Mwl Nyerere aliwahi kusema huko nyuma kwamba , nanukuu "ANAYEKULA NYAMA YA MTU HAACHI" Mwisho wa kunukuu , kwa tafsiri pana maana ya usemi huu wa Nyerere ni kama ile methali ya wahenga iliyosema MAZOEA HUJENGA TABIA
Kwamba ukizoea kufanya jambo fulani basi utaendelea tu kulifanya hata kama ni baya , ili mradi wewe binafsi au familia yako inafaidika .
Bandari zetu wamepewa Waarabu kibwege kabisa kwa vile tu wenye mamlaka wameamua kuigawa ili wao wafaidike , nakuhakikishieni kwamba hakuta kuwa na ufanisi wowote ule , NIPO HAPA JF NIMEKAA , Yaani tunauza mali zetu kwa ajili ya uvivu tu wa kazi na fikra , yaani tunaamini tu kwamba hatuwezi , ila wanaoweza ni waarabu ! Poor Tanzania !
Tumesahau ya NET GROUP , ATCL , TRL , TTCL na hata RICHMOND , tulitumia nguvu kubwa kushawishi na kudanganya umma kwamba kutakuwa na Tija , leo kiko wapi ?
Haya mmeuza Bandari kwa watu wenu ni Shirika lipi lingine mnafuatia kuliuza ili tujiandae ?
Nakulilia Tanzania .
View attachment 2652644