Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Nimesikia kuhusu mkataba wa DP world na Tanzania nimesikia ni mkataba wa milele kuna mtu anaweza kutuma pdf ya mkataba huo humu? Nataka kusoma mwanzo mwisho kiunaga ubaga
Pdf tayari sasa leta maoni yako.
 
Mungu aingilie kati suala hili, wabunge wetu hawatabiriki.
Hili swala shida yake ni kwamba litamwinua mno Mama na hivyo mahasimu wake wa Oktoba 2025 ndiyo wanaofanya jitihada za kuchanganya watu, hawajafurahi. Bunge zima haliwezi kupitisha kitu ambacho kina tatizo kwa nchi

Ebu jiulize maswali haya. Kwani Serikali ya Mama ilikuwa anashindwa nini kuuingia mkataba huo kimya kimya tu kama ilivyowahi kuingiwa mikataba mingine kama vile ya SGR na ya Bwawa la Mwalimu Nyerere?

Kwa nini Serikali iamue kuingia mkataba usio na maslahi kwa nchi halafu wakati huo huo tena uipeleke Bungeni kwenda kujishtaki yenyewe? Ilikuwa inshindwa nini kuufanya bila kuupeleka Bungeni?

Tundu Lissu tayari ameshasema kuwa mkataba huu ni nyeti na ndiyo maana umepelekwa Bungeni, na baada ya hapo TL yuko kimya

Tutumieni akili ili tusiwe tunachanganywa na wanasiasa.

Kwa mkataba huu, Mama anatarajia kuwa anaingiza si chini ya TZS TRILLION 26 kwa mwaka kupitia Bandari peke yake, wakati sasa pato letu kupitia bandarini linakisiwa kuwa ni TZS TRILLION 2 (mbili) tu. Kwa kishindo cha aina hii, wewe mwenyewe utakuja kushuhudia ni nani atakayekistahimili kishindo hiki cha Mama come Oktoba 2025! Utaniambia ni nani atakayeweza kusimama na Mama
 
sasa akili yako yenyewe ipo hivo halafu mnauliza nani kawaloga,haya endeleen kumtafuta mchawi wenu
"Sasa akili yako ipo hivo"
Sidhani kama unaweza ona kosa kwenye hili, lakini eti na wewe unajadili mada za watu wenye akili, Jiwe sijui aliwapa nini nyie wanyonge
 
Hili swala shida yake ni kwamba litamwinua mno Mama na hivyo mahasimu wake wa Oktoba 2025 ndiyo wanaofanya jitihada za kuchanganya watu, hawajafurahi. Bunge zima haliwezi kupitisha kitu ambacho kina tatizo kwa nchi...
We nae walewale mikataba yote inayopelekwa bungeni ni kwa sababu haiendani na sheria za nchi so inapelekwa kule kwa watengeneza katiba (sheria).

Ni hivi hayo makubaliano kipengele kimoja wapo kinasema tatizo likitokea mwamuzi n msauzi na kwa sheria za uingereza yaaani sheria za watawala wetu wa zamani ni nini hiki?

Au tuseme kwa ligha rahisi wewe hapo uoe mwanamke aliyetalikiwa ila kwa masharti mkizinguana ex mumewe ndio awe muamuzi.
 
Hapa kijiweni kwetu kwa walalahoi tunapokunywa kahawa amekuja mgeni na kusema boss mkuu wa tiss aliondolewa ofisini kwasababu alikataa kabisa swala la waarabu kuuziwa bandari ikabidi achague heshima kuliko kuingia kwenye historia mbaya sana ya kuuza nchi

Wazalendo tunawasihi jitengeni na Hawa mafisadi majina yenu yaandikwe kwa wino wa dhahabu
 
Hapa kijiweni kwetu kwa walalahoi tunapokunywa kahawa amekuja mgeni na kusema boss mkuu wa tiss aliondolewa ofisini kwasababu alikataa kabisa swala la waarabu kuuziwa bandari...
Bongo ni kawaida mambo haya... Refer issue ya Assad. Ukisimamia misingi yako ya kaz au kukataa kushiriki jambo flan lisilo na maslahi lazima uondolewe!!
 
Hili swala shida yake ni kwamba litamwinua mno Mama na hivyo mahasimu wake wa Oktoba 2025 ndiyo wanaofanya jitihada za kuchanganya watu, hawajafurahi. Bunge zima haliwezi kupitisha kitu ambacho kina tatizo kwa nchi

Ebu jiulize maswali haya. Kwani Serikali ya Mama ilikuwa anashindwa nini kuuingia mkataba huo kimya kimya tu kama ilivyowahi kuingiwa mikataba mingine kama vile ya SGR na ya Bwawa la Mwalimu Nyerere?

Kwa nini Serikali iamue kuingia mkataba usio na maslahi kwa nchi halafu wakati huo huo tena uipeleke Bungeni kwenda kujishtaki yenyewe? Ilikuwa inshindwa nini kuufanya bila kuupeleka Bungeni?

Tundu Lissu tayari ameshasema kuwa mkataba huu ni nyeti na ndiyo maana umepelekwa Bungeni, na baada ya hapo TL yuko kimya

Tutumieni akili ili tusiwe tunachanganywa na wanasiasa.

Kwa mkataba huu, Mama anatarajia kuwa anaingiza si chini ya TZS TRILLION 26 kwa mwaka kupitia Bandari peke yake, wakati sasa pato letu kupitia bandarini linakisiwa kuwa ni TZS TRILLION 2 (mbili) tu. Kwa kishindo cha aina hii, wewe mwenyewe utakuja kushuhudia ni nani atakayekistahimili kishindo hiki cha Mama come Oktoba 2025! Utaniambia ni nani atakayeweza kusimama na Mama
Nitachelewa kuamini hili
 
Hapa kijiweni kwetu kwa walalahoi tunapokunywa kahawa amekuja mgeni na kusema boss mkuu wa tiss aliondolewa ofisini kwasababu alikataa kabisa swala la waarabu kuuziwa bandari ikabidi achague heshima kuliko kuingia kwenye historia mbaya sana ya kuuza nchi

Wazalendo tunawasihi jitengeni na Hawa mafisadi majina yenu yaandikwe kwa wino wa dhahabu
Hii ndio TZ ukiwa makin na maslah ya Taifa utapotea!
 
Yaani kati ya wa Tanzania milioni 60, tumeshindwa kujisimamia kuendesha bandari zetu, tunaenda kuwapa watu wasiozidi milioni 4 ili watuendeshee bandari zetu. Maana yake kati ya watu milioni 60 hakuna watu wenye akili timamu wa kuweza kuendesha bandari kwa ufanisi, lakini kati ya watu wasiozidi milioni nne kuna watu wanaoweza kusimamia bandari kwa ufanisi.
Kigezo kikubwa eti wanaendesha bandari Uingereza.
Kwangu mimi hii ni dharau kubwa sanaa.

(Sensa yao 2023, wapo 3,564,931)
 
.
20230607_003514.jpg
 
Back
Top Bottom