Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Ninyi wapumbavu si ndio mlikuwa mnafurahia hao makahaba wa mbogamboga na hao wa kununuliwa toka chadema kwa kuhongwa kuingizwa humo bungeni ?
Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.



======

Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023

UTOAJI HUDUMA HAUJAFIKIA VIWANGO VINAVYOTAKIWA KIMATAIFA
Prof. Mbarawa amesema: "Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”

“Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”

"Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

“Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa

MSINGI WA MKATABA HUU KUENDANA NA MIKATABA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Mkataba wa DP World kuendesha Bandari utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za Miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa Mikataba ya Nchi mwenyeji na Mikataba ya miradi

Amesema "Msingi wa Mkataba huu kuendana na Mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa Mikataba 10 Nchini."

KAMPUNI YA DP WORLD INA UZOEFU WA KUENDESHA BANDARI BARANI AFRIKA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema Kampuni ya DP World ina uzoefu katika uendeshaji wa shughuli za Bandari Barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini

Amesema "Baadhi ya Kampuni zilizowasilisha nia ya kuwekeza Bandarini hazina wakati Kampuni ya DP World inaendesha takriban Bandari 6 Afrika na Bandari zaidi ya 30 Duniani kote kwa ufanisi mkubwa.”

DP WORLD INATAKIWA KUENDELEZA AJIRA ZA WATUMISHI WALIOPO
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema “Uwepo wa ajira za Watanzania hususani Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao Nchi itaufanya.”

Amesema “Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za Watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma.”

TAUHIDA: KIONGOZI ANAYETAMKA KAULI ZA UBAGUZI TUNAMSHANGAA SANA

Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo amesema “Nikimuona kiongozi anayewaongoza watu anatamka kauli ya kibaguzi tunamshangaa sana, mimi natokea Songea, mama yangu ni Mzaramu lakini ni Mbunge wa #Zanzibar.”

Ameongeza “Serikali haikatai kukosolewa, ikikosolewa inafanya uboreshaji zaidi.”

MDEE: MKATABA WA DP WORLD UMETAJA VITU KIJUMLAJUMLA
Akizungumzia mkataba wa #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld, Mbunge #HalimaMdee amesema “Tuna nafasi ya kubadilisha baadhi ya vitu katika Mkataba huu lakini najua hatutabadilisha

Ameongeza “Kama Mkataba huu unagusa Mtwara, Tanga, Mwanza, Dar es Salaam na Kigoma kwani usizungumzwe kwa mapana yake? Tukiupitisha unaenda kuwa mkataba wa Kimataifa, chochote ambacho kimetajwa kijumlajumla kuhusu Bandari kitahusika.”


BOFYA HAPA KUSOMA: Maoni ya Kamati ya Pamoja Kuhusu Azimio la Bunge Kuridhia Makubaliano Kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali Ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii Kwa Ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji Wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023

RASMI: BUNGE LAPITISHA AZIMIO LA KUUNGA MKONO MKATABA WA TANZANIA NA DP WORLD
View attachment 2653047View attachment 2653047View attachment 2653047View attachment 2653047View attachment 2653047
Bunge limepitisha mkataba kuhusu Ushirikiano wa Tanzania na Kampuni ya Dubai ya DPWorld katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara, ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam

Sehemu ya Azimio hilo imesomeka, "kwa kuzingatia manufaa ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itayapata kutokana na Mkataba huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 11 na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, linaazimia kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi katika Bandari Tanzania"

Mkataba huo uliibua maswali kutoka kwa Wananchi ikiwemo thamani na muda wa utekelezaji
 
DP WORLD NI WAWEKEZAJI UCHWARA. NI WEZI ambao wameamua kushirikiana na Wabunge ambao ghafla wamekuwa makuwadi wao.
 
Unaweza kuishia kucheka tu[emoji1787]

Hivi ARAB CONTRACTORS tulioingia nao mkataba ambao haukupelekwa bungeni si WAARABU?

Hivi mkataba wa SGR na Yerpi Merkez ambao nao ni waturuki ulipelekwa bungeni kujadiliwa?!

Eti hawa waarabu wa Dubai walikataliwa MAREKANI kwa sababu za kiusalama....Ugaidi ?!!!

Dubai na Ugaidi wapi na wapi ?!!![emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kongole kwake mh.Rais SSH kwa kuithibitisha dunia kuwa DEMOKRASIA imetamalaki Tanzania.

Rais SSH anakuwa rais wa kwanza kuwa muwazi katika mikataba mikubwa.....

Mh.Chifu Hangaya ni mzalendo wa kiwango cha kupigiwa mfano.

Ataandikwa kwa wino wa dhahabu kama mwanamke wa shoka.

Uingereza wanamkumbuka IRON LADY "MAGRETH THATCHER"....Tanzania tunaye THATCHER wetu kutoka Makunduchi.

Mwezi wa 7 nitakwenda Makunduchi katika sherehe za MWAKAKOGWA(kuoga mwaka) nitambike na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa Rais mzalendo ,mwanademokrasia nguli ,msikivu ,mwenye huruma na maono.


#Kupitia DP WORLD ninajiandaa kuiona nusu ya bajeti ya nchi inapatikana kila "fiscal year"[emoji7]

Mwenyezi Mungu atuhifadhie mpendwa Rais wetu chifu Hangaya SSH ,amen amen amen[emoji120]


Mkunazi Njiwa
Kwa sasa kwetu Matema Kyela[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mnasingizia corona.

 

Attachments

  • ABF204E3-971D-4767-8EF2-B1340942E217.jpeg
    ABF204E3-971D-4767-8EF2-B1340942E217.jpeg
    65.5 KB · Views: 1
  • 161FBB1A-16FC-451A-854C-1E7A9B694739.jpeg
    161FBB1A-16FC-451A-854C-1E7A9B694739.jpeg
    64.5 KB · Views: 2
  • C1E4E6E1-1011-43A6-BC78-1FD20E8D37DD.jpeg
    C1E4E6E1-1011-43A6-BC78-1FD20E8D37DD.jpeg
    57 KB · Views: 1
Huu ujinga unaoitwa maridhiano toka mwanzo tulijua utatumika kama sehemu ya kutioana woga. Waliokuwa wanaona maridhiano ni kitu cha maana, hayo ndio masimango yake. Mbowe amekimbilia jambo lisilo na maana, saa wanamuona msaliti wa maridhiano uchwara.
 
Hahahaha,Nape ninaona upo kwenye kambi yako sasa.Magufuli alifanya vizuri kukukomesha.
 
Kuna kitu hakipo sawa kwenye hili Taifa na ni wakati wa kuamka sasa, Siku zote Raisi wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania ana dili na Tanzania Bara kama ndio Tanzania nzima, sijawahi sikia Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa hata kipande cha Aridhi Zanzibar kwa ajili ya uwekezaji fulani,

Hii maana yake Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hana mamlaka na aridhi ya Zanzibari ila ana mamlaka na aridhi ya Tanzania Bara tu.

Watanganyika Mungu atatushangaa siku ya kiama kama kweli opo, Mungu atatushangaa kiwango chetu cha ujinga tulicho kuwa nacho na kushindwa kutetea Mali za Babu zetu.

Kumbuka hizi Mali ni za Babu zetu walipigana na Mkoloni lakini leo hii sisu hatuwezi kuzilinda.


kuna sehemu niliona Mdau anauliza kwamba ni nani anaye simamia mali za Tanganyika kama Tanganyika? make Raisi ni msimamizi au mlinzi wa mali za Tanzania ingawa sana ana dili na mali za Bara tu, sasa vipi mali za Tanganyika?

Make bila Tanganyika kuwa na msimamizi wa mali zake tunaenda kuumia sana awamu hii, ni lazima sasa Tanganyika iwe na msimamizi wa mali zake ukiachana na za Tanzania nzima.

Vizazi vijavyo vitatushangaa kiwango cha ujinga tulicho kuwa nacho.
 
Tumechelewa sana, tuungane tuwe nchi moja kamili na serikali moja.
Baba wa Taifa alishagharamika sana kwa pesa za Watanganyika kuikomboa Zanzibar.

Operesheni ya kumuondoa Sultani Zanzibar.
Chama kilichoongoza Mapinduzi Zanzibar kilikuwa cha Mwalimu Nyerere.
AFRO-SHIRAZI ASP, Mama yake ni chama cha African Association mtoto wa Tanganyika African Association ya Mwalimu.

Alipounda AFRO-SHIRAZI usiku wa tarehe 5 February 1957 pale Rahaleo alikuwepo yeye mwenyewe Mwalimu akiongozana na katibu wa Zebuir Mtemvu.
Siku hio Mwalimu akamuajiri Abeid Karume wa Malawi na Thabit Kombo kuwa viongozi wa chama hicho.

Yalijaribiwa Mapinduzi mara 11 yakafeli kwa sababu ya watu kuvujisha siri kwa Sultani.
Hata yale 1961 waafrika wengi wakafungwa na waarabu na Mwalimu akawaletea wanasheria wazungu.

1963 Sultani akaomba Mamlaka kamili kwa mwingereza ili ajiunge kisiasa zaidi na nchi za Kiarabu apate misaada ya kupambana na Nyerere na Waafrika kwa ujumla.

October 1964 Waingereza wakaipokonya Mombasa na Pwani ya Kenya kwa Zanzibar kama maandalizi ya kumpa mamlaka kamili Sultani.
10 December 1963 Mtawala wa Uingereza anaondoka Zanzibar ili Zanzibar ipinduliwe na waafrika kwa msaada wa Uingereza.

8 January 1964 Meli ya silaha za kivita zakabidhiwa kwa Oscar Kambona Daressalaam ambae Kambona alikuwa ni mwingereza askari na Waziri wa Ulinzi wa Tanganyika.
Viongozi walioajiriwa na Nyerere kuongoza Mapinduzi wafichwa Tanganyika.

12 January 1964 Maaskari Waingereza weusi wenye asili ya Tanganyika na maaskari wa Nyerere waanza kazi wakitumia zana za kivita za kisasa, wakiwepo kina Ibrahim Makungu na Edington Kisassi mwingereza mwenye asili ya Moshi.

Vita viliendelea Waingereza wote wakiwa wamekusanyika kwenye hotel moja Mji Mkongwe Forodhani wakicheza na kulewa na kusherehekea kurudisha nchi kwa waafrika walioichukua 1836 walipomleta Sultani feki wa kwanza Sayyid Said tokea utumishi wa British India Company Mumbai.

halafu leo vinyani vimeletwa juzi tokea Congo na Tippu Tipp wanabana pua na kujiita wenye visiwa.
Serikali moja ndio dawa halafu wasukuma tuhamie Zanzibar tukale neema yetu.
 
Back
Top Bottom