benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amemtembelea na kumjulia hali Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dk Festo Dugange ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari.
Habari toka vyanzo mbalimbali zinaeleza Dk Dugange alipata ajali hiyo usiku wa kuamkia Aprili 26, 2023. Hata hivyo, mpaka sasa si Jeshi la Polisi wala viongozi wa wizara yake waliokuwa tayari kuthibitisha kuhusua ajali ya kiongozi huyo.
Kwa mujibu wa picha ya inayomuonesha Makamu wa Rais akiwa hospitalini, Naibu Waziri huyo amevunjika mkono wa kulia.