Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Leo nimesikiliza mwanzo mpaka mwisho wa mjadala wa Bunge kuhusu Mkataba huu.

Wahusika wamejitahidi kufafanua vipengele mbalimbali vilivyokuwa vinaleta utata kwa Watanzania.

Kwa maoni yangu, kama maelezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu Mkataba huu na ufafanuzi wake ni sahihi, nadhani mkataba huu hautakuwa na mapungufu mengi labda wawe wametuficha Mambo mengine ya hatari yaliyomo ndani ya mkataba huu.

Kipekee nawashukuru Watanzania wenzangu waliotilia shaka mkataba huu tangu uliposambazwa mitandaoni. Reaction ya iliyotokea ndo iliyofanya wahusika kuchambua zaidi Azimio hili kipengele kwa kipengele na kutoa ufafanuzi wa kina.
 
Nimeshawahi kushauri humu kwamba kwa hatua lilipofikia suala hili, Watanganyika wanatakiwa Kuanzisha MKAKATI MAALUMU NA WA DHARULA WA "KUZIHAMI" BANDARI ZA TANGANYIKA pamoja na Rasilimali nyinginezo za Tanganyika. Suala hili linatakiwa lifanyike mara moja bila ya kuchelewa.
Unataka kutufanyia maajabu ya dunia?!!

TANGANYIKA ilishaoza huko kaburini.....Tanganyika ni HAYATI....[emoji1787][emoji1787]

RiP Tanganyika[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hapo vip!!
Sitaki niongee maneno mengi kuhusu huu mkataba wa Dp world na mambo ya loliondo,kwasababu mambo mengi yamewekwa wazi dhidi ya ubaya wake kwa watanzania.

Kwasababu samia hataki kusikiliza maoni,madai na malalamiko ya watanzania wanyonge basi kupitia andiko hili watanzania wanyonge tunamkabidhi Mungu malalamiko yetu na tuna imani atatujibu kwa haraka.

Unapuunza maamuzi ya watanzania wengi ukijiona wewe una akili kuliko wao,hakika umejidanganya sana.

Naomba yeyote yule anayekubaliana na kumkabidhi Samia kwa Mungu ashughulike naye comments AMEN.
Mh.Rais SSH "asiposikiliza" watanzania....kuna nani mwingine atawasikiliza?!!![emoji1787][emoji1787]

Jina lake lenyewe ni "KUSIKIA-KUTAKA SULUHISHO"[emoji123]

#MamaAnaupigaMwingi[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema huko nyuma kwamba , nanukuu "ANAYEKULA NYAMA YA MTU HAACHI" Mwisho wa kunukuu , kwa tafsiri pana maana ya usemi huu wa Nyerere ni kama ile methali ya wahenga iliyosema MAZOEA HUJENGA TABIA

Kwamba ukizoea kufanya jambo fulani basi utaendelea tu kulifanya hata kama ni baya , ili mradi wewe binafsi au familia yako inafaidika .

Bandari zetu wamepewa Waarabu kibwege kabisa kwa vile tu wenye mamlaka wameamua kuigawa ili wao wafaidike , nakuhakikishieni kwamba hakuta kuwa na ufanisi wowote ule , NIPO HAPA JF NIMEKAA , Yaani tunauza mali zetu kwa ajili ya uvivu tu wa kazi na fikra , yaani tunaamini tu kwamba hatuwezi , ila wanaoweza ni waarabu ! Poor Tanzania !

Tumesahau ya NET GROUP , ATCL , TRL , TTCL na hata RICHMOND , tulitumia nguvu kubwa kushawishi na kudanganya umma kwamba kutakuwa na Tija , leo kiko wapi ?

Haya mmeuza Bandari kwa watu wenu ni Shirika lipi lingine mnafuatia kuliuza ili tujiandae ?

Nakulilia Tanzania .

View attachment 2652644
Tenesco ndo wameanza taratibu
 
Dp ilikataliwa USA kipindi cha G. Mushi kwa hoja za kiusalama hasa Ugaidi.
Umekuja na hili ?!!![emoji1787][emoji1787]

Kwa hiyo kila wanachokikataa US na kukipinga ni lazima iwe kweli kwa dunia nzima?!!![emoji15][emoji15][emoji1787]

Hivi ukiacha sisi tunaotumia bongo ninyi mnatumia viungo gani kufikiria ?!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ninachojua mimi Mzanzibari ni Mtanzania lakini Mtanganyika sio Mzanzibari. Hivo wazanzibari wana advantage ya kufaidi kote kote. Au mnasemaje wakuu 😀
 
Back
Top Bottom