Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Mnakumbuka baada ya ziara Dubai, " wanangu nimezunguka huko nikapata ... Zijenge madarasa 20 kila wilaya...."
Chawa wote " kapu la mama hiloo"
Tukatae aibu na ujinga huu
 
Serikali inapaswa isimame imara kwenye mambo ya msingi lwa masilahi ya wananchi.

sio watu wote watakubaliana na jitihada zinazo fanywa na Serikali za kukuza uchumi wetu.

wapingaji wapo na wataendelea kuwepo tu, jambo la msingi ni mbele kwa mbele
 
IMG_7588.jpeg
 
Wajua tunapo zungumzia bandari Kuna vijana hamwelewi

Tupo sisi ambao tulisomea karibu na Hiyo na Bandari tukiwa na matumaini ya kumaliza kazi tuombe bandari.

Hasikwambie mtu bandari lilkuwa lango zuri la upigaji FEDHA bhana,ukiachana na upigaji Bado pia ni miongoni mwa pahala palipo kuwa panalipa vizur sana.

Yaani wafanyakazi wangeacha tamaa,kuikataa RUSHWA hakika hayo yanayo kuja ya Dp yangelikuja ila sio kwa Leo.

Nina uhakika Kwa wizi RUSHWA na mambo mengine yaliyokuwa yanaendelea bandarini Bora tuwape DP World na hapo Nataka tuelewane hakuna anae wakataa ila mikataba ibadilishwe kidgo iboreshwe,

Lazima watanzania tukubaliane wizi na RUSHWA vikomeshwe

Sasa Kwa kuwa tumeona technologia ya namna hii ni vema Sasa tukubaliane yafatayo;

Jeshi la polisi libinafusishwe walau miezi 6 tu Ili nao wapunguzwe tulindwe ma maroboti Nina hakika yapo ya kulinda kama yapo ya kufanya nayo mapenzi Kwa Nini tukose ya kulinda?

Takukuru IBINAFSISHWE Nina hukakika tutapata roboti la KUKAMATA wara RUSHWA wachache.

Tiss inabinafusishwe wiki moja tu.

TRA nao wabinafusishwe Kodi ikusanywe na roboti halipokei RUSHWA linakuja kudai ukizingua unakula mbata mbili tatu mwenyewe unatoa pesa.

Mwisho nakubaliana na technolojia mijizi ya Bandari ifukuzwe tuajili roboti tu zitusaidie.
Screenshot_20230623-183408.jpg
 
HATUWAKATAI HAO WAARABU.

TUNACHOKIKATAA NI HUO MKATABA WA HOVYO KUWAHI KUTOKEA DUNIANI.

YANI NI VIPENGELE VYA MKATABA.
 
Mrisho mpoto amewashukia wale wanaosema kwamba Bandari ya Tanzania imeuzwa, akinukuliwa kwenye mtandao wa Twitter amesema

"Mnaosema tumeshasaini mkataba na kuuza bandari kwa DP naomba mnijibu;

1. Kama tushasaini, mbona DP World hawajaingia bado hapo bandarini? au mshasikia kwamba Watanzania wamefukuzwa Bandarini?

2. Kama tumesaini, mbona mnaendelea kujadili kana kwamba kuna kitu kinaweza badilika?

UKWELI: Hadi sasa kuna makubaliano kati ya Dubai na TZ, NDIO, lakini bado hatujasaini mkataba wa utekelezaji na Dp World.

Mnaendelea kujadili sababu mnajua Rais Samia Suluhu anawasikiliza, na kuna nafasi ya kurekebisha mkataba.
#mamaanafanikisha
"
 
Dr Mrisho Mpoto yupo sahihi
 
Back
Top Bottom