Dodoma: Kijana afariki kwa kukanyagwa na treni akiwa anasikiliza muziki

Dodoma: Kijana afariki kwa kukanyagwa na treni akiwa anasikiliza muziki

Labda siku yake ilipangwa iishie hivyo..maana inaonekana ni mwenyeji wa maeneo hayo na alifahamu kabisa kwamba reli ile inatumika. Apumzike kwa amani.

Ujumbe uwafikie wale wanao tembea barabarani na ear plugs
 
Daah kuna haja sasa nipewe tenda ya kuzungushia reli uzio au nipewe tenda ya kusambaza vijana maeneo reli inapopita kufunga maspika ya matangazo ya tahadhari.may his soul rest in peace
Nadhani ungepewa ya kulinda kabisa maeneo yote... Huyu ndugu yetu aliamua kukaa relini ili apate hisia ya alicho kuwa anakisikiliza
 
Kama kutafanyika uchunguzi sahihi itajulikana ukweli wa kifo hicho sio treni, inawezekana ameenda kuwekwa relini akiwa ameshakufa.

Kutosikia honi kwa sababu ya earphone haiwezekani, honi ya treni ina sauti kubwa sana, pia wanasema alikaa relini, vibration kwenye reli ni kubwa treni ikiwa karibu
 
Hivi kuna earphones za maskioni zina sound waves kubwa kuliko honi ya treni?
 
Mkazi wa Mtaa wa Ndejengwa jijini Dodoma, Laurent David, amefariki dunia baada ya kugonga treni ya mzigo akiwa eneo la reli.

Inaelezwa aliaga nyumbani kwamba anaenda kufanya mazoezi.

Ajali hiyo imetokea leo, Jumamosi Desemba 30, 2023 saa 12 asubuhi kwenye Reli ya Kati. Laurent inaelezwa alikuwa amekaa juu ya reli akisikiliza muziki kwenye spika za masikioni, hivyo hakusikia honi za treni.

Athumani Sweya, aliyeshuhudia tukio hilo amesema aliiona treni ilipokuwa inapita na ilipiga honi lakini kijana huyo hakusikia.

Anasema alipotaka kumsukuma ili atoke relini treni tayari ilikuwa imeshafika na kuigonga.

David Zabron, baba mzazi wa Laurent, akizungumza akiwa eneo la tukio amesema kijana wake aliondoka nyumbani saa 11 alfajiri akisema anaenda kufanya mazoezi uwanjani.
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa, unakaa juu ya reli na earphone amevaa. Halafu hizi lugha ya kusheria eti "aligonga treni", wanasheria mwogopeni Mungu
 
Tena? Maana miaka kadhaa iliyopita mwingine aligongwa hivyo hivyo relini dar akitembea kwenye reli na earphone masikioni. Na wale wanaotembea barabarani huku wakichati kwenye simu zao bodaboda zitawamaliza
Hakugongwa na treni, aliigonga treni
 
Huyu jamaa huenda pia alikua na nia ameogopa kujipiga kitanzi !! Lile dude lilivyo na kishindo yana mita 300 kabla ya kukufikia ile chuma inakua inatikisika balaa na honi yake hata ungeweka sauti hadi mwisho itakustua tu asee !!
 
Sometimes treni hazipigi honi hta zikipita maeneo ya makazi, inawezekan huyo dgo aliweka saut had mwsho na concentration yke ilikua kweny mziki hta hakusikia vibration, ila angekua anasikiza habar au mawaidha uislam/ ukristo, i hope angesikia vibration.. sijui alikua anasikiliza mziki gan? Amapiano!!
 
Huyu jamaa huenda pia alikua na nia ameogopa kujipiga kitanzi !! Lile dude lilivyo na kishindo yana mita 300 kabla ya kukufikia ile chuma inakua inatikisika balaa na honi yake hata ungeweka sauti hadi mwisho itakustua tu asee !!
mwamba ka commit suicide huyo. alidhamiria kugongwa. ushahidi wa mazingira
 
Kwa kuwa treni haziwezi kusimama haraka, zitengenezewe ngao(kifaa maalumu) mbelevya kichwa kitakachokuwa na uwezo kuzoa mtu bila kumdhuru na kumtupa pembeni au kumbeba.

Nakazia tu, Treni huwa inagongwa ila haigongi hata kama mtu atakayeigonga alikuwa amelala.
 
Back
Top Bottom