Watanzania walioaminishwa na Hayati Magufuli kwamba wanaweza na nchi yao ni tajiri na wakaanza kujenga miradi ya matrillioni ya fedha kama ndege, SGR, bwawa la umeme, kuhamia Dodoma, elimu bure, madaraja marefu Afrika mashariki na ya kati etc, ghafla sasa upepo umebadilika viongozi wote wanahubiri watanzania hawawezi na hawajiwezi kwa lolote kabisa!
Bunge linasema kila kitu kipitishwe kwa sababu watanzania hawana uwezo wa kifedha wala akili ya kuendeleza miradi mikubwa kama ya bandari.
Wapo pia wanasema hata taasisi za bunge na urais nazo zibinafisishwe ili ziweze kutoa matokeo chanya na ya haraka kwa wananchi.