Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Mwl Nyerere aliwahi kusema huko nyuma kwamba , nanukuu "ANAYEKULA NYAMA YA MTU HAACHI" Mwisho wa kunukuu , kwa tafsiri pana maana ya usemi huu wa Nyerere ni kama ile methali ya wahenga iliyosema MAZOEA HUJENGA TABIA

Kwamba ukizoea kufanya jambo fulani basi utaendelea tu kulifanya hata kama ni baya , ili mradi wewe binafsi au familia yako inafaidika .

Bandari zetu wamepewa Waarabu kibwege kabisa kwa vile tu wenye mamlaka wameamua kuigawa ili wao wafaidike , nakuhakikishieni kwamba hakuta kuwa na ufanisi wowote ule , NIPO HAPA JF NIMEKAA , Yaani tunauza mali zetu kwa ajili ya uvivu tu wa kazi na fikra , yaani tunaamini tu kwamba hatuwezi , ila wanaoweza ni waarabu ! Poor Tanzania !

Tumesahau ya NET GROUP , ATCL , TRL , TTCL na hata RICHMOND , tulitumia nguvu kubwa kushawishi na kudanganya umma kwamba kutakuwa na Tija , leo kiko wapi ?

Haya mmeuza Bandari kwa watu wenu ni Shirika lipi lingine mnafuatia kuliuza ili tujiandae ?

Nakulilia Tanzania .

View attachment 2652644
Kwa meno yale na anapotokea, siwezi kumkatalia.
 
Mchaga kaongelea DP kukataliwa marekani, ila hapa ndo tuukubaliii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hivi mtu ukiwa CCM akili inahama?? Khaaaah
Kila akikataacho mmarekani ni lazima wengine wote wakikatae?!!!

Hivi unajua kuna "ujasusi wa kiuchumi"?!!!

Huu unaweza kumchafua "mfanyabiashara" yeyote yule [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

#MamaAnaupigaMwingi[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mjadala ulikuwa wa wazi kweli ni kitu kizuri, ila mjadala hakuwa fair kwa wanao ujadili hasa waliokuwa na hoja kinzani na mkataba hawakupewa mda wa kuwasilisha hoja zao ,zaidi ya kukatishwa katishwa kila mara,mfano Mdee alitolewa kwenye reli kabisa,yaani mdee kachangia dk 2 tu,dk zilizobaki ni spika kugeuka kuwa wakili upande wa mkataba na baadhi ya wabunge wenzake kumkatisha.

Hata ile maana ya uhuru wa kutoa maoni,bila kujali upo upande gani,naona kama imepotea.
 
Back
Top Bottom