Kuna msemo wa kiingereza kwamba " the devil is in the details"!
Hii ndo sababu vi.laza wengi hawapendi details kwa sababu wanaogopa kukutana na shetani uso kwa uso!
Tumemsikiliza Profesa Shivji, Profesa Anne Tibaijuka, Dr.Rugemeleza Nshala, Tundu Lissu, Boniface Mwabukusu n.k .
At least naweza kusema hizo ni Big Brains tulizo nazo kama Taifa!
Sasa msitulazimishe sijui kuwasikiliza kina Zembwela, Maulidi Kitenge, Shehe 'Ubwabwa" Mwaipopo, Steve Nyerere , Majaliwa, Mbarawa na hata Sa100!
Hatutaki habari za kwamba wana nia njema na Taifa! Even the way to hell is paved by people with good intention!
Mkataba huo (Bogus Treaty) Rais kama ni msikivu na mwelewa asiusaini na aurejeshe Bungeni na wabunge waache ushabiki wa kiCCM kwani hata mimi ni mwana CCM lakini najua hii Nchi si mali ya CCM wautupilie mbali huo mkataba au kama Mbarawa na team yao wanaupenda watafute Bandari zao wawape hao Waarabu!
Tunachotaka Katiba yetu iheshimiwe, Uhuru wetu kama Taifa uheshimiwe ,sheria zetu zifuatwe na kama kuna haja ya uwekezaji katika Bandari zetu basi sheria za manunuzi zifuatwe na si kuletewa Bogus treaties!
Halafu wanaCCM tuache unafiki kwani ni jana tu hapa mwamba Hayati Rais Magufuli alikuwa akisema TUNAWEZA sote tulishangilia lakini ghafla chini ya Rais Samia HATUWEZI chochote!
Kama binadamu angekuwa anakufa halafu baada ya muda anarudi basi siku Hayati Magufuli anarudi tungeona wanafiki wanaomsifia Rais Samia sasa kuhusu Bandari zetu ambavyo wangemkimbia kwenda kumlaki Magufuli! Hili hata yeye Rais Samia anajua deeply kwamba hajatutendea haki kuwapa Waarabu Bandari zetu kienyeji hivi!
Chini ya CCM yetu, tumeuza madini, mbuga za wanyama, gesi n.k basi sasa tuone aibu kama tumeshindwa kununua tu cranes na systems za kuendesha Bandari tuziache wengine pia waje wakute cha kuuza!
Narudia kusema Mimi ni mwana CCM ila tujue hii Nchi si mali ya CCM!
Kwa hili la Bandari Serikali yetu ya CCM na Bunge la Tulia Ackson zimetutia aibu mbele ya Watanzania wenye maarifa!