujuzi upi kama tu hawa wameshindwa kuleta ufanisi? Duh! Mh, hao wafagiaji na wafanya usafi huenda wakawa na elimu za juu ili kuleta ufanisi
 
Kama uwekezaji utatuwezesha kufikia viwango vya bandari zingine hiyo Iko poa tu! Nchi ya wajinga huliwa na wajanja!

Hawa wote wanaoongoza nchi ni wazee tutaenda nao mavumbini na watoto wetu hawatafanya ujinga ujinga kama wao maana hawamjui Mwalimu Wa butiama Wala mkoloni wanamjua Magu tu and what he did for bongoland!
 
Hivi Bunge letu lina jipya na cha maana kweli ukiondoa compliance ya Katiba? Nina maanisha does it meet objectives of its establishment or it merely the matter of Katiba compliance?
Just a rubber stamp only.

Hivi wewe na akili zako ulitarajia bunge hili la Tz lingekuja na kitu chochote kipya na cha maana kuhusu suala hili????
Seriously???????!!!!?????????
 
DP World itakuza na kuchochea:-
# Kukua kwa sekta za uzalishaji
# Itakuza na kuongeza ajira kwa wazawa;
# Itakuza viwanda vya ndani;
# itaongeza pato la taifa;

CCM kupitia DP World mmeipiga pabaya CDM, ACT, NCCR, CUF, UP, NLD nk. Kwa vyovyote vile CCM lzm wananchi wawaamini tena 2025 - 2030.
Hongera sana SSH Mwenyekiti wa CCM taifa.

Msakila Kabende Msakila
Kakonko.
 
Ngojeni nilie kwanza nitacomment baadaye maana kwa Sasa jinsi nilivyo na hasira na Hawa wabunge wa fisi_emu naweza kutukana kabisa!View attachment 2652751
Pole sana ndugu, Ila hii picha haina uhalisia kwa upande wangu, kama alikuwa anakata mti apate kuni, sasa angepata vipi hizo kuni wakati huo mti ulikuwa unaangukia mtoni? Au alitaka kutuambia nini huyu artist. Ila nimeipenda imefungua akili yangu kutafakari kwa kina kuwa Watanzania hatuna pa kukimbilia, hapa ni kwetu na tupambane kwa akili zetu binafsi. Mwisho wa siku maamuzi ya mwisho ni yako, fanya kazi ulishe familia mengine Mungu atayamaliza.
 
Bunge limepitisha kwa 100% azimio la "kubinafsisha" bandari zote nchini kwa kampuni ya DP World, milele. Hongereni sana.!.

Mchezo umeisha kazi imeisha ,bandari zote zimebinafsishwa huko kwenye mjadala wa mkataba kumzidi akili mzungu au mwarabu sahau,alifanya hayo hayo magufuli kwenye mambo ya makinikia akatuahidi Noah kila mwananchi tuliziona ? Na trion 300+ tuliziona? Baadae kabudi akaja kusema ule mkataba au mazungumzo ilikuwa uongo.
 
Hakuna cha bure kuna Quid Pro Quo; kama kuna uwezekano wa watu kuvuna shamba la bibi kwa bei chee watafanya hivyo ukizingatia walamba asali hio Quid Pro Quo sio kwa manufaa ya Taifa bali kwa manufaa yao...., yaani ni wale ambao tunaweza kusema wana - Cut Their Noses to Spite their Faces, Nadhani wakimaliza huku hata Serengeti itakwenda....
 
Haya maandamano yanayofanywa na mashabiki wa yanga, wangeelekeza kuiondoa CCM tungekuwa mbali sana. Tate Mkuu unasemaje maana pia ni yanga lia lia huku CCM wakitupiga
Dah! Yaani tupo kama misukule vile. Watu hawa hawa ukiwaambia kesho wajitokeze kuandamana kudai Katiba Mpya ya wananchi, au kuishinikiza serikali kuacha kusaini mikataba ya Kimangungo; kamwe huwezi kuona mtu akijitokeza.
 
Potential side effects of giving Tanzania ports to DP World:

Increased foreign control over Tanzania's economy: DP World is a foreign company, and the deal gives it control over a major strategic asset in Tanzania. This could lead to increased foreign control over Tanzania's economy, which could have negative consequences for Tanzania's sovereignty and development.

Job losses: The deal could lead to job losses at the Port of Dar es Salaam, as DP World is likely to replace some Tanzanian workers with its own employees. This could have a negative impact on the Tanzanian economy and society.

Increased prices: DP World may raise prices for port services, which could make it more expensive for Tanzanian businesses to import and export goods. This could make Tanzanian goods less competitive in the global market, and it could also lead to higher prices for consumers.

Environmental damage: DP World's operations could cause environmental damage, such as pollution and the destruction of marine life. This could have a negative impact on Tanzania's environment and tourism industry.
 
Naunga mkono mkataba huu, ni mkataba wa kimkakati, kuna vifungu viwili virekebishwe

1: Muda, labda uwe wa miaka 33, baada ya miaka 33 ikiwa mkataba utaenda vizuri tuongeze tena muda.
2: Kifungu cha kuvunja mkataba, kuwe na provision ikiwa kuna sbb kubwa na ya msingi mkataba tunaweza kuuvunja

Mengine yote ni mazuri, manufaa ni makubwa sana.

Hongera sana Mh. Rais wetu, Mama Samia
 
Kwahiyo nyie mlitegemea bunge litakataa huo mkataba😃😃 basi mi nilikuwa mbeke ya muda maana nilishajua kitakachotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…