Dodoma City vs Arusha City (The Battle of Tanzania Capital City vs EAC Capital City)

Hoja dhaifu Sana hii
 
Embassy zitakujaje wakati hakuna Airports na miundombinu mingine muhimu?

Nigeria iliweka Nguvu kubwa Abuja ila sisi hapa Tanzania Serikali inajivuta vuta.

Kwa hiyo mambo yatajipa
 
Nani anaweza kuishi kwenye lile vumbi la Dom nilikaa pale siku mbili kwakweli nilishindwana na vumbi
 
Nani anaweza kuishi kwenye lile vumbi la Dom nilikaa pale siku mbili kwakweli nilishindwana na vumbi
Dom ndio Third largest City in Tanzania in terms of population.Una swali jingine au wivu ndio unakusumbua?
 
Nani anaweza kuishi kwenye lile vumbi la Dom nilikaa pale siku mbili kwakweli nilishindwana na vumbi
Tutajie barabara yoyote ya vumbi uliyokaa kwa hizo sikumbili.....hakuna mji wowote Tanzania unaogusa hata pua kwa jiji la Dodoma lenye lami kila kona hadi ndani ndani huko Nkuhungu. Wadanganye wenzako ambao hawajawahi kufika Dom City
 
Huko ambako sio planned mara ya mwisho umesikia lini [emoji53]
Rudi shule aisee...umewahi kusikia popote tukio la ujambazi au wizi mkubwa ndani ya jiji la Dodoma?? Jiulize ni kwanini.Miji mingine yote mikubwa ya Tanzania ujambazi ikiwemo wa kutumia silaha ni kawaida sana.
Dom City is the only safest city in East and Central Africa(ukibisha uje na facts kama hizo apo juu)
Na hiyo yote inatokana na ubora wa mipango miji. Mji umepangiliwa kiusalama ndiomana hata majambazi wanaogopa kufanya uhalifu watakamatwa kiulaini tu.
Just imagine ufanye ujambazi katikati ya jiji utakimbilia njia ipi ...main roads zinajulikana,feeder roads zimepangiliwa hakuna vichochoro wala makazi ya ovyoovyo,kila upande wa Jiji kwamfano kuna kambi za Jeshi Ihumwa-njia ya Dar,Makutupora-njia ya Arusha,Msalato njia ya Arusha na Singida,Kambi ndogo ya Jeshi Ntyuka-njia ya Mvumi n.k
 
Mkuu mbona hueleweki ...manake sioni changamoto yoyote unayoitaja exactly kuhusu ukuaji wa jiji la Dodoma. Maendeleo ni continuous&sustainable process sio suala la sikumoja.
So far mpaka sasa Dom inashika nafasi ya pili kwa ubora na ukuaji wa majiji Tanzania baada ya Dar na vigezo ni vilevile ambavyo Arusha na Mwanza hawafiki hata robo kwamfano
1.ubora wa miundombinu
2.ubora wa mipangomiji
3.ubora wa huduma za kijamii
4.uwekezaji mkubwa wa serikali
Just imagine Dodoma ilipewa hadhi ya Jiji 2017....miaka mitano baadae spidi yake huwezi kulinganisha na Mwanza iliyopewa mwaka 2000 au Arusha
 
Unachekesha sana mkuu eti mji hauna ukuaji👇👇
-makao makuu ya serikali(Executive)...ofisizote,taasisi,wizarazote za serikali
-makao makuu ya chama
-makao makuu ya Bunge
-makao makuu ya Judiciary

Kwenye upande wa ubora wa mipangomiji Dodoma haina mpinzani yoyote East and Central Africa .Dodoma inafuata master plan ambayo imetengenezwa kuaccomodate miaka 100 mbele huko refer barabara za Ring Roads....yaani hata mji ukue vp haitakuja kutokea changamoto ya mipangomiji kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na CDA from the scratch.
 
Tukuletee takwimu??
 
Tukuletee takwimu??
Leta takwimu za kipolisi...
-umewahi kusikia tukio lolote la ujambazi au wizi mkubwa ndani ya Dodoma Jiji
-Mara ya mwisho kumuona kamanda wa polisi Dodoma akitangaza tukio lolote la uhalifu lini
 
..mkuu swali zuri kuhusu changamoto zipi za ukuaji wa dom...changamoto kubwa ni uzembe wa wenyeji wa dom kushindwa kujiongeza na kuchangamkia fursa...uzembe wa wenyeji umeshindwa kuwavutia wageni (watz kutoa maeneo mengine)...wenyeji wana sehemu kubwa sana ya kuchochea ukuaji wa mji...kuna wageni wamejaribu kujenga hotel nzuri tu hapo dom lakini kwasababu zilizo wazi wameajiri baadhi ya wenyeji ambao wamepelekea hotels kuwa na huduma mbovu kwa kutojiongeza!

..dom ni mji pekee wenye hadhi ya capital city ukanda wa afrika mashariki ambao ikishafika saa mbili usiku unakua umelala...sijapata kuona mji ambao watu hulala mapema na kuchelewa kuamka kama dom kwa hadhi ya capital city!..sababu nyingine ni za kimazingira ambazo zitachukua miaka mingi sana kuzibadilisha kwa uzembe wa wenyeji.
 
..mkuu hakuna barabara za ring roads zinazoweza kukidhi mahitaji ya capital city kwa miaka mia ijayo..hakuna..miji mikubwa ilishatoka huko kwa ring roads miaka zaidi ya 50 iliyopita...wenzetu tena majirani tu hapo walishajenga flyovers, expressways, etc..hapo nairob tu kuna expressway yenye urefu wa 27km..yaani unatembea 27km hewani bila kushuka chini...sasa utalinganisha na ring-road?watu walishajenga na wengine wanamipango ya underground tunnels za trains (subways)..hizi ndio mambo za kukaa miaka mia sio hizo ringroads mkuu!..tembea utaona mengi mkuu but dom bado sana maana toka imeanza kuwa capital city 49yrs ago haikutakiwa kuwa ilipo sasa.
 
-nimeishi na kufanya kazi halmashauri zote 8 za mkoa wa Dodoma ...Warangi,Wasandawe,Wanguu,Waburunge,Wasagara,Wanyambwa,Wakaguru hawana sifa ya uzembe wala uvivu.Ukienda pale sokokuu la Majengo Wanguu wametawala biashara pale,ukienda maduka ya One Way Warangi wametawala pale hadi kuna mitaa inaitwa ya Warangi.
-Hizo hotels unazosema zina huduma mbovu ni zipi ebu tutajie kama ni Royal Village,St Gaspar,NAM,DearMama,DM,Golden Crown,Miramonti,Dodoma Grand,DodomaHotel,Morena,African Dreams,Midlands,Karibu Rafiki,Nasheera au Bestern Western City Hotel(5 star hotel in Dom)
 
Mkuu naona unachanganya mambo Dom ilipewa capital status 1974 ikiwa na population ya watu elfu 40 tu,mwaka 1980 ndio ikapewa hadhi ya manispaa na ikapewa city status 2018.Dom ilipopewa capital status iliwekwa chini ya uangalizi wa CDA na kulikua na changamoto nyingi za kifedha pamoja na kutokua na nia thabiti ya serikali kuhamia.Kuanzia 2018 ndio hapa tunaweza kusema kiuhalisia mambo yalianza kupush kuelekea lengo halisi.
Ukifuata hizo facts nadhani kulinganisha Dodoma na majiji ya nje ya nchi sio sawa utakua unaionea tu....lakini ukilinganisha kibongobongo hapa Dom City is much better kuliko majiji yote.Kwa mfano kigezo hicho kimoja tu cha mipangomiji ukifika Dodoma nyumba zote zimepangiliwa(hairuhusiwi kujenga bila kupitisha kwanza ramani yako kukaguliwa CDA/Jiji,Paa la nyumba au jengo lako linatakiwa kufuata rangi iliyowekwa kwa kila mtaa) ujenzi holela ni kiwango kidogo sana .Mitaa ambayo unaweza kuiita uswahilini labda baadhi ya maeneo ya Chang'ombe,Kizota,Mkalama na Chadulu lakini kwingine kote kumepangwa vizuri huwezi kulinganisha na mji wowote Tanzania.
 

Sijajua, ofisi za atomic hazipo tena Arusha? Majengo yao pale wanayafanyia nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…